Mistari dadisi: Roma ft Jose & Darasa!

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,120
37,674
Katika ngoma mpya ya Roma aliowashirikisha wakali wengine, Jose na Darasa, kuna mistali kadhaa inaeleweka na mingine inahitaji tafakuri shirikishi ili kwa sisi wafuasi wa Hip Hop itupe ile kitu roho inapenda. Binafsi nimeokota ifuatayo:
Roma: Jamaa humu katambaa na mistari kibao inayoeleweka haraka haraka, haiitaji udadisi sana, hapa naweka ile inayohitaji udadisi!
Siku hizi kila demu ukimuuliza “naishi Mbezi………!” hili ni dongo la wazi, tupeane udadisi wapenda hip hop. Hili dongo la mrembo gani ama la wote?
Mstari mwingine huu: when I’m gone, mikoba ntawapa central zone! Hapa napo Roma anawalenga kina nani?
Roma tena: “… sio unadiss tu na kwenye show unapigwa mawe”
Wadau tuambiane, ni nani huyu?

Jose:
Jose Mtambo nae kama kawa. Ana mistari kibao ipo dhahiri shahiri kwetu watu wa tasnia, lakini nae kama Roma, katia mistari tata, mifano hii hapa!
Sikuwa sober, natoa ngoma kali na viroba! Hili lazima litakuwa ni jibu kwa watu fulani, je ni kina nani hao?
Nawazidi umri, siwezi kuwa shemeji yao, wanajua wazazi wao, mi dingi yao!
Hapa Jose kawapa ukweli watu anaowajua kuwa wana madharau, tuambiane tuwajue, nani hao!
Hawajui kuchana mnaskiliza kelele zao!
Jose anatuaminisha kuwa kuna watu katika Hip Hop wanapiga kelele tu, na sio kuchana!
Mi najua ni mchawi afu unajiita …..!
Jose ana-declare kuna mtu anamchawia, nani huyu?
Nshakujua ntakushika kwenye kilima!

Na yule "mchawi" wake anampa promise kuwa atamshika tu, na Jose anapajua pa kumshikia, napo ni kwenye Kilima.

Darasa: Huyu nae akafunga kazi kama wenzie tu
…Sina mistari ya majungu, nikikuchana nakutag! Darasa anaweka wazi, hamuogopi mtu, tupeane mfano jamani!
….Ukienda dukani anauza Mr. oyooh oyooh…!
Inasemwa Sele ni mkali, Mtaani Solo ni mkali, ila dukani ni Mr. Oyooyoh! Ndio nani huyu? Tukumbushane!
Unaweza mwambia mtu ukweli akahisi unamkejeli!
Jamani, nani huyo alihisi kukejeliwa na Darasa?
Kaka mkubwa kuwa makini, muwa huzamishaga meli…!
Daah sina uhakika na matamshi ya Darasa hapa na kile nilichoskia mimi, lakini tunaambiwa na Darasa kuwa kuna ukweli huisiwa kejeli, na pia Muwa huzamisha Meli!
 
Mtambo mtu wa kunywesha sana na story kibao kuwa jamaa mlevi so anatoa ujumbe kuwa akipiga viroba anatoa mistari mikali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom