Mitandao ya urais yaanza kuundwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,661
239,153
Mitandao ya wanaotamani kuwa viongozi wa juu wa Tanzania , hasa nafasi ya Urais imeanza kuundwa.

Wanaotajwa kuundwa kwa mitandao hiyo ni baadhi ya mawaziri waandamizi wa serikali ya Rais John Magufuli na wale walioshindwa kupata uteuzi katika serikali hiyo mpya.

Hatua ya Mawaziri hao inaakisi mienendo aliyopitia Dk Kikwete kabla ya kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania.

Dr Kikwete aliwahi kukiri kuwa alitumia muda mrefu kuhakikisha anaweka mikakati na kuwa na mtandao ambao ulimuweka ikulu .

" Kura zangu hazikutosha mwaka ule , lakini sikulala , nilianza kupambana siku ile ile na baada ya miaka 10 , hatimaye kura zikatosha .

Chanzo - MwanaHalisi .

Swali - Mitandao hii ni kwa ajili ya 2020 au 2025 ?
 
Mwanahalisi bila kutaja ni akina nani wanaounda mitandao hiyo, kivipi na wanajipangaje, habari yako ina kosa mashiko, hakuna asiyejua kuwa kila baada ya uchaguzi, watu huanza kujipanga upya taratibu na kuanza mikakati ya uchaguzi unaofuata.
 
Kwa sasa majina yanahifadhiwa kwanza ili kuepuka utumbuaji .
 
[QUOTE="Erythrocyte, post: 19525643, member: 109263"

Umenena vema mdau.
Si kwa nafasi ya urais, hata ubunge pia kumewaka moto.

Kuna baadhi ya wachaguliwa wameanza kwa kudhibiti
kila aina ya maendeleo katika halmashauri zao yanayodhaniwa
kuwa ni ya kumjenga mtu fulani kisiasa kwa uchaguzi ujao.

Madiwani wamegawanyika na kufitinika (timu za kuwaunga mkono zimeundwa)

Mfano mzuri ni katika jimbo la Kondoa Vijijini ni mtifuano bila huruma.
ALIYEPO ANADHANI MIPANGO NA UBUNIFU UNAOFANYWA NA BAADHI YA
MADIWANI NI MKAKATI WA KUMDHOOFISHA ASIRUDI MHULA UJAO.

Wafanye tu hizo kambi ila wasiguse maslahi ya wananchi maskini.
 
ACHENI ULAFI NA UROHO WA MADARAKA NYINYI WANASIASA! WALAHI TUKIWAGUNDUA KAZI YETU ITAKUWA KULA PESA ZENU HADI MFILISIKE HALAFU KURA HATUWAPI BASI MKIKOSA MADARAKA MNAYOYAOTEA USIKU NA MCHANA MTAPATA VIHARUSI, KISUKARI NA MAGONJWA MENGINE SUGU IFIKAPO NOVEMBA 2020. PIA NAHISI WENGI WENU MTAKUWA NA MADENI NA MTAFILISIWA! SIJUI NI NINI KITAWAPATA BAADA YA HAPO. RIDHIKENI NA MAISHA MLIYONAYO!! ACHENI KUPENDA MAKUU....MNAZITAABISHA FAMILIA ZENU MARAFIKI NA JAMAA!
 
Mitandao ya wanaotamani kuwa viongozi wa juu wa Tanzania , hasa nafasi ya Urais imeanza kuundwa.

Wanaotajwa kuundwa kwa mitandao hiyo ni baadhi ya mawaziri waandamizi wa serikali ya Rais John Magufuli na wale walioshindwa kupata uteuzi katika serikali hiyo mpya.

Hatua ya Mawaziri hao inaakisi mienendo aliyopitia Dk Kikwete kabla ya kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania.

Dr Kikwete aliwahi kukiri kuwa alitumia muda mrefu kuhakikisha anaweka mikakati na kuwa na mtandao ambao ulimuweka ikulu .

" Kura zangu hazikutosha mwaka ule , lakini sikulala , nilianza kupambana siku ile ile na baada ya miaka 10 , hatimaye kura zikatosha .

Chanzo - MwanaHalisi .

Swali - Mitandao hii ni kwa ajili ya 2020 au 2025 ?

Kumbuka MwanaHalisi leo hii wameomba radhi kwa kuandika uongo.
 
Mwaka huu kuna uchaguzi wa ndani wa CCM kwa hiyo ni lazima wajipange kiushindani.

Ni kawaida kwa chama kikubwa kilichoshika dola.
 
Hakuna ajabu ilimradi waheshimu katiba, kanuni na miongozo ya chama kisha baada ya kura ya maoni wavunje makundi yao
 
Mitandao ya wanaotamani kuwa viongozi wa juu wa Tanzania , hasa nafasi ya Urais imeanza kuundwa.

Wanaotajwa kuundwa kwa mitandao hiyo ni baadhi ya mawaziri waandamizi wa serikali ya Rais John Magufuli na wale walioshindwa kupata uteuzi katika serikali hiyo mpya.

Hatua ya Mawaziri hao inaakisi mienendo aliyopitia Dk Kikwete kabla ya kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania.

Dr Kikwete aliwahi kukiri kuwa alitumia muda mrefu kuhakikisha anaweka mikakati na kuwa na mtandao ambao ulimuweka ikulu .

" Kura zangu hazikutosha mwaka ule , lakini sikulala , nilianza kupambana siku ile ile na baada ya miaka 10 , hatimaye kura zikatosha .

Chanzo - MwanaHalisi .

Swali - Mitandao hii ni kwa ajili ya 2020 au 2025 ?
Wakati wana CCM wanaandaa mitandao wenzao wa vyama vya upinzani kuna viongozi wametamka bayana kuwa watagombea nafasi ya rais 2020. Hawa ni wakweli mioyoni mwao na wanawapa nafasi wapiga kura fursa na muda wa kuwatathimini kabla ya uchaguzi.
 
Kuna haja ya wananchi kuyasusia baadhi ya magazeti........

Ya kiuni yanayoandika upumbavu kama huu..............

Watu wanapoteza muda kusoma magazeti ya kiuni kama haya halafu wengine tukisusia na kuanza kusoma Magazeti ya Daily mail,The Sun,The guardian mnasema tumekosa uzalendo...........

Uchaguzi umeisha juzi Sasa hivi eti mitandao? How comes upuuzi mtupu.........
 
Back
Top Bottom