Mitambo ya Dowans yauzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mitambo ya Dowans yauzwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WikiLeaks, Mar 16, 2011.

 1. W

  WikiLeaks Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans, tayari imeshauzwa nje (Cyprus) kinachosubiriwa sasa ni kumalizika kwa taratibu za kimahakama dhidi ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) iliyoko Mahakama Kuu ya Tanzania.

  Jana nilianzisha thread hii Mods wakaipeleka kwenye Jokes/utani+udaku please Mods muwe waangalifu kabla ya kutenda. Nilikuwepo.

  Source:Mwananchi

  Link: Mitambo ya Dowans yadaiwa kuuzwa nje
   
 2. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wasamehe bure Mods, kama ni kweli basi kuna changa la macho hapa ndiyo maana JM anakazana Dowans wapewe mkataba mfupi wa miezi mitatu mitatu ili litimie sharti la mnunuzi kazi tunayo.
   
 3. M

  Maimai Senior Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  DOWANS WAS an investment specifically to raise hot monies from Tanzanian economy. Jamani yaani nchi hii haina mwenyewe.. tunaliwa na kubakia wapambe. Nilikuwa siku moja nakula lunch ubungo plaza kukiwa na semina ya wabunge, jamaa mmoja akaniambia nimpishe waziri mmoja kwenye foleni na kumlazimisha dada kumbebea chakula.. eti kwa sababy **** **** **** them
   
 4. M

  Maimai Senior Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tutafute mjerumani mmoja mwenye umri wa miaka 50 tumpe nchi angalau miaka 5 airekebishe kisha amuachie slaa au mbowe
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Sadick Mtulya
  MITAMBO ya kuzalishia umeme inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans, ilinunuliwa na Cyprus Independent Power Cooperation (CIP) kwa Dola za Kimarekani milioni 70 mwaka 2009, imefahamika.Habari hizo zinakuja wakati serikali ikiwa mbioni kurekebisha sheria ya manunuzi ya umma kwa kile kinachoelezwa ni mkakati wa kutaka kuinunua mitambo hiyo.

  Mitambo hiyo ililetwa nchini baada ya Dowans kurithi mkataba wa Kampuni ya Richmond wa kuzalisha umeme wa kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wakati taifa lilipokumbwa na upungufu wa umeme mwaka 2006.

  Hata hivyo baadaye ilishindwa kuondolewa nchini kufuatia hatua ya Tanesco kufungua shauri la pingamizi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ikidai mitambo hiyo kuwa ndiyo dhamana ya Dowans katika kesi ya msingi ya kudai fidia iliyotokana na hasara iliyoipata kutokana mkataba utata.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, katika shauri hilo Tanesco ilidai kama Dowans ingeshindwa kesi na kama isingekuwa na fedha za kulipa, mitambo hiyo ingefidia fedha hizo.

  Hata hivyo kinachosubiriwa sasa ni kumalizika kwa taratibu za kimahakama katika kesi ya Dowans dhidi ya Tanesco iliyoko Mahakama Kuu ya Tanzania.Kwa mujibu wa habari, CPI imeilipa Dowans lakini, kampuni hiyo haitachukua fedha hiyo hadi itakapotimiza masharti makuu mawili.

  Masharti hayo ni pamoja na mnunuzi wa mitambo hiyo kuitaka Dowans kuhakikisha kuwa mitambo hiyo inapata mkataba wa kuzalisha umeme nchini ambao si chini ya miezi sita, lakini ikishindwa hilo, ihakikishe kuwa imepakiwa ndani ya meli ili isafirishwe kutoka nchini ndipo iruhusu kuchukuliwa kwa fedha hizo.Juzi Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans Tanzania, Stansalus Munai, alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, hakukana wala kukubali.

  Alisema "mitambo yetu haijakosa soko. Wanaihitaji wengi wa kuisafirisha nje ya nchi."Kwa mujibu wa Munai, kila siku wanapokea watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanaotaka kununua mitambo hiyo."Wanakuja wengi kila siku wa ndani na nje, mazingira ya huko nyuma yalizuia tusiuze sasa hilo linaelekea kwisha," alisema.

  Alipotakiwa kueleza kama watakuwa tayari kuiuza mitambo hiyo kwa serikali, Munai alisema hawatalazimisha biashara na serikali, lakini wakienda kwa nia ya kuinunua watawasikiliza."Hatutalazimisha biashara na serikali, hawajaja ila wakija tutawasikiliza. Tutawafikiria kama watu wengine, bei inategemea," alisema Munai.

  Chini ya sheria ya mwaka 2004, inayotumika sasa, serikali hairuhusiwi kununua bidhaa au mitambo ambayo tayari imetumika.Lakini kama sheria hiyo ikirekebishwa, itatoa nafasi kwa serikali kununua mitambo iliyokwishatumika kama inayomilikiwa na Dowans.

  Sheria ya sasa inayoizua serikali kutonunua bidhaa au vitu vilivyotumika ilitafsiriwa katika sheria ya manunuzi ya Benki ya Dunia (WB), inayolenga kuepuka mazingira ya ufisadi.Mwaka 2008 Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd ilitangaza zabuni ya kuuza mitambo yake ya kuzalisha umeme ikiwa ni miezi mitatu baada ya serikali kusitisha mkataba wake na (Tanesco).
   
 6. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  serikali haina nia njema na wananchi hata kidogo!!!!!
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Sure, kwanini ilazimishe kununua mitambo ambayo inaonekana wazi ina utata hadi serikali inataka kubadili sheria ya manunuzi kwa ajili ya Dowans, why lakini?????????????? ipo siku watakuja kutuambia wakiwa wamekufa watoto wao watatuambia.
   
Loading...