Missed connection: ''kaka, Samora Road ndo iko wapi?''

Missed connection: ''kaka, Samora Road ndo iko wapi?''

Noma sana...huko posta ma diva wa design hii wapo sana sijui wengine ndo micjongo yao ...hua wana tokea from nowhere.
 
Lipa kodi ya nyumba usije sahau... Mama ntilie kamlipe pia. But story yako kipaji tosha umeipanga in high definition.
 
Hamjagundua tatizo? Alikuwa na buku asubuhi wakati anaamka, chai kabomu, jero katoa nauli, sasa si tayari ni uhanithi atampeleka wapi mrembo?

Sasa hivi ishu iliyompeleka taun ishalipa sasa kidume kimedinda wakati mrembo hayupo. Just thinkin' loud
Kwa style hii ya vichochoro na kutembea kwa mguu atabaki kuwaita watoto wa posta shemejiiiiiii
 
Mademu siku hizi huwa wanafunguka wenyewe sema na wewe j3 tshrt black chini ukaki na tims akajua baunsa wa bills.Huwa miguvu mingi akili hamna.

Ungepiga hata ushati wa draft.

Natania ila next time wajambia mbali hawacheleweshwi unachukua namba fasta.
 
yaani wewe nakuonea huruma laiti kama ungelikua karibu na mzee kifimbo cheza na hiyo lugha yako.
 
Mkuu wangu Kiranga, kwakweli kwa uzembe nilofanya leo, nastahiri bakora! Ila kichwa kilikuwa kimejam that time Mkuu.

Sikucheza kama Pele, ona sasa ninahamaki !
Hakuna uzege hapo mkuu Pengine halikua zali lako!
 
Umembwela mwamba sio kesi lakini bila doo mfukoni hata mm sound zinapotea tu
 
Leo J’tatu nikaamka mornie sana, nikaenda ground kupasha tizi kidogo ili kuweka mwili fit. Then nikarudi geto mishale ya saa 1 asubuhi. Nikawa nimechill pale nje ya geto nasubiri mwili upoe ili nikapate ‘shower’ ya kopo. Nikaanza kuwaza mawili matatu pale, maana niliamka sina ramani kabsa kwa siku ya leo, channel zote chenga. Nikawa nawaza leo nitaweka vipi luku wakati sina ata buku?!! Afu kodi ya chumba alarm ishagonga since March mosi. Majangest!! Uwanja mkavu… refa kauzu, kilichobaki kucheza rafu! Ama kweli huku site mambo tight sana ndugu zangu, walahi ipo siku nitaenda kuomba ‘poo’ kwa mungu wa Kakobe animwagie mavumba! Japo mungu wa Kakobe ni mbaguzi, anataka waumini waliotusua tu, alienacho ndo anaongezewa… YES, no fairness chini ya jua.

Mishale ya saa 3 ivi, napata text ya mchizi. Oyaa kiongozi pande zipi mida hii? Nikamjibu nipo kitaa tu babu, sina mchongo. Akanijibu dondoka downtown fastaa, kuna inshu. Nikasema barida, dakika sifuri nitamwagika hapo. Maana akina sie tuliofuzu ElimuMtaani.Kom … ‘deiwaka’ (ila sio mazabe) ndo zinatuweka mjini. A Mastermind hana MaterPlan. So the MasterMind must link na mwenye MasterPlan ili to make things happen! Makomredi wa uswazini na mahustlers wa town wananielewa vizuri hapo! Kuishi uswazi form SIX. Kuzaliwa Darisalama chuo chikuu. Mishe twenti four seven, and Alhamdulilah life goz’on. Maisha nguzo yake ushujaa, alishasema mkongwe Salu-T.

Fasta sana nikazama bafuni kupata ‘shower’ ya kopo. Then on my way to downtown. Navuka chochoro kadhaa kukaribia road kubwa, mara namuona mama ‘ntilie akitoa huduma ya asubuhi. Supu za kongoro, maandazi, chapatti, na mazaga mengine kibao yanapatikana hapo. Tunafahamiana huyu mama. Nikamtonya… mama eeh, aaagh mimi leo mambo sio mambo, sa tunafanyeje bi’mkubwa. Mama akanata na beat. Anaelewa maisha ya mtaa. Chapati mbili nzito plus harage nazi… nikapelekwa pwani! Then huyooo nikala kiatu kuelekea stand ya daladala.

Road ilikuwa nyeupe, no foleni wala mizengwe. Kulikuwa na kimvua in aste aste mode. A couple of minutes, nishatimba downtown posta. Nikaanza kuikata mitaa kumfuata mchizi alipo. Posta bhana, asali tupu. Kila demu unaepishana nae ni diva. Kila demu ana ‘screen chogo’ nyuma utadhani wanachambia hamira. Vidume ni mwendo wa ‘kuvunja shingo’ tu na kushangilia uumbaji wa mwenyezi Mungu, japo nawadeiz Mchina nae ni ‘steki-holder’ kwenye uumbaji wa dada zetu. Hawa wadada wa darisalama walivyonona, usipokuwa 'cost-conscious' walahi utaishia ‘kukata mpunga kama Kyela’ na usijenge ata kibanda uswahilini. Wadada wana ‘mikia’ yani utadhani ya maonesho sabasaba. Mdada yupo posta, anajambia salender bridge. Kha! Ila zote hizo ni neema za ALLAH. Mimi huwa navunja shingo nakula kwa macho, kisha nasema ‘tawire’! naendelea na mishe zangu. Ndo maana hatung'oki mjini ata kwa greda za Heche Saguti. Ila mind you... msije mjini (in mwana F.A voice). lol

Mishale ya saa 5 ivi, nishaonana na mchizi keshanipa mchongo. Naelekea point B nyingne fulani kupitia pale jengo la Posta mpya. Pale koridoni posta mpya, zero-brains na mabitozi wanapouzia sura na kutega mademu. Nikazama ndani ya jengo la posta ili 'nile kipupwe' dakika kadhaa. Alaaa bongo joto bhana! nikaegesha mule ndani for some minutes afu nikatoka nje pale koridoni ili sasa niendelee na direction yangu. Ile natoka nje tu pale golini usawa na ile stationery ya nje, nakutana na bro mmoja ivi ambae hatukuonana since back in ze dei kitambo. Ni mshikaji wangu sana huyu. Ni homeboy. Trading stories ika-kick off promptly. Za miaka mingi niaje, mitikasi vipi apa town, tuka-exchange madini, and blah blah.

Tukiwa tunaendeleza stories pale na uyo bro, mara ghafula nasikia ‘sauti ya kwanza’ inaniongelesha, nikavunja shingo kumsikiliza…

Binti: Kaka, samahani…

Mimi: Bila samahani best… ehee nambie (with an intensive concentration)

Binti: Naomba kuuliza, eti ‘Samora Road’ ndo iko wapi?

Mimi: Ahaa, sa sikiiza… nyosha moja kwa moja, usipinde kokote, we nyosha tu, utaona sheli apo kati, endelea tena kwenda mbele mpaka uone round-about yenye mnara wa askari kashika bunduki. Yani kwenye hiyo round-about kuna sanamu ya askari kashika bunduki. Hapo kwenye round-about, utaona barabara nyingne inashusha kaskazini yaani kushoto kwako, ama inapandisha kusini yaani kulia kwako. Hiyo street ndo Samora Road. Hope umenisoma fureshi.

Binti: Yeah nimeelewa, nimeelekezwa maduka la samsung mtaa huo. Ahsante sana.

Mimi: Alight, haina nowma. (demu akasepa huku mie ‘nikivunja shingo’ kiaina ili kufanya ‘tathmini’ ya macho mpaka alipo-vanish)

Convo hiyo iliteki place within dakika sifuri kati ya mimi na mrembo uyo mwenye sura nzuri sana. Mrembo fulani ivi lainiiiii, nahisi hawezi ata kubofya remote. Black beauty fulani ivi mixa chocolate. Ana sura nzuri sana, na ‘vishimo’ shavuni kwa mbaaali akiwa anaongea. Sura yake ndo alinivutia zaidi, moyo ukalia ‘paaaah’ juu kwa juu. Pia nyuma 'mjengo' anao, ‘nyoro’ inaita si haba. Chini alikuwa amevaa trouser jeans blue mpauko (if my memory serves me well), juu alitupia simple top rangi ya kijivu (dizaini kama cotton laini au shifonni ivi). Kwa tathmini yangu ya haraka, kichuna yule ni ‘foreigner’ hapa jijini.

We mrembo, kama utasoma uzi huu, please hebu do the needful. Mimi nilivaa trouser kadeti ya kaki with American boot. Juu nilitupia tshirt black. Mkononi nilishika nokia ya tochi. Please, ebu sema japo ‘hi’ tu moyo wangu upone! Teh

Tangu mida ile mpaka usiku huu naandika thredi hii, mind yangu umeiteka na moyo wangu umeupeleka gereza la mahaba! Nakuona kabsa they way you were kindly asking me. You looked very innocent lady. It’s my sincere anticipation that tonight you are going to wave ‘kitambaa cheupe’ in my dreams.

To Love A Stranger…. Njiwa peleka salaamu!


- Kaveli -
Duuh mwana, kama ulikuwa hujui kipaji chako ngoja leo nikusanue.

Kazi ya Erick shigongo unaiweza braza. Haha
 
Noma sana...huko posta ma diva wa design hii wapo sana sijui wengine ndo micjongo yao ...hua wana tokea from nowhere.


Upo sahihi Mkuu, mademu wa posta ndo mikato yao iyo. Wengine wanakuwa wapo 'kazini' in that style.
 
Mademu siku hizi huwa wanafunguka wenyewe sema na wewe j3 tshrt black chini ukaki na tims akajua baunsa wa bills.Huwa miguvu mingi akili hamna.

Ungepiga hata ushati wa draft.

Natania ila next time wajambia mbali hawacheleweshwi unachukua namba fasta.


Mkuu nilinoga fureshi sana. Nilitinga simple american boot ya shingo fupi kabsa (not yale matims ya kibaunsa) hahaa. Kwenye kutupia am professional. When it comes to 'dressing code', the DOs & DONTs are at my finger tips. Njoo nikusupply maujanja ktk sector hii. Teh

Kweli wajambia mbali siyo wa kuwakawiza. Ila pia dizaini kama baadhi ya mademu wa posta ndo mikato yao iyo, coz hizi situations zishanitokea mara kadhaa huko huko mitaa ya postal na yote sikumbwela. Isipokuwa hii ya jana ndo cha ajabu nikaichukulia poa kabsa.

Naanza kuiwaza baadae sana usku. Nowma sana mzazi
 
Puli inakuhusu blaza...kweli __nge huja baada


Hahahaa ngenye huja baada. Umetisha sana mkuu. Nimefika geto eti ndo ngenye zinaanza kuflash back the diva. Nouma sana
 
Hakuna uzege hapo mkuu Pengine halikua zali lako!

Bora wew Mkuu umefikiria nje ya box la wachangiaji wengi. Surely hilo halikuwa zali langu, coz mitaa iyo iyo ya posta huwa nakutana sana na mikasa iyo na huwa nacheza kama Pele. Ila surprisingly jana yule gashi nilimchukulia poa kabsa. Cjuw kwa vile head ilishajam na mitikasi ya doo
 
Umembwela mwamba sio kesi lakini bila doo mfukoni hata mm sound zinapotea tu


Yep, kula tano baharia. Bila mavumba, huwezi kupangilia ngenga fureshi. Uchawi wa kizungu ndo lubricant muhimu sana ktk mitongozo. Ila haina nowma, barida tu.
 
Duuh mwana, kama ulikuwa hujui kipaji chako ngoja leo nikusanue.

Kazi ya Erick shigongo unaiweza braza. Haha


Hahahaa mkuu nakufa njaa uswazi wakati kumbe naweza fuata nyayo za Shigongo nikapiga hela. Lol. Sasa let me develop this damn talent. Sometimes it needs talent to discover your pure talent. Haha
 
Talent ya kuandika unayo,.mi nikidhani ni lara 1 karudi kivingine
 
Back
Top Bottom