Miti ya cyprus Iringa

Uparo

Member
May 4, 2012
55
9
Wajasiriamali wenzangu ningependa kujua miti aina ya cyprus huchukua muda gani baada ya kupandwa mpaka kuvunwa? Na pia inahitaji mtaji kiasi gani kwa hekari moja? Na unapanda miti mingapi kwa heka?
 
Wajasiriamali wenzangu ningependa kujua miti aina ya cyprus huchukua mda gani baada ya kupandwa mpaka kuvunwa? na pia inahitaji mtaji kiasi gani kwa hekari moja? na unapanda miti mingapi kwa heka?

Kwa uzoefu kidogo nilionao ni kwamba, miti hii inamea vizuri ktk high altitudes, kama unaweza pata shamba maeneo yafuatayo unaweza kuotesha miti hiyo, Makete,Njombe,Kilolo,Mfindi,Mby na West Kilimanjaro. Miti hii mara nyingi inakuwa tayari kwa mavuno baada ya miaka 15, nazungumzia mavuno mazuri ya mbao. Mimi naotesha miti hii.

Tatizo la miti hii ni mbegu, yani ni taabu kidogo kupata mbegu pale Kituoni Iringa. mimi ninacho fanya ni kuchagua miti bora na kutengeneza mwenyewe. Kwa sasa wengi wanakimbilia sana pinus patula ambazo baada ya miaka kumi ijayo itakuwa mingi sana. Watz wanaopanda miti hii ni wachache sana. ni kazi ngumu kuona shamba la eka kumi lenye miti hii ya umri wa miaka saba hivi. juzi nimeona Ihanga Njombe kuna jamaa amepanda zaidi ya eka 50 cyprus tupu, nimemvulia kofia.

Soko la miti hii ni kubwa ajabu sana. Kwa mitaa ya Njombe, mti mmoja kwa sasa wanauza Tsh 60,000/. Kwa hiyo eka moja ile familia inapata 600 x 60,000/ na kama wakipasua wenyewe, hela yake si mchezo. Kama unataka kuotesha miti hii, sema nikuonyeshe vijiji sahihi vya kupanda miti hii. Sio kila sehemu inakomea pines unaweza kuotesha miti hii.
 
Ndugu yangu plan yako ya kupanda Cyprus ni nzuri sana ila inabidi uwe muangalifu kupita kiasi. Manundu amekupa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kwa kiasi fulani ama pia yanaweza kukutumbukiza katika umaskini ambao haukuufikiria kabla. Ni kweli kuwa huku Iringa watu wanapanda sana Pinus species kuliko Cyprus, lakini nadhani sababu kubwa inatokana na matatizo yanayoikabili Cyprus species. Kuna vijidudu vinaitwa Cyprus aphid ambavyo hushambulia sana miti aina ya Cupresus lusitanica, katika mikaka iliyopita serikali ilipiga marufuku kabisa upandaji wa miti hii kutokana na kushambuliwa na kuharibiwa na hivyo vijidudu ambavyo inasemekana viliingizwa kwa makusudi kutoka South Africa ili kuharibuu soko la miti hiyo iliyokuwa inastawi vizuri sana Tz na kutishia soko la South Africa. Nachoweza kukushauri ni kwenda kwa wataalamu wa mbegu za Miti pale TTSA (Tanzania Tree Seed Agency) iliyopo Morogoro au Iringa ili upate full maelezo kabla hujaanza kuandaa mbegu kwaajili ya kupanda. Rotational age ya Cyprus nadhani ni kati ya miaka 15 hadi 20 kama unataka good quality timber. Pia idadi ya miti kwa hekari moja inategemea na upandaji wako utatumia spacing gani kati ya mti na mti. Nakushauri kama utaamua kupanda tumia spacing ya 3m x 3m ambapo kwa hekari moja itachukua miti kama 1111 kwa makisio. Nakutakia mafanikio mema mkuu katika kutimiza ndoto yako hiyo ya kuwekeza katika upandaji miti na ukiona hiyo Cyprus inasumbua, unaweza kupanda hata Eucalyptus au Pinus patula na ikakupa hela nzuri sana na kuuaga umaskini. Lakini inabidi ujue kuwa Plantation business is long a term investment with both very high profit and very high risk.
 
Ndugu yangu plan yako
ya kupanda Cyprus ni nzuri sana ila inabidi uwe muangalifu kupita kiasi.
Manundu amekupa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kwa kiasi fulani ama
pia yanaweza kukutumbukiza katika umaskini ambao haukuufikiria kabla.
Ni kweli kuwa huku Iringa watu wanapanda sana Pinus species kuliko
Cyprus, lakini nadhani sababu kubwa inatokana na matatizo yanayoikabili
Cyprus species. Kuna vijidudu vinaitwa Cyprus aphid ambavyo hushambulia
sana miti aina ya Cupresus lusitanica, katika mikaka iliyopita serikali
ilipiga marufuku kabisa upandaji wa miti hii kutokana na kushambuliwa na
kuharibiwa na hivyo vijidudu ambavyo inasemekana viliingizwa kwa
makusudi kutoka South Africa ili kuharibuu soko la miti hiyo iliyokuwa
inastawi vizuri sana Tz na kutishia soko la South Africa. Nachoweza
kukushauri ni kwenda kwa wataalamu wa mbegu za Miti pale TTSA (Tanzania
Tree Seed Agency) iliyopo Morogoro au Iringa ili upate full maelezo
kabla hujaanza kuandaa mbegu kwaajili ya kupanda. Rotational age ya
Cyprus nadhani ni kati ya miaka 15 hadi 20 kama unataka good quality
timber. Pia idadi ya miti kwa hekari moja inategemea na upandaji wako
utatumia spacing gani kati ya mti na mti. Nakushauri kama utaamua
kupanda tumia spacing ya 3m x 3m ambapo kwa hekari moja itachukua miti
kama 1111 kwa makisio. Nakutakia mafanikio mema mkuu katika kutimiza
ndoto yako hiyo ya kuwekeza katika upandaji miti na ukiona hiyo Cyprus
inasumbua, unaweza kupanda hata Eucalyptus au Pinus patula na ikakupa
hela nzuri sana na kuuaga umaskini. Lakini inabidi ujue kuwa Plantation
business is long a term investment with both very high profit and very
high risk.

Umesomeka kaka
 
Ndugu yangu plan yako ya kupanda Cyprus ni nzuri sana ila inabidi uwe muangalifu kupita kiasi. Manundu amekupa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kwa kiasi fulani ama pia yanaweza kukutumbukiza katika umaskini ambao haukuufikiria kabla. Ni kweli kuwa huku Iringa watu wanapanda sana Pinus species kuliko Cyprus, lakini nadhani sababu kubwa inatokana na matatizo yanayoikabili Cyprus species. Kuna vijidudu vinaitwa Cyprus aphid ambavyo hushambulia sana miti aina ya Cupresus lusitanica, katika mikaka iliyopita serikali ilipiga marufuku kabisa upandaji wa miti hii kutokana na kushambuliwa na kuharibiwa na hivyo vijidudu ambavyo inasemekana viliingizwa kwa makusudi kutoka South Africa ili kuharibuu soko la miti hiyo iliyokuwa inastawi vizuri sana Tz na kutishia soko la South Africa. Nachoweza kukushauri ni kwenda kwa wataalamu wa mbegu za Miti pale TTSA (Tanzania Tree Seed Agency) iliyopo Morogoro au Iringa ili upate full maelezo kabla hujaanza kuandaa mbegu kwaajili ya kupanda. Rotational age ya Cyprus nadhani ni kati ya miaka 15 hadi 20 kama unataka good quality timber. Pia idadi ya miti kwa hekari moja inategemea na upandaji wako utatumia spacing gani kati ya mti na mti. Nakushauri kama utaamua kupanda tumia spacing ya 3m x 3m ambapo kwa hekari moja itachukua miti kama 1111 kwa makisio. Nakutakia mafanikio mema mkuu katika kutimiza ndoto yako hiyo ya kuwekeza katika upandaji miti na ukiona hiyo Cyprus inasumbua, unaweza kupanda hata Eucalyptus au Pinus patula na ikakupa hela nzuri sana na kuuaga umaskini. Lakini inabidi ujue kuwa Plantation business is long a term investment with both very high profit and very high risk.

Naomba nichangie kidogo,
Spacing ya 3m x 3m itakupa miti 544 mpaka 576 hivi na ndio maana wakulima wengi wanapanda miti 600 ktk eka moja na sio 1111 kama ulivyosema. Spacing hii ya 3m x 3m itakupa mavuno mazuri kwa mbao. Na kama unataka kupata mavuno ya boriti ( eucalyptus) tumia 2m x 2m ambapo utakuwa na boriti 1200 kwa eka moja.

Wadudu wanaoshambulia miti hii, huathiri zaidi kizazi cha nne cha mti husika. Nilikwenda Iringa kituoni kufuatilia suala hili ndio nikapata ukweli huu.Tatizo hili lilifuatiliwa kupitia Nairobi, Cape town na mpaka Cyprus kwenyewe ilikotoka miti hii. Kwa faida ya wengine, miti hii ilitoka Cyprus, ikapelekwa SA, ikaja Nairobi, ikaja Tanganyika na baadae ikasambaa Malawi/Zimbabwe/Burundi na Uganda. Kilichotokea ni kwamba hapakuwepo na MSDS yo yote.

Mkuu nakushauri uipande kama una eneo zuri la kupanda, kwa sasa wakulima wengi wanapanda pinus patula, ambayo miaka michache ijayo itakuwa mingi sana. Hata leo ukiwa na cyprus eka moja wewe ni mfalme. Pale mitaa ya Njombe Vijijini mti mmoja wa cyprus sasa hivi ni Tsh 60,000/ cash hapo haujapasuliwa
 
Kwa uzoefu kidogo nilionao ni kwamba, miti hii inamea vizuri ktk high altitudes, kama unaweza pata shamba maeneo yafuatayo unaweza kuotesha miti hiyo, Makete,Njombe,Kilolo,Mfindi,Mby na West Kilimanjaro. Miti hii mara nyingi inakuwa tayari kwa mavuno baada ya miaka 15, nazungumzia mavuno mazuri ya mbao. Mimi naotesha miti hii.

Tatizo la miti hii ni mbegu, yani ni taabu kidogo kupata mbegu pale Kituoni Iringa. mimi ninacho fanya ni kuchagua miti bora na kutengeneza mwenyewe. Kwa sasa wengi wanakimbilia sana pinus patula ambazo baada ya miaka kumi ijayo itakuwa mingi sana. Watz wanaopanda miti hii ni wachache sana. ni kazi ngumu kuona shamba la eka kumi lenye miti hii ya umri wa miaka saba hivi. juzi nimeona Ihanga Njombe kuna jamaa amepanda zaidi ya eka 50 cyprus tupu, nimemvulia kofia.

Soko la miti hii ni kubwa ajabu sana. Kwa mitaa ya Njombe, mti mmoja kwa sasa wanauza Tsh 60,000/. Kwa hiyo eka moja ile familia inapata 600 x 60,000/ na kama wakipasua wenyewe, hela yake si mchezo. Kama unataka kuotesha miti hii, sema nikuonyeshe vijiji sahihi vya kupanda miti hii. Sio kila sehemu inakomea pines unaweza kuotesha miti hii.
Mkuu hii mbao kitanda chake ni imara?
 
Back
Top Bottom