Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,802
Zifuatazo ni dhambi zilizohalalishwa na mitandao na zinafanywa bila hofu ya Mungu kwa kujua au kutokujua.
1. Uongo. Kupitia simu na mitandao kusema uongo imekua ni kawaida. Watu wanazusha habari za uongo na kusingizia vifo au kushikwa ugoni ilimradi kujipatia umaarufu.
2. Kuzini. Tunawatamani wanawake wengi kwa kupitia picha na video chafu za zilizotapakaa mitandaoni lakini Mathayo 5:27 inasema:-
“Mmesikia kwamba watu waliambiwa: ‘Usizini!’ Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.
Je Mara ngapi ndugu yangu umemtamani mwanamke kupitia picha na video chafu zinazopostiwa mitandaoni au kupitia matangazo yanayojitokeza kwenye simu yako ya Smart?
3.Kuchukuiana. Ni dhahiri imekua rahisi mno watu kueneza chuki baina ya mtu na mtu au kikundi. Mtu akipost harusi yake au kununua gari jipya,comment ni chuki tupu!
4.Wizi na utapeli. Watu wana iba na kufanya utapeli wa pesa,bando,kirahisi tu wakidhani ni mzaha.
5.Kutukana.Si rahisi kumtukana mtu matusi mazito huku unamtizama na mbele za watu.Lakini kutokana na ID fake ni rahisi mno mtu kuporomosha matusi yoyote kwa sababu hajulikani. Unaweza muona mtu wa heshima kumbe anashinda mitandaoni akitukana watu ovyo!
6.Michezo ya kamari. Huko nyuma ilikua ni vigumu kukuta mtu mwenye heshima na hofu na Mungu akicheza michezo ya kamali.Hii ilikuwa michezo ya walevi na wavuta bangi. Lakini kupitia simu shetani kawakamata wengi. Si ajabu Shekhe au mchungaji kukuta wanashiriki kucheza kamali kwa kujua au kutokua.
Kwa upande wako ni dhambi ipi imekukamata kupitia mitandao kwa kujua au kutokujua?
Nawasilisha.