Mitihani ya kidato cha nne imemwagika kama si kuvuja?

pcman

JF-Expert Member
Oct 9, 2008
742
186
Ndugu wana JF,

Jana nilipata bahati ya kuwahoji baadhi ya vijana wanaofanya mitihani ya kidato cha 4.Hawa vijana wakaniambia mitihani imevuja, paper kama ya histori na biology walizopata nje ndizo wlizozikuta ndani ya chumba cha mtihani. HIVI TUNATENGENEZA TAIFA LA NAMNA GANI?
 
Maghembe ameomba miaka mitatu zadi aboreshe shule (majengo) hana habari na viwango vya elimu ndo maana vijana wanasaka kuiba mitihani. Ah!!
Kama elimu yenyewe ndo hii walah tumiliwa kweupeeee
 
Linatengenezwa Taifa la Walaghai, wezi na wazandiki. Hali iko vivyo hivyo hata 'University'. Tunapata Maprofesa feki ambao hata ukimuhoji huyo profesa kuhusu uprofesa wake alizamia jambo lipi hawezi kujibu maana wengi wanapata uprofesa kwa kupublish kutoka kazi za wanafunzi wao. Hii ni aibu katika sekta ya Elimu na ni 'time Boom'. litalipuka wakati ukifika.Mungu Ibariki Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Inabidi Dr Slaa alipue kama kawaida, maana mtot aliye kijijini huko, hayo mambo ya kuiba paper hawezi kupata!! kwa hiyo watoto wa fisadi wanafaulu tu kwenda bila hata jasho. JK apumzike jamani, nchi imemshinda.
 
Ndugu wana JF,

Jana nilipata bahati ya kuwahoji baadhi ya vijana wanaofanya mitihani ya kidato cha 4.Hawa vijana wakaniambia mitihani imevuja, paper kama ya histori na biology walizopata nje ndizo wlizozikuta ndani ya chumba cha mtihani. HIVI TUNATENGENEZA TAIFA LA NAMNA GANI?

Rushwa na ufisadi vinaanzia mbali jamani.

Wanaoiba mitihani leo, siku wakiwa viongozi tutarajie nini?
 
Tuko bize na kampeni za uchaguzi, wacha tu paper zivuje watajijua wakienda A level.Hahahahaaaaaaa:A S 13:
 
Wakuu ivi inakuwaje kampeni zilisimamishwa kupisha mitihani ya darasa la saba, ilhali kwa hii ya kidato cha nne zinaendelea kama kawaida?
 
Tangu mwaka 1991/1992 mitihani kuvuja ni jambo la kawaida tu!

Ni sehemu ya kuongeza pato la wafanyakazi wa sector ya elimu kama ilivyo kwenye sector ya siasa wakati wa zoezi la uchaguzi!
 
Kuna breakin' news hapa?!

Naomba nitajiwe mwaka ambao pepa haikuvuja....

Tushazoea bana.
 
...........subirieni Dr. Ndalikacho (Katibu Mkuu wa NECTA atakavyokurupuka kutoa majibu ya kitoto). Mama ni jeuri sijapata kuona!! hata staff wa NECTA wanakiri mama hawezi uongozi kabisa!!! kuna watu wanafikiri kuwa na vyeti basi uongozi unaweza!!! Uzuri wa nchi hii, kujuzulu kwa uwajibikaji ni neno la kichina halipo kwenye kamusi ya watanzania!!!
 
taifa la wanafki, wazandiki, mbayuwayu,m,afisadi papa,mafisadi nyangumi,mafisadi sato,mafisadi sangara,kambale,prons bila kusahau wale wanaodharau vijisenti vya watanzania,kwani unadhani hawa watu walianzia wapi?walianza kuiba mitihani mwishowe wakajikuta wanaiba mabilioni ya watanzania
 
Back
Top Bottom