kwandikwa
Member
- Dec 9, 2016
- 5
- 11
SERIKALI TAZAMENI KWA UNDANI SUALA HILI:
Tusaidieni tafsiri ya sheria hizi.
1. "The Medical, Dental and Allied Professionals Act, No. 11 of 2017"
2. "The Medical, Dental and Allied Professionals (Internship) Regulations, 2018".
3. "The Medical, Dental and Allied Professionals (Inquiry) Regulations, 2018".
4. "The Medical, Dental and Allied Professionals (Continuing Professional Development) Regulations, 2018".
5. "The Medical, Dental and Allied Professionals (Examination and Registration Procedures) Regulations, 2018
Kwa mujibu wa mrejesho wa kikao cha Baraza la Madaktari Tanganyika kilichofanyika Mwaka 2020, kiliazimia kuwafanyisha mitihani wanafunzi wanaomaliza masomo yao Katika Vyuo mbali mbali. Mitihani hiyo ya Pre-intern na Post-intern (yaani kabla na baada ya mafunzo tarajali). Na Katika ufafanuzi ambao umepatikana ni kwamba suala hili lazima lipewe mkazo Sana maana siku hizi madaktari hawajui hata kuweka Iv Line (iv cannulation). Kwa mtazamo huu Rais wa chama Cha madaktari Tanzania alionyesha Kuwa Kuna wahitimu wengi ambao hawana skills ya udakatari (alipozungumzia suala la mhitimu mmoja kushindwa kuweka iv line).
Mimi ninachofahamu Ni kwamba Baraza la Madaktari Tanganyika(MCT) na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) hushirikiana pamoja kwa kukagua na kujiridhisha ubora wa Elimu ambayo hutolewa vyuoni. Elimu ya udakatari kwa ngazi ya shahada ya Kwanza hutolewa kwa muda wa si chini ya semista 10 na si zaidi ya muda wa semista 14 na Katika kipindi hiki chote vyuo hutakiwa kuhakikisha kutoa mafunzo kwa mujibu wa Curriculum zao ambazo zimekuwa approved na TCU(kwa kushirikiana na Baraza la Madaktari Tanganyikwa Moja kwa Moja ama indirect).
Mwanafunzi kufika mpaka anamaliza chuo Ni kwamba amefanya mitihani ya masomo yote yanayomuandaa Kuwa daktari na kwamba kufaulu mitihani hiyo ni kukidhi Kuwa daktari!. Mitihani hiyo hutungwa na members wa Baraza la Madaktari Tanganyika, yaani walimu ambao wengi wao Ni Madaktari na wanachama wa Baraza la Madaktari Tanganyika hutunga mitihani hiyo. Bado ninajiuliza Kuwa Kama Baraza limeamua kuanzisha mitihani hii(ya pre na post intern) Nini maana yake?
Ni kwamba hawawaamini walimu(ambao pia ni wanachama wa Baraza Hilo) ama vyuo vya wanafunzi Hawa? Au Baraza haliwaamini wanachama wake ambao kimsingi ndiyo walimu wa wanafunzi Hawa!. Wanachama wa Baraza ndiyo wanahusika Kama external examiners kwa mitihani ya Clinical Exams na Oral Examinations, wanam-approve mwanafunzi Kuwa kafauru, then hao hao wanakuja kusema hatuna uhakika na Elimu yake, tuna mashaka nayo.
Sikatai Kuwa hakuna tatizo la wahitimu wengi Kuwa hawako vizuri Katika skills, lakini tuangalie kiini Cha tatizo, Kama wanafunzi hawajui vitu na wamefaulu kwanini tusiseme tatizo ni la mwalimu?(Na Hapa Kuna harufu yw Rushwa).
Kuna wazazi huko wameuza ng'ombe, mashamba na mazao mengine ili mtoto apate Elimu, halafu kwa sababu ya uzembe na ubinafsi wa watu wachache ndiyo usababishe hatima ya mtu hutu kutokufikiwa. Mh Rais ambaye amekulia Katika mazingira ya familia za chini/kawaida anaifahamu Hali hii, jinsi ambao wazazi wanaweza kupambana kumsomesha mtoto, yeye anaweza pia kuguswa na Jambo hili maana anayajua maumivu na mapito ya namna hii.
Huwezi ukamfundisha mwanafunzi, ukampa mitihani yote na ukaleta external examiners wakamfanyisha mtihani halafu akafauru bado unasema ha-qualify, Hana skills.
Tusidanganyane, udaktari Ni mgumu Sana na Ni kozi nyeti Sana, huwezi test understanding ya mwanafunzi kwa maswali 500 hata kwa kozi mojazndiyo maana kwenye miaka ya clinicals Kuna junior clerkship rotation na senior clerkship rotation. Huwezi kumu-assess mwanafunzi kwa maswali 150 Tena ya MCQs kwa kozi sijui nne basic.
Mimi nafkr Kama Kuna tatizo Ni vyema kusolve mzizi wa tatizo na siyo kuanza kupambana na tatizo huku mizizi ukiiacha.
Nalishauri Baraza kuanza kutatua mizizi ya tatizo na siyo matokeo ya tatizo, haiwezekan serikali imsomeshe mwanafunzi kwa miaka mitano imlipie Ada, fedha ya kujikimu, tafiti na mahtaji mengne halafu anapelekwa pelekwa tu bila kujua vitu halafu mwisho wa siku unasema hajui hivyo afanye mitihani Kwanza. Inasikitisha Sana, uzembe wa wakufunzi na kutafta maslahi Kuna tufikisha hapa.
Naiomba serikali kuingilia Kati na kuchunguza vitendo hivi wmbavyo ndani yake Kuna harufu ya Rushwa na vimelenga kuwakandamiza watu wa hali ya chini.
Serikali inatumia pesa nyingi kufadhili wanafunzi Hapa nchini, hivyo Yeyote anayechangia kuzorotesha ubora wa Elimu hiyo Ni lazima ashughulikiwe, hawezi mh Rais Dkt John Pombe Magufuli kupambana kutafta pesa wanafunzi wasome halafu watu wachache kwa maslahi yao wa-compromise na quality ya Elimu hiyo halafu wanalipwa na fedha.
Mh Waziri wa Elimu na waziri wa Afya Kama watahitaji Clarification juu ya Jambo hili nikotayari kutoa Clarification hiyo.
Ni Mimi niliyesauti ya wanyonge wanyongwao.
Email: ayubumathi1@gmail.com