Mitsubishi Pajero iO (GDI) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitsubishi Pajero iO (GDI)

Discussion in 'JF Garage (Magari na Vyombo vya Usafiri)' started by Exav, May 28, 2010.

 1. E

  Exav Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Habari za leo wana JF!

  Nina nia ya kununua gari dogo la kunisaidia kwenye mizunguko yangu ya maisha. Nafikiria kununua Mitusbishi Pajero iO (GDI), lakini kusema ukweli sifahamu uzuri na ubaya wa aina hii ya magari. Kama kuna anayefahamu/wanaofahamu naomba a/wa-nisaidie, sitaki kukurupuka. Unaweza pia kurecommend aina nyingine unayoimani kwa ubora.

  Natanguliza shukrani za dhati sana.
   
 2. m

  muafaka Senior Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Evax

  Ningeshauri ueleze ni jinsi gani unatarajia kulitumia, katika mazingira gani, matarajio ya aina ya mizigo, concern kuhusu fuel consumption, whether you need 4WD or not, petrol engine or Diesel etc. Itakuwa rahisi kupata ushauri na wenye uhakika. Thats my advise
   
 3. E

  Exav Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mkuu Muafaka,
  Nashukuru sana kwa maelekezo yako. Nia yangu ni kwa matumizi ya safari za kawaida, hususan kwenda kazini na kurudi nyumbani. Pia kama kukiwepo na safari zingine za kawaida ndani ya DSM litatumika pia. Sina mpango wa kulitumia kwa safari za mbali zaidi ya umbali wa (mfano) Dar-Morogoro. Ni kwa ajili ya kubeba watu tu, siyo mizigo. Ila si unajua kuna vile vimizigo vya kawaida mfano. umetoka kazini ukapitia vyakula sokoni au umeenda kumpokea mtu mfano Ubungo then ukapakia begi lake kwenda nyumbani n.k. Ningependa engine size isizidi 2000cc. Fuel inaweza kuwa petrol au diesel. Preferably 4WD.

  Natanguiza shukrani za dhati sana.

  Exav
   
 4. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Exav, pajero io nsio nzuri sana kwani hata mitsubish japan walisema zilikosewa na sasa hawazitengenezi tena so spear parts zitakuwa shida sana, usione hao walizo nazo sema watafanyaje walishaingia mkenge.Mi nashauri sana kama unaweza pata Suzuki Vitara (Escudo) ni nzuri, cc zake ni kama 1800 hivi na fuel consumption ni minimal.
   
 5. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2010
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Exav na Tonge , Mimi nilinunua hiyo gari 2007 mpaka leo ni nzuri sijagusa chocho zaidi ya Pancha tu na Matairi yote yaleyale toka Japan na Spare tyre sijaitumia bado ,wengine nasikia wananiambia gari yako vipi haikusumbui nawaambia hawaamini , lakini mimi kwa upeo wangu Japan kuna magari mengi tu aina ya hiyo GDI Jipinde nunua gari isiyozidi Km 40,000-50,000 itakuwa bado bomba lakini ukinunua 80,000- 100,000 baada ya muda itakuwa shida tusinunue magari yaliyotembea sana , na spare zipo nyingi maana gari hizo sasa zipo nyingi ,ila zinaibiwa power window sana , Otherwise ni gari nzuri na Sasa nimemuachia Wife na bado iko bomba saana tuu!
   
 6. E

  Exav Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Asante sana Mkuu Tonge.
   
 7. E

  Exav Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Asante sana Mr. Endaku's kwa uzoefu na ushauri wako.
   
 8. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Aksante mkulu, anyway mi sina pajero io GDI ila kuna wakati nilitaka kununua ndio nikapata hizo cautions toka kwa mafundi, mi nina starlet ni ndogo but bomba mbaya bwana hii gari, familia ikiongezeka nitanunua gari kagari kakubwa.
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Pajero iO si nzuri sana; Na kwa mji weu wa Dar ulivyo na foleni nakushauri uchuke hata Toyota duet; cc 900! aaah na huu mfumuko wa bei za mafuta wewe utapeta tu! Na mizigo midogo utabeba tu bila shida; Ila kama huko Morogoro ni moja ya kazi zako; Fikiria gari kubwa Mzee; kwa usalama wa barabarani si vizuri hata kidogo kutembelea hivi vigari vidogo.
   
 10. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Mimi nimekuwa na gari kama hiyo kwa muda wa miaka mitatu sasa, ni gari nzuri kwa kweli.

  Shida mafundi hawana uhakika with what is going on with that car. ni mafundi wachache sana ambao wako tayari kujifunza mambo mapya mafundi wanaojua hizi gari ni wachache sana.

  Pili spare parts zake ni bei ghali kidogo ukilinganisha na magari mengine tuliyoyazoea. nakushauri kabla haujanunua nenda kwenye maduka ulizia bei za vitu kama shock absober, brake linnings and pads, spark plugs kama ni petrol engine bushes na hivi naongelea genuine parts halafu utaweza kufanya maamuzi naitakuwa bora zaidi kama utaweza kutafuta mtaalamu akakupa mwanga zaidi
   
 11. B

  Bizzly Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ni kweli kabisa mafundi wanaozielewa hizi mitsubishi ni wachache, kuna siri moja ambayo mafundi wakiigundua utengenezaji wake hauwapi tabu. mimi binafsi sina hiyo pajero isipokuwa kuna wakati nilikuwa naongea na fundi wangu nikimwomba ushauri kuhusu hilo gari aliniambia hiyo gari kuna baadhi ya system inabidi wazi disable ndo inatulia lasivyo itakusumbua. kwa ujumla mafundi wengi wana recommend Suzuki escudo kuwa ni gari nzuri, na haina gharama sparewise.
   
 12. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  fyi: Ukiagiza gari jiapan, Kama imezidi 100,000kms. Lazima ifanyiwe full overhaul. yaani unawekewa kila kitu kipya. did you know that?
  GDI ni gari nzuri sana!! Very very comfortable Car. Sitting at the fdrivers gives you a comfortability that you can never get in most of the avarage price cars.

  Kama wachangiaji wengine walivyosema. Mafundi wa kitanzania wanaogopa sana haya magari. Tatizo kubwa misi. Hizi misi zinasababishwa na Plug feki. Plug ya kawaida ni Tshs.7,000. Lakini ya ile gari ni 30,000. sasa mtanzania lazima atakimbilia kwenye 7,000. hapo shughuli ndio inaanza. hizo misi utatamani kuliacha gari kwenye foleni utembee kwa mguu.
  Pia hii gari utafurahia sana kama utatumia unleaded petrol. Nyonya mafuta BP, GAPCO na TOTAL.
  Nilikua na gari kama hii nikapata tatizo kidogo nilipo peleka kwa fundi, nakuambia hizo story alizonipa nilitoka pale nikamuuzia m2 for 8.5m, Gari ambayo nilinunua 12m withi just two months. Mpaka sasa namuona shosti yangu anadunda nalo tu.

  Go ahead and buy that car.
  Kama unaagiza andaa kunzia 8.5m to 12.5m utapata gari nzuri tu.

  Tcheerz.
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  I dont advise you to go for this. I had one but due to its intricases, I sold it out. Hizi gari kwa umbo ni nzuri na confortable hata kuendesha japo hazina speed sana, lakini zina mfumo wa umeme ambao mafundi wengi hapa bongo hawaujui. Hii gari ikifa kitu chochote cha umeme, unaweza kupaki uani. Mwaka jana zilikuwa zina uzwa kati ya TZS 12 - 15 mil, na hata ukiagiza Japan utalipa wastani wa kiasi hicho hicho hata leo, ila kutokana na ubovu huo hapa bongo wamezistukia na zimeshuka thamani mpaka TZS 7 mil (unaenda show room unalipa unaondoka nayo).

  Really, the final decision is your but I dont advise.
   
 14. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Duu Mkuu naomba hizo Show room zilipo nikatungue kwa ml 7 maana naweza fanya biashara hapo please !
   
 15. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2010
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
   
 16. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Where can I get that car at That Price maan. please do me a favour.
  Ila jamani. siku hizi watanzania katabia kakutumia magari halafu wanapeleka show room. Am sure hizo ndo zinauzwa 7m!!
  M2 jamani Auze GDI 7M showroom! kwani yeye atakua ameagiza kwa shilingi ngapi?
  When the deal is too good think Twice mamen
   
 17. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Maskini, huwezi amini mimi nina starlet sio new model ila ni ile ya nyuma kidogo, ni ya 1999.Nimesafiri nayo kwenda mbeya, mwanza na arusha mara kibao, Kaka hii gari ni save barabara kubwa kuliko escudo na pajero io.Kwanza inakaa barabarani ikikimbia inakuwa nzito kama benzi ila escudo na pajero ziko juu hupea kunoma na unaweza kuacha njia ukikumbwa na upepo wa basi kubwa au roli na pia ukikata kona kali kwa haraka zinahama barabarani, kwa duet sijawahi endesha ila ukiwa na starlet funga spoti rim na tyre pana kitu inatulia mbaya, shida ni huo udogo tu ila iko poa rodini.
   
 18. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,946
  Likes Received: 21,069
  Trophy Points: 280
  duh si mchezo.
   
 19. E

  Exav Member

  #19
  May 29, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru wote mliotoa michango yenu ya mawazo na uzoefu kwenye maada hii. Ukweli nawashukuruni sana wote na MUNGU aendelee kuwabariki. Nathamini sana mawazo yote mliyoyatoa na naendelea kuyafanyia kazi kama mliyonishauri na kunielekeza. Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, nimeanza kufikiria RAV 4 na nahisi aina hii ni nzuri (sina ushahidi). Mwenye uzoefu na aina hii anielimishe. Ikiwa aina hii ya magari itaonekana ni bora, nitaanza kutafuta mwenye RAV 4 ya kuuza tutawasiliane kwa exav@live.com au hapahapa jamvini - kadri atakavyopenda. Nitapenda iwe na hali nzuri, mileage at most 100,000km, engine size at most 2000cc, milango 5. Kwa ujumla isiwe na matatizo.

  Natanguliza shukrani kwenu.
   
 20. j

  john gharish Member

  #20
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Hello,ukweli pajero io ni bomba sana.ila mafundi wengi hawajui jinsi gani mfumo unafanya kazi.kosa kubwa watu wengi wanafanya ni kutembelea taa ya mafuta inawaka ni kosa lajinai kwa pajero io.kama utahijai ushauri wa kiufundi.piga simu ,0755399613,0715399613.niko dar es salaam.pia spare zinapatikana.napenda kuwambia wanajamii wote pia tumeongeza vifaa vya kupima magari yote madogo na makubwa(light cars and Trucks)diagnostic tool,AUTOCOM DIAGNOSTIC.KTS 540 DIAGNOSTIC TOOL.TUKO TABATA SHELL KUELEKEA ST MERRY..KARIBUNI
   
Loading...