Wote mliochangia thread hii mmesahau kitu kimoja muhimu sana. Mtu
atakuwa na very strong will na determination ya kufaulu kwenye maisha,
lakini linapotokea la kutokea kama ilivokuwa kwa bwana Mitchel, kiwango
cha huduma ya afya itolewayo kwenye nchi ni muhimu mno.Baada ya
kuburuzwa na gari kisha moto kulipuka, angekuwa anaishi tuseme - Tanzania -
huo ndo ungekuwa mwisho wake na ndoto zake. Motivational stories
zenye kuhusisha kupona ajali kubwa ni stori zifaazo kwenye nchi zilizoendelea
na si hapa kwetu ambapo dawa za kawaida kabisa hazipatikani hospitali.