Mitandao isitumike kumchafua Rais

Kuna haja ya kuwashtaki waandishi wa habari magazetini,ni kwa nini wanaiba habari za JF na kuzifanyia biashara kwenye magazeti yao?hii ruhusa ya ku copy habari za JF nani anawapa?Uongozi wa JF hamulioni hilo,JK HAJACHAFULIWA NA MTU BALI MWANAE NDIO KAMCHAFUA,sasa mlitaka tumsifie Mwanaasha kwa kufeli?
 
Tatizo ni baraza la mitihani na wizara ya elimu. Kama siyo wao hii mitandao ingepata wapi hayo matokeo. Huu ujinga wa kuanika majina ya watoto hadharani ukomeshwe. Matokeo ya mitihani ni private matter. Wanachofanya baraza/wizara ni kama vile upime afya halafu matokeo ya lab yatolewe hadharani. Sioni sababu ya Tz daima kulaumu mitandao
 
Asanteni Tanzania Daima kwa kuwajulisha watanzania woote kuwa mtoto wa JK kilaza!!
Maana mitandao inabagua, si kila mtu anaweza kuipitia kama gazeti,..... big uo!!

Kama ile stori ya kuhongwa suti na mwarabu!
 
amkane basi kwamba yule sio mwanae ili ajitenge na 'uchafu' ............kama mwanae kupata Div 4 ni uchafu.

mwanaume mzima kuhongwa nguo unakuwa ushajichafua kabisa mbele ya wanaume wenzako, hata mbele ya wanawake wa maana.

Amkane kwa lipi? na wewe cha ajabu unachokiona ni kipi? Hapo kwenye red ELIZA na wewe ni mmoja wa hao wanawake wa maana?
 

labda unipe maana ya kumchafua mtu kwa mtazamo wako wewe
 
Huu ni mwanzo wa anguko la cdm kama chama cha upinzani. Hii tahariri ya tanzania daima ilipaswa kuandikwa uhuru na habari leo. Ngoja tuendelee kutazama hii sinema
 
JK is a public figure ni lazima tumjadili. Nyie magazeti endeleeni kulala tu.
Ninategemea mngetuletea hata mahawara wa JK na wengine na hata mkewe/wakewe. Kioo cha jamii kinatakiwa kiwe kweli kioo hakuna kufichaficha. Kama nyie magazeti mmeamua kurudi ughaibuni rudini siye tutaendelea. Rais Kibaki ilibidi aende kwa waandishi wa habari na kumtangaza Lucy kama mke pekee!! Huyu JK anaishi kwa kodi zetu anakula, anavaa lazima tumchambue kila wakati.
 
Bwana yesu apewe sifa, wote sema amen!. Jamani binafsi nampongeza rais kwa kuwa mzalendo kwa nchi anayoiongoza, kama binti yake mwenyewe anasoma hapa nyumban. Jamani tujaribu basi kuwaheshimu hata wanaotuongoza! Kwan yeye rais kasema nin kuhusu watoto wetu/dada zetu walio fail? Kwan yeye alie fail hatakiw ku fail kisa ni mtoto wa rais? Ama yeye ni malaika? Au huu mtandao watoto wamezidi? Au wengi hawana shule? No, tubadilike, na tuache tabia ya kusakama maisha binafsi ya mtu!
 
kutokana na sayansi mtoto anarithi sehemu kubwa ya akili ya baba na mama. wewe unataka tumsifie kwa lipi? analeta ubishoo shuleni kwa vile baba ni Rais. Hana control na internet ingekuwa gazeti sawa wangelifungia na bado tutamuonyesha uchafu wake ili ajisafishe
 
Huu ni mwanzo wa anguko la cdm kama chama cha upinzani. Hii tahariri ya tanzania daima ilipaswa kuandikwa uhuru na habari leo. Ngoja tuendelee kutazama hii sinema

Utatazama mpaka uchoke hakuna anguko lolote kutoka CDM.
 
Huu ni mwanzo wa anguko la cdm kama chama cha upinzani. Hii tahariri ya tanzania daima ilipaswa kuandikwa uhuru na habari leo. Ngoja tuendelee kutazama hii sinema

Mkuu. Kumbuka pia Tanzania Daima linasomwa na yeyote si wa wenye mlengo wa CDM tu. Kwa mantiki hiyo, TD wamefanya vema kuutahadharisha umma wa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.
 
Kufeli kwa mtoto wake kuna uhusiano gani na urais wake? na je wewe kwenu hakuna waliowahi kufeli mitihani na pengine ukiwemo wewe, je nani alimsema Baba yako?

Uhusiano uliopo ni kwamba yeye ndio mwenye dhamana ya elimu hapa nchini.

Kwa muda mrefu elimu imeendelea kushuka bila hatua zozote madhubuti kuchukuliwa.
Walimu wameendelea kudharauliwa na serikali, vitendea kazi shuleni hakuna.
Kufeli kwa halaiki, wizi wa mitihani, ukosefu wa maabara, madawati,vitabu n.k..

Kufeli kwa mtoto wake ni kielelezo kizuri kushindwa kusimamia hata elimu ya mtoto wake.
Kama ameshindwa ya mtoto wake atapata wapi uwezo kuhakikisha Tanzania inatoa elimu bora kwa watoto wote na kuzuia hili tatizo la sasa la kufeli kwa halaiki. Ni lazima kwanza uwe kiongozi bora ndani ya familia yako ndio uweze kuwa kiongozi bora nje ya familia yako.
 
Sidhani kama kuna mtu kasema Mwanaasha kashindwa maisha, tunachosema ambacho kiko wazi ni kuwa mtoto wa rais kapata DIV IV.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…