Miti ya Milonge

Miti ya Milonge

teku

Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
28
Reaction score
4
Habari za jioni,
Nilikuwa naomba kwa mtu anaefahamu lolote kuhusu upandaji wa hii miti na ukuzaji wake kibiashara.
Au kama kuna thread yoyote ambayo ilishawahi kujadiliwa kuhusu hii miti naomba mnitumie.
Nimeshindwa kuisearch.
Nitashurkuru sana nikipata hii elimu.
 
thread ipo Malila anahusika zaidi hapa
 
Last edited by a moderator:
thread ipo Malila anahusika zaidi hapa

Huu uzi upo humu,

Tatizo la zao la Mlonge ni soko lake, japokuwa unaonekana/uko na matumizi mengi, kuanzia dawa hadi chakula.Huku Pwani niliko mlonge unatumika kama mboga, wafugaji wanatumia kwa chakula cha mifugo,Wachina wanatumia kama dawa. Wakulima wa Mzenga walihamasishwa sana kulima mlonge, ilipokuja suala la kuvuna na kuuza, serikali/wahusika wakaingia mitini.

Unaweza kuotesha kwa kutumia cuttings au mbegu ( cuttings - yaani kama mhogo unavyooteshwa), ila maeneo unayotaka kuotesha hakikisha hakuna mbuzi kabisa. Unavumilia ukame sana baada ya kumea.

Nachoweza kukushauri, nenda TFDA wanaweza kukupa mawili matatu, au nenda idara ya dawa asili pale Muhimbili.

Kwa ujumla, mazao yote ambayo soko liko nje/Ulaya ni kizungumkuti kwa wakulima, mara waseme hivi, mara waseme vile, yaani shida sana.

Mwisho, kwa huku Pwani, mlonge hutumika pia kwa mambo yetu yaleeeeeee.
 
Habari za jioni,
Nilikuwa naomba kwa mtu anaefahamu lolote kuhusu upandaji wa hii miti na ukuzaji wake kibiashara.
Au kama kuna thread yoyote ambayo ilishawahi kujadiliwa kuhusu hii miti naomba mnitumie.
Nimeshindwa kuisearch.
Nitashurkuru sana nikipata hii elimu.

Nenda kwenye sehemu ya kutafutia nyuzi, search place, andika neno mlonge, kisha bonyeza search, zitakuja nyuzi nyingi sana, anza na ile aliyotoa G.MWAKASEGE, imecover vingi sana.
 
Huwezi kuamini barani India huwezi kulima na kuvuna bila kibali cha serikali. Waingereza walipofika India enzi hizo walikuta utapia mlo uliokithiri ndipo zao hili likatumika kama lishe kwa watoto ili waepukane na kwashiarkor!
 
Malila,naomba ufafanuzi wa kwanini MBUZI wasiwepo mahala panapolimwa mlonge?
Nalog off
 
Last edited by a moderator:
Malila,naomba ufafanuzi wa kwanini MBUZI wasiwepo mahala panapolimwa mlonge?
Nalog off

Mbuzi wanakula jamii nyingi za majani, ikiwemo milonge. Mlonge, mwembe,mchongoma,mlingoti mwekundu,mianzi, inaliwa sana na Mbuzi. Nilijaribu, nikapata hasara taslimu, walikula miche ya embe za kisasa kama hawanijui vile, mlonge wanabandua hadi ngozi ya tawi/shina.
 
Nimekuelewa mkuu. Pole kwa hasara uliyoipata.
Nalog off
 
Naitaji Mlonge kg 20000 ndani ya mwezi kila wiki nipate kg 2500
Call 0682426975/0654894210
Nb.naitaji sana kila kg ntanunua kwa 3000
 
Bei yako ipo chini sana.
Fanya 1kg@12000/= tufanye biashara..
 
No no hakuna biashara kama hyo.kama ingekua hivo wasingesoma wangeuza mbegu tu
 
Naitaji Mlonge kg 20000 ndani ya mwezi kila wiki nipate kg 2500
Call 0682426975/0654894210
Nb.naitaji sana kila kg ntanunua kwa 3000

Sasa kila wiki 2,500 kgs... mara nne si ni 10,000 kgs... hiyo 20 tons kwa mwezi kwa formula yako hii inatoka wapi... ndio inaitwa 'bongo yetu' hii...
 
Back
Top Bottom