Misungwi, Mwanza: Aenda jela miezi 6 kwa kosa la kumdhihaki Rais Magufuli

Kuna Uzi umeanzishwa wa kufananisha Nyerere na Mandela kwa Uzi huu Mandela ataendelea kua best sisi hata katiba bora mzee Alisahau atakutuachia
 
Kuna uzi ulikuwa na kichwa cha habari "Kuna anayefahamu wapi Magufuli anatupeleka?" . Uzi huo sikuuchukulia maanani sana, ila leo nimeanza kuukumbuka kuwa uzi huo ni wa Almasi kama si dhahabu.

Nilidhani najua anakotupeleka, kumbe nilikuwa mbumbu. Na sijui ni wangapi ambao ni mbumbu kama mimi, nafikiri ni wengi sana. Kama hivyo ndivyo, watanzania tumekwisha. Haya mambo nilikuwa nayasikia nchi za wafalme tu kama Filipine, Moroko, Saudi arabia n.k. Leo Tanzania nayo imo ndani!!!!!!!! Ni ajabu. Sasa hatutaweza kuzungumza chochote kile.

Subiri nirudi kuutafuta ule uzi wa anayefahamu Magufuli anakotupeleka, nikiamini kuwa swali lenyewe si kumdhihaki Rais. Sinahakika ngoja nichukue risk tu.
 
mhh!!! siku wangedukua huku, jf ingekuwa segerea forum. sikuhizi kama sio ccm au huungi mkono baadhi ya juhudi roho juujuu tu. ukiropoka tu hakuna salia mtume. kazi kwelikweli. Haya mambo yakienda sanjali na mahakama ya mafisadi kula vichwa na kuvitia gerezani nyumbani kutanoga kupitiliza.
Binafsi mpaka muda huu sijaliona kosa la kumtia huyo kijani hatiani, hivi kusema Raisi kitu gani kunamfanya kweli rais kuwa kitu gani ?, kwanini hao wapambe wake wasituoneshe kwamba rais ni kitu !!, Natafakari utendaji wa mahakama zetu.
 
Huu ni ujinga, sasa mtu akisema 'Rais Magufuli kitu gani bwana' ndio anafungwa miezi 6, amekuwa Mungu? Seriously, mapolisi na majaji tuache kujipendekeza kwa Rais ili kupandishwa vyeo, mnaumiza wananchi bure..
Kinachonishangaza kuna mijitu inajitoa ufahamu na kudai eti acha akatiwe fundisho, shame to the Law makers, Police and Megistrates, hivi kweli Polisi aliamua kuacha kazi zake za ulinzi akampeleka huyo kijana mahakamani, na hakimu nae akapoteza muda wake kushughulikia hilo jalada ??, mbona tunasikia kuna mahabusu wengi magerezani kesi zao hazijaisha na zina muda mrefu tu !!, na kwamba kmahakama ina upungufu wa mahakimu ?.
 
Tuko katika nyakati za hatari ambazo hata muhasisi wa taifa hili haliziona ila nashangaa alitutoka pasipo kuzifanyia kazi. Tunavuna tulichopanda.
 
Tuko katika nyakati za hatari ambazo hata muhasisi wa taifa hili haliziona ila nashangaa alitutoka pasipo kuzifanyia kazi. Tunavuna tulichopanda.
Ndio, nakumbuka aliwahi kusema (Katiba hii inanipa madaraka makubwa sana, siku akitokea rais mwehu akaitumia vibaya mtalalamika sana, Ni bora sasa tukayapunguza madaraka ya rais), yametokea, cha kushangaza kuna watu walitaka Eti madaraka ya rais yaongezwe.
 
Ndio, nakumbuka aliwahi kusema (Katiba hii inanipa madaraka makubwa sana, siku akitokea rais mwehu akaitumia vibaya mtalalamika sana, Ni bora sasa tukayapunguza madaraka ya rais), yametokea, cha kushangaza kuna watu walitaka Eti madaraka ya rais yaongezwe.
Tumlilie Mungu atajibu maombi;
Tufanyie kazi mawazo tuliyo nayo kwa pamoja - tutaona majibu. Tukikaa kimya watoto wetu watatudharau sana kwa sababu tutashtukia tuko katika hali ambayo hatuwezi kujikwamua. Kila kitu kikishakuwa chini ya maamuzi ya mtu mmoja, tutakwisha.
Kwa Tanzania hii wapo wanaoruhusiwa kutukana wenzao na wengine ni wa kutukanwa tu. Hii sio nchi tena ya sharia moja. Kuna mtu aliwatukana wazee wenzake kabisa eti malofa .. sikusikia hata mtu yeyote mwenye mamlaka akikemea kauli hiyo.
 
Pole sana mfungwa ila tunakuombea angalau ndugu wajichange wakuchomwe mapema, Maana huko ni kubaya ndugu yangu kila kitu ni ndio.
 
jamani wadau ilishindikana kabisa kumtolea faini?, kaka Mtatiro alikuwa wapi asimtolee kijana wetu. wengine tujifunze kupitia hili alipoposti watu tulimsapoti kwa kushare, kucomment na kulike mwisho wa siku amebaki peke yake bila msaada.
Mtatiro yupi wa cuf au wa kijani, ukiunga mkono unasamehewa dhambi zote unazaliwa upya na kufanya kiumbe kipya
 
Bashite na makontena yenye bilions ya kodi anachekewa tu.huyu mlalahoi anaonewa hata 200k hana maskini kosa lenyewe hata onyo halistaili.
Pole mnyonge
Kuna tofauti kati ya mpakwa mafuta mteule na msaga soli.
 
Back
Top Bottom