Mistari kwenye hip hop ya Bongo ilitia fora

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,719
1,440
Wale wakongwe wenzangu watakubaliana nami kuwa Hip Hop ya Bongo haikuwa nyuma katika mistari makini ,majigambo na style za kutisha. Kwa sasa wapo vijana wanaoweza kuuendeleza Music huu hapa Bongo ila kuna vionjo vinakosekana haswa matambo ya kipindi kile.

Hebu tujikumbushe tambo za enzi zile sio mbaya pia ukaweka tambo za mistari ya kipindi hiki.

Prof Jay (Nigger jay)-wimbo wa Funga kazi(HBC)

''Kwa Jay mtapata maneno makali na mengi ya kashfa mfululizo,
Iwe ni onyo na funzo,
Kwa wanye kelele pasipo uwezo,
Wanatumia vigezo,
Unataka kurap pasipo na nyenzo,
Hayo ni mambo ya chezo,
Kutokataa maelekezo wakati huna uwezo''

Imam Abas -wimbo mitaa ya kati
''Niguse bahati mbaya ,nikuumize makusudi''

Mr. II-Sugu (II Proud)-wimbo mikononi mwa polisi
''Afande anataka kilo,
Mfukoni mimi na zero,
Nazidi kuwa mwenyeji ndani ya sero,''

Simple X -wimbo Nawakilisha
''Natikisa bongo visiwani mpaka bara,
Nimekuwa kinara ,
Kila kitengo mi nang'ara,''

Endelea....
 
KURA YANGU: DR LEVY FT SUGU & NATURE

kura yangu toka mikononi mwangu
napiga kumchagua kiongozi wangu
atakae ongoza nchi yangu
niliopewa na Mungu
isiwe kura ya kula
nikapata hasara
kwa kumchagua kiongozi aliekosa busara
tusiwe na mawazo fukara
tukageuza biashara zoezi la upigaji kura
tusichague mradi chama tuangalie ubora wa sera
kura yangu iwaondolee adhabu bibi na babu
kwa kutembea maili nyingi kwenda kufata matibabu
nikashindwa kumlaumu kati ya waziri na katibu
kaka zangu huko jela isiendelee kuwasulubu
napoenda mahospitalini manesi wawe na adabu
kura yangu iwapunguzie machungu
kwa ndugu zangu kufukuzwa machimboni
salamu mpaka mbuguni
MZAWA ANAPOONDOLEWA
MGENI ANAPOKELEWA

MIAKA MITANO MWANZONI USHURU ANAFUTIWA
nisingependa mambo aya tuendelee kutendewa
kwa yeyote mwenye akili nachosema nakielewa
wanamuziki atufiki
tunakosa hatimiliki
wabunge wetu watarajiwa kasemeni vikaoni
naamini ata nyie hampendi tushinde vijiweni
HACHENI FIKRA POTOFU KUWA HAKI IPO MBINGUNI

CHORUS : BY SIR NATURE.
nawauliza viongozi waliosimama
ni yupi kati ya wale tumpe dhamana
aweze kutuongoza tuishi kwa amani
maisha bora mijini na vijijini
hakika sasa jibu ninalo kichwani X 4
 
Me ninaweza fanya hadi madawa yakaugua -jasusi fid q
2.kama biashara ya madini,migodi yote naimiliki mimi by mwanafa
3.don kama corleone,maadui wangu hawaponi by fa
huu uzi unabidi uwe sticky!
 
Wao wanawachunga mademu zao kwa bakora,sisi tunawachunga kwa condomu nani bora by nick wa pili
2. Wingi wa mashori si kipimo cha urijali,kama we mwanaume wa kweli nyumbani wapate ugali by nick
3.watakuwa makahaba,wadogo zangu nikicheza! Nick.
 
dEMU AKISEMA ANANICHUKIA,NAMAANISHA ANANIZIMIA,KICHECHE AKINIKMBIA MWACHE ATARUDI ANALIA
2. TUSIGOMBANIE VICHECHE HUO NI URITHI WA KWETU,YOTE YAWEZEKANA,PEKU PEKU AU KWA VIATU
3. KAMA ULIDATA UKAMUONESHA UTUPU MKWEO,UTAMUANGALIA VIPI LEO?
ZOTE FA!
 
Kuna ngoma ilifanywa na Bongo records team inaitwa "bongo cherea pina" - lwp majituu primitive wanakwambia....tupo hapa,tumeshachanganyikiwa nakudata,tukikamata maiki tunaishambulia kama mbwa mwitu,we mtoto wa mama sisi utuelezi kitu....
......mchuma pelu,tuliza maweruweru,yakhee karibu bas chakula upate japo kikombe cha gahawaa,kama mali ya mtu yaliwa kulaa,,,alafu linapigwa chorus usawa ni mgumu ata ukivuta ndumu watu yeyaah ikizidi sana jua utakula sumu watu yeaaaah eeh ngangari waaah waaah watu kumbe ngangari wansegeju..Gangwe mob hao hahahaha dah wapi babuuu.Babu alipogombana na Luteni akamuimba...gangwe imekulea,hadi mke imekuolea,Leo unaikandia?...hahaha babu noma sana enzi zake.
 
HUYU JAMAA. wanamuita kaka poa huyu jamaa, wanamuita mtoto wa mama huyu jamaa,sijui ni dhiki au laana huyu jamaa,naomba Mungu anamsaidie maulana. BONGE LA SONGI BONGE LA BEAT.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom