Kuna fundi alikuwa ananishonea nguo alikuwa architect by professional. Alikua na kipaji cha ubunifu alitaka kujifunza kushona baada ya kumaliza form six akiwa amepasua. Baba yake ambae ni mwanasheria nguli alimwambia hakulea fundi charahani.
Bidada alipiga course yake safi, alipomaliza alimwambia mzee nimefanya ulichotaka sasa niache ninfanye ninachotaka.