Mistari kwenye hip hop ya Bongo ilitia fora

Mistari kwenye hip hop ya Bongo ilitia fora

Mwanadamu ameacha dira moyoni anaona fahali,
mwongozo ameupa kisogo hatari,
walai kama kamali makaburi yanaongezeka mabwanyenye wanavinjari,
kama mchezo wa kidali,
pambano si la hatari sasa harufu ya damu inanuka kila mahali,
mpaka akili zinafyatuka kama ngedere wa mochwari,
watawala wameacha lengo kwanza wanalimbizika mali....... Kalapina
 
Usinione msela kisa jeans zangu kata k,nshazama nazo hadi ikulu we muulize hata jk-ngwair

nimeanza kwenye nyumba.sina presha na corola.seuze bajaji.naweza panda daladala,makondakta me washkaji so nasafiri kisela jmoe a.k.a mbakiaji
 
wanao Skiliza hawaskiii wanaoskia Hawaskilizi,, machizi si miujiza tunasonga namna Hii!!

Tunasonga Kwa Mwendo wa Farasi Au Kinyonga!!
Hawa jamaa kwenye hii track walipangilia mistari sana ,ni moja ya track bora kwa mtazamo wangu .
 
wale wakongwe wenzangu watakubaliana nami kuwa hip hop ya bongo haikuwa nyuma katika mistari makini ,majigambo na style za kutisha. Kwa sasa wapo vijana wanaoweza kuuendeleza music huu hapa bongo ila kuna vionjo vinakosekana haswa matambo ya kipindi kile.

Hebu tujikumbushe tambo za enzi zile sio mbaya pia ukaweka tambo za mistari ya kipindi hiki.

Prof jay (nigger jay)-wimbo wa funga kazi(hbc)

''kwa jay mtapata maneno makali na mengi ya kashfa mfululizo,
iwe ni onyo na funzo,
kwa wanye kelele pasipo uwezo,
wanatumia vigezo,
unataka kurap pasipo na nyenzo,
hayo ni mambo ya chezo,
kutokataa maelekezo wakati huna uwezo''

imam abas -wimbo mitaa ya kati
''niguse bahati mbaya ,nikuumize makusudi''

mr. Ii-sugu (ii proud)-wimbo mikononi mwa polisi
''afande anataka kilo,
mfukoni mimi na zero,
nazidi kuwa mwenyeji ndani ya sero,''

simple x -wimbo nawakilisha
''natikisa bongo visiwani mpaka bara,
nimekuwa kinara ,
kila kitengo mi nang'ara,''

endelea....

tetete mi nakumbuka hiiii

profesa jay....alieuziwa cheni katoa hela ya bandia na aliyepokea hela uza cheni katoa ya bandia
gwm....daladala yenyewe mia 150 ni bola niende kwa mama ntilie anijazie..nipate flesh
tmk family....una act ukaa upanga kumbe kwenu keko mwanga halafu inasemekana bibi yako mwang
juma nature...vuguru za mbembechai watu tulikuwa hatunywi chai
profesa jay...rudi mwanyamala ohh mateja kibao katiza saa moja moja uone roba za mbao
manzese crew...usiombe wavae nguo zao halafu wanaime na ukame lazima usimamee
afande sele....kama alieanzisha ccm imeondoka bila kuaga na ndivyo ccm itaondoka bila kuagwa
gagwe mobb....nataka kwenda msanga ooh nauli bure..chii watu ngangalii kinomaa
mabaga flesh..mtulize kisa muulize akileta jeuri mtwange mtu ngumi jiwe....
Fleva unit..kama jimbo la ubungo mnaaongoza ccm ipo litaenda upinzani ilikuwa mwaka 2001
fid q...huyu anapedwa yule ana damu ya kunguni...huyu mademu yule sabuni
 
Vp dj haupgi hewani.na unasikiliza getho.hizi vocal chumbani demu wako anapgia nyeto, q hebu kata hyo instrumental,usishndane na sis utakuwa mento by ngwair.

Wanataka namba ya simu waruke hewani,waje wapajue skani,tuwachumishe mboga flani by ngwair.
 
Haimaanishi ukiwa baba,basi vijiti huwezi zaba,jcb mbna ni baba tena jirani yake shaba! -bonta!
Ukipinda kinondoni,utanyoka segerea -bonta.
 
hajui bei ya topaz..,na kwake vuz.i laota!..solo thang
 
"Simba mwenye njaa hashibi ubuyu,ni tai sio mbayuwayu......"MWANAFA ktk albam ya MWANAFALSAFANI
 
"Dunia tambara bovu nalidekia kwa shida,najaribu kui'solve bila kutumia four figure". "Umasikini unanipodoa bila kutumia cosmetics,daily unanizodoa unanivuta kama magnetics".

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
HUYU JAMAA. wanamuita kaka poa huyu jamaa, wanamuita mtoto wa mama huyu jamaa,sijui ni dhiki au laana huyu jamaa,naomba Mungu anamsaidie maulana. BONGE LA SONGI BONGE LA BEAT.

walikuwa wanajiita Born Crew..nimeutafuta huo wimbo bila mafanikio
 
Back
Top Bottom