BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,738
- 3,198
Majibu ya mtandao haupo/upo down ni kauli za kawaida ukienda sehemu mbalimbali hasa za huduma za kijamii.Serikalini hili ni jipu lililo iva lakini watanzania hatuko makini wala hatuhangaiki kupata ufumbuzi wa kudumu kama lilivyotatizo la umeme.
Unataka kupata taarifa muhimu ili ufanye maamuzi au ufanye malipo unaambiwa mtandao haupo na hatujui lini au mda gani utarudi! vitengo vya ICT vipo.watu wanalipwa mishahara nchi inapata hasara.watu hawafanyikazi kisa mtandao.wengine wanaacha kazi zao kufuata huduma wanaishia kupoteza mda wao bila kuhudumiwa.
Nipo hapa Ilala upande wa mipango miji ofisi ya fedha.toka wiki iliyopita nikienda kufanya malipo naambiwa hakuna mtandao au uende wizarani kwa baadhi ya.malipo(mengine lazima ulipe hapohapo haijalishi lini mtandao utarudi) hii hali sio mara ya kwanza ni kawaida sana.
Kwanini teknolojia itese wananchi badala ya kuweka maisha yetu yawe marahisi? kwanini tunashindwa kuwa na mtandao wa uhakika huku tunajinasibu tuna mkonga wa uhakika wa mawasiliano.Hili waziri mhusika/Rais atuondolee hii kero.