Mistubishi Pajero Jr Vs Toyota Cami

jino kwa jino

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
785
170
wandugu sijawa kutuma hizi gari wenye uzoefu naomba kujua lipi bora kwa matumizi ya Tz hasa DAR ES SALAAM, nina ka baloon linanipa hasara ya mafuta sana, nataka niagize dogo kati ya haymawili
Pjero Jr CC 1092 ya mwaka 1996/7 imetembea km 70,000
Cami CC 1290 mwaka 1999/2000 imetembea Km 100,000

nitafurahi zaidi nikipata uzuri na ubaya wa kila moja

mbarikiwe sana wapendwa watu wa mungu.
 
mkuu mi naskuma cami mwaka wa pili...na wala sijapata shida ya spare parts...ipo safi sana kwenye suala la mafuta...nakushauri uvute cami mkuu
 
Mimi nilikuwa namiliki Mitsubishi Pajero Mini, ambayo haina tofauti kubwa sana na Pajero Jr. Tatizo la hapa bongo ni kwamba, magari ya Mitsubishi yanahitaji umakini wa hali ya juu katika kuyatengeneza, si rahisi kama gari za Toyota. Mafundi, kama unavyowajua, huwa hawakubali kushindwa, hatimaye wanakuingiza hasara. Unatoa pesa nyingi, unatengeneza gari, mwisho wake inagoma, inaharibika, unaingia hasara, na kwa hasira, wala hutaki kumwona fundi aliyekuingiza mjini.

Suala la Cami halina ubishi. Ni gari isiyo na utata. Mwanzoni watu walilalama kwamba hakuna spare, lakini hicho kinatokana na (a) kutokujua kwa watu wanaojifanya wajuaji, na (b) ubabaishaji, ili mradi aonekane anajua, kumbe hajui.

Cami gari nzuri sana, haitakupa shida. Spare zipo na ni rahisi kuitengeneza.
 
thanks sana mkuu nimekupata vema
 
Back
Top Bottom