1) Nakumbuka wakati mi mdogo kutoka angani kulipeperushwa karatasi zenye picha ya Mwalimu Nyerere wakati huo akiwa Rais. Picha hiyo ilikuwa ikimuonyesha Rais akiwa ameshika kichwa huku akionyesha sura ya huzuni, majuto na masikitiko! Pembezoni mwa picha hiyo kulikuwa na picha ya mtu mwingine akiwa anatabasamu na kuonyesha furaha na bashasha huku akijaribu kumdhihaki Baba wa Taifa!
Naomba anaekumbuka tukio hili anieleze hiyo picha nyingine ilikuwa ni ya nani? Jee, haya yalitokea kote TZ au ni huku kwetu Kaskazini? pia nakumbuka watu waliamriwa kuchanachana hizo picha haraka na atakae kutwa nazo atakamatwa kama Mhaini!
2) Tukio lingine ambalo liko kichwani mwangu mpaka leo ni kutekwa kwa Ndege ya TZ na kupelekwa Uingereza, Jee, nani anakumbuka majina ya Watekaji, Wako wapi sasa, na walihukumiwaje?
3) Nakumbuka Mwalimu Nyerere alitangaza miezi 18 ya kujifunga mkanda! jee, hiyo miezi 18 ilikuaje? iliisha kama ilivyotarajiwa?
4) Nakumbuka Mwalimu alikuwa na Bakora aliyoipenda sana, jee, ni kweli kuna siku Malkia Wa Uingereza alimpa Mwalimu mkono uliovishwa mpira na Mwalimu kujibu kwa Bakora yake?