Mitandao Ya Kijamii Itawadondosha CCM Asubuhi Na Mapema

Mitandao Ya Kijamii Itawadondosha CCM Asubuhi Na Mapema

Mtu mmoja kutoka Mwanza alieleza kuwa ule utitiri wa watu ulienda kumshangaa fisadi mkuu ambaye hawajamuona majukwaani tangu 2008. Mtu huyo alidokeza kuwa hukumu ya kweli ni Oktoba 25.

Siku ya kumwapisha lowasa kuwa rais wa 5 ndio atazimia huyo mtu wako wa mwanza
 
Kikatio changu nakitunza kama lulu oct 25 chichiem lazima wang'oke. Vijana wote 2mehamasika Lowasa na UkAWA ndio gumzo la nchi

Hata mkeo husimuonyeshe mkuu maana hao kwa ccm hawafai
 
lowasa atakuwa raisi wa wanywa viroba wa mitandaoni siyo wa wananchi makini,kuna majimbo hadi sasa ccm imepita bila kupingwa

Naona wewe tayari ndiyo umebugia viroba,mwaka huu hiyo habari ya kupita bila kupingwa sahau kabisa
 
Hakika ukombozi unatakiwa kwa hali na mali.. Mie najitolea kutengeneza APP ya Android ya kukusanyia matokeo na kuyaonesha kwa watu wengine papo kwa oapo.. hii app itakuwa na uwezo wa kuweka geotag ili kutambua eneo husika au kituo cha kura kilipo.. matokeo yatakuwa yanapelekwa moja kwa moja kwenye server maalum (cloud server). Kwa maana hiyo, ukawa hawatategemea NEC ambao wana maagizo ya bao la mkono. Pia kwa namna ya pekee, matokeo yatakayo kusanywa kwa njia hii yataweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani endapo dalili za bao la mkono zitajitokeza.. Huduma hii niko tayari kuitoa bure kwa UKAWA tu.. tuwaoneshe ccm kuwa tuna shule si ya kitoto, ambayo wwnyewe wamewanyima watanzania.. mnaweza ku pm kwa maelezo ya kina
 
Siku ya kumwapisha lowasa kuwa rais wa 5 ndio atazimia huyo mtu wako wa mwanza

Hawezi kuzimia Mkuu, demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya walio wengi. Kama wengi watamchagua EL, wale ambao hawakumchagua itawalazimu kuwa wapole hadi nyakati tano zitakapotimia. Hata JK amekuwa Rais kwa miaka 10 haimaanishi kuwa Watanzania wote walimpa kura bali wengi walimpa, wachache waliomnyima kura wamekuwa wavumilivu kwa miaka yote 10, vivyo hivyo hata wale tusiomtaka Lowassa kama atashinda itatupasa kukubali matokeo na kuwa wavumilivu kwa ustawi wa Taifa letu.
 
Hakika ukombozi unatakiwa kwa hali na mali.. Mie najitolea kutengeneza APP ya Android ya kukusanyia matokeo na kuyaonesha kwa watu wengine papo kwa oapo.. hii app itakuwa na uwezo wa kuweka geotag ili kutambua eneo husika au kituo cha kura kilipo.. matokeo yatakuwa yanapelekwa moja kwa moja kwenye server maalum (cloud server). Kwa maana hiyo, ukawa hawatategemea NEC ambao wana maagizo ya bao la mkono. Pia kwa namna ya pekee, matokeo yatakayo kusanywa kwa njia hii yataweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani endapo dalili za bao la mkono zitajitokeza.. Huduma hii niko tayari kuitoa bure kwa UKAWA tu.. tuwaoneshe ccm kuwa tuna shule si ya kitoto, ambayo wwnyewe wamewanyima watanzania.. mnaweza ku pm kwa maelezo ya kina

Jitahidi kaka we c ndo Lubuva, baada y kukusany matokeo kwahiyo app yako mtangaze na mshindi kabisa
 
Utafiti wangu nilioufanya toka Mhe.Lowassa kuanza ziara kwa mikoa ya Dar,Mbeya,Arusha,Mwanza na hatimaye Zanzibar Ccm washadondokea pua.

We fikiri ule utitiri wa kizazi hiki cha digital ambacho kwa asilimia mia kina tofauti kubwa na kile cha 95 ya Mrema

We jiulize mwaka 2010 watanzania wangapi walikuwa wanatumia social network?

Vijana wangapi walikuwa na hamasa ya kupiga kura?

2010 Ccm walipata 90% ya promo kwenye media zote na waliponea chupuchupu kudondokea pua.

Leo hata media zote zibane social network zinatosha kuwatoa madarakani Ccm

Mfano"Kura zote kutoka vituoni zitakuwa zishajulikana idadi yake,Hata kama Tume itakuwa inajivutavuta.Unaweza kuona kasi ya picha za mafuriko kwenye mikutano ya UKAWA zinavyosambaa nchi nzima kwa sekunde.

Ndivyo kura za urais zitakuwa zikisambaa,Na ukweli kujulikana nani kashinda wapi na kwa kura ngapi.

Kwa upande wa Ubunge na udiwani sehemu zote za mjini matokeo rasmi kabla hata mkurugenzi kutangaza yatakuwa wazi lisaa limoja Baada ya vituo kufungwa,Na yote hiyo itawezekana kwa hisani ya social networks

Ndio maana nasema,Kelele za Nape ni sawa na kusimamisha treni kwa mruzi hii ni 2015 na si 1995.Wajiandae tu kisaikolojia kukabidhi madaraka October 2

Saa 4 asubuhi tunakuja kuwagongea pale magogoni,UKAWA ni mpango wa mollah!

Sept mosi imekaribia
 
kwahio watu wa UKAWA ndio mnatumia mitandao peke yenu?. akili za kushikiwa ni balaa.
 
TANZANIA YETU
1. Kwa miaka 51 hii inchi imeongozwa na ccm peke yake ambayo ni zao TANU na ASP.
2. Tz ina ukubwa ukubwa wa 945,000 km square yani sawa na uchukuwe
Denmark,France, United kingdom(uk),Netherland,Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.
3. Tz ni nchi ya tatu kwa uzalishaji dhahabu afrika na ipo top 20 duniani.
4. Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani.
5. Tz ina migodi pia ya almasi,uranium kule dodoma ambao unamilikiwa na
warusi,chuma kule lganga na mchuchuma mbeya ambacho kimechanganyika na
tatinum ambacho kilo 1 ni karibia laki moja. Tz ina hifadhi ya kubwa ya makaa ya mawe kule mbeya
6. Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 kilometers bahari inaleta fursa za
usafirishaji,uv uvi,utalii na nyinginezo,
7. Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda mengi duniani baada ya marekani na uturuki
8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.Maziwa matatu
makubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwa
matatu yote yapo Tanzania..Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani(la kwanza
afrika) na ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa(la pili afrika) na la kwanza kwa
kuwa na kina kirefu duniani.Ziwa nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani(ni la 3 afrika).
9. Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto kagera,mto Ruvuma,mto rufiji,mto wami,mto maragarasi,mto mara,mto pangani,mto mara,mto gombe,mto mweupe wa nile.na ina mito midogo mengi km mto kilombero,mto mbemkuru.
10. Tz ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani.
11. Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu duniani Serengeti na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro.
12. Tz ni nchi ambayo hajawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya
ardhi,magonjwa kama ebola,mafuriko na vimbunga au ukame.
13. Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nnchi za Africa zimekikosa AMANI kwa miaka yote 51 ya uhuru hajawahii kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.
14. Tz ni nnchi ambayo imepakana na nchi (Uganda,Rwanda, Burundi,Zambia,
Malawi,Drc congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.
15. Tanzania imechaguliwa kama Nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa na vivutio vinavyohamasish a Utalii. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.
16. Tz ndiyo nchi ya kwanza africa kuwa na maji mengi yaio na chumvi yaliyokuwa
kwenye uso wa dunia(fresh surface water) kutokana na kuwa na mito na maziwa
mengi na kupitiwa na bonde la ufa.
17. Nadhani kila mtz anajua juu ya sifa ya Tanzania kwenye swala la kuwa na ardhi ya rutuba inayofaa kwa kilimo
Pamoja na sifa zote hizi Lakini Tz ni nchi iliyokwenye kundi la nchi maskini duniani
ambao asilimia kubwa ya raia wanaishi chini ya dola moja.
Jitahidi kuiombea kwa bidii nchi hii inayotakiwa kuwa kwenye top 10 ya nchi nzuri na imara duniani.

TAFAKARI
 
ndugu zangu ukisikia mapinduzi ya kweli yaliyo wahi kutokea ni wazi yalianzishwa na vijana wa vyuo vikuu walio choshwa na mifumo kandamizi ktk nchi zao
tuanze na mifano michache zamani kabla ya kuwa na wasomi wengi wakolon walitusomeshea wazazi wetu wachache
lakin wale wachache mfano mwalimu nyerere alikuwa msomi wakati ule aliongoza wenzake ktk harakati xa kudai uhuru kamili wa nchi yetu Tanganyika japokuwa utawala wa mkolon ulikuwa umeimarika sana lakin nyerere kwakutumia mtandao wawasomi waliwaelimisha wengi na wakapata uhuru japo ilikuwa kwa mateso mengi sana

afrika kusini mzee nelson mandela naye aliongoxa mtandao wawasomi kwa mateso makubwa kupata uhuru kamili wa nchi yake leo ni nchi nzuri
na nyingi za afrika. hiyo yote nilitaka kurudisha mawazo yako hapa iliujitambue kama kijana na nafasi yako ktk ukombozi wa pili wa nchi yetu
ndugu xangu hii mitandao ya kijamii ni njia nzuri katika uhamasishaji wa mabadiliko sasa tunasisitiza vijana wasomi kuitumia ipasavyo kuhamasisha ili watu kupata elimu ya kutosha ya kimapinduz ya mabadiliko ktk taifa letu. tuwaelimishe watanzania umuhimu wa kuwa na kiongozi bora asiye kuja kulinda maslahi ya viongozi wenzake mwenye nia ya kuliinua pato la taifa na kuwa inua wananchi sio kuja kusimamia mikataba mibovu kwa maslahi yao binafsi sio kiongoxi mweka chama chake mbele bila kuzingatia wananchi wana hali gani
watu waliobaki ni ss vijana wasanii wa taifa hili wamesha tumiwa kwa maana hiyo wamefungwa midomo wameshakuwa makasuku wa taifa wa watawala kwa matakwa yao sasa sis tuchukuwe jukumu kupinga vikali hadharan bila kuogopa chochote tukiamini mapinduzi yataletwa kwa utashi wetu juu ya kiongozi tunaye mwitaji

ndug wasomi vyuo vikuu huu mtandao wa whats up umeshawahi kupindua serikali kadhaa kwa kutumia vijana wasomi waliokataa kutumika kwa maslahi ya wachache
angalien mhawanyo wa stahiki za uma zilivyo zimezingatia jina na nguvu aliyo nayo mtu ktk cheo chake
tukataen kuwa kati aina moja hii ya utawala tusisitize demokrasia tuwafundishe watu wote ubaya wa hiki chama tawala na mfumo wake tuwakatae ktk box la kura napia tuwe tayari kulipigania taifa letu hata ikifikia kupoteza uhai wetu

watuwetu hawana elimu bora, afya zao zinayumba hawana matumaini deni la taifa limepanda uchumi wa taifa umeshuka fedha yetu imeporomoka hatuna majibu ya matatizo ya watu wetu jamn tufundishe watu makanisan, misikitin na wasio na din tunalotaka taifa letu lile ambalo lilikuwepo kabla ya kutawaliwa

kijana mwenye uchungu na taifa hili atakuwa mzalendo na mwalimu ktk jamii aliopo ilikuwafundisha ndugu zetu watz juu ya nani atafaa kuliongoza taifa letu
tukataen hadharani mfumo wao na watu wao pia
kijana chukuwa hatua sasa nikwa moaka mitano tena kama hukuwa na kazi ujue hutaipata tena, maana sera zao ni zilezile waliuza viwanda na vingine wakaviuwa kwa ulafi leo hakuna ajira
wametupeleka vyuo vikuu tukasome ili tujekuwa ombaomba kwako
hawana sera kabisa mtawasikia cha zaidi watahonga fedha nyingi na vitisho vingi

vijana tuamuen sasa kesho mbali tutumie hii mitandao asiwepo wakulala mpaka ukombozi umekamilika
 
Msilemae na mafurika mkadhani wote wanaohudhuria ni wapiga kura wa Lowasa wengine wanaenda kusikiliza tu kama kuna jipya, mjini hata kuku wakiwa wanapigana utaona watu wanajaa na kuwazunguluka inamaana nao ni wafuasi wa kuku???
 
Back
Top Bottom