Miss Tanzania

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,784
Reaction score
12,592
STORY OF MISS TANZANIA SEHEMU YA
KWANZA
?Patrick amka basi darling inakaribia saa nne
sasa?Alisema Veronika kwa sauti laini ya
kubembeleza.
?Mmmmhhh?Aliguna Patrick ,akajigeuza
upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.
?Amka basi bwana uende ukaoge?Alizidi
kubembeleza Veronika
Kwa uchovu mwingi Patrick akaamka na
kunyoosha mikono yake juu huku akijipinda
?Loh !I?m veeery tired?Akasema kwa uchovu.
?lakini ukishaoga uchovu wote utaisha my
darling ?Akadakia Vero.
Kwa uvivu Patrick akajiinua kitandani na
kuelekea bafuni .Dakika chache baadae alitoka
akiwa amechangamka.
?Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu.Sasa
najisikia saafi kabisa.Nadhani itabidi kwa
sasa nipunguze muda wa kufanya kazi
.Nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi
sana kwa siku kiasi kwamba nakosa hata
muda wa kupumzika.naogopa tukija kuonana
nisije kuwa nashindwa kutimiza majukumu
yangu kama mume kwa sababu ya uchovu?
Vero akatabasamu halafu akatoa kicheko cha
chini chini na kusema
?Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kujaribu
kupata muda wa kutosha wa kupumzika.?
?Nitajitahidi baby?
Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero
akamshika mkono Patrick na kumpeleka
sebuleni kupata stafstahi.
?Patrick dear nataka unisindikize Supermarket
nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani .Si
unajua kesho Andrew na vicktoria wameahidi
kututembelea?Alisema Veronika wakati
wakiendelea kupata chai.
?Mhh Vero we nenda tu mwenyewe mi niache
nipumzike bwana?Patrick akajibu
?jamani dear usifanye hivyo naomba bwana
unisindikize ,mi naona uvivu kwenda peke
yangu?
?haya mama ,tumalize twende ili tuwahi
kurudi?
?Nashukuru dear?
Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa
kuwa navyo ni uwezo wake mkubwa wa
kushawishi.
*********************************************
*********************
Veronika Rugi alikuwa ni binti mrembo
mwenye mvuto wa aina yake.Binti huyu licha
ya kujaaliwa kichwa kizuri chenye nywele laini
,nyingi na ndefu ,alikuwa na uso mpana wa
mviringo ulionakshiwa na macho mapana
yenye kurembua muda wote.Midomo mizuri
,laini ambayo akikupiga busu hutatamani
abanduke.Mtoto huyu alijaaliwa shingo murua
ambayo iliungana na kiwiliwili kilichokuwa na
kifua chenye kupendeza kilichobeba chucu
changa zenye kusisimua,zenye kuwatoa
udenda wakware.Kimwana huyu mwenye uzuri
usiopimika alijaaliwa umbo la utatanishi
kuanzia kiunoni kushuka chini.Ni mabinti
wachache sana waliopewa upendeleo wa
namna hii na manani..
Pamoja na sifa hizo zote za nje lakini bado
alikuwa na sifa lukuki za ndani.Kikubwa zaidi
kinachomfanya apendwe na kila mtu ni uwezo
wake mkubwa wa uelewa .Ni binti mwenye
roho nzuri ya huruma na upendo asiyependa
kujivuna wala kujikweza licha ya uwezo
mkubwa familia yake ilionao.Ni binti mwenye
heshima kwa watu wa rika zote
,mcheshi,asiyependa ubinafsi na zaidi ya yote
ni mtu anayejua kupenda.
Veronika ambaye bado anaishi na mama yake
mzazi baada ya baba yake kufariki miaka
kadhaa iliyopita ,alikuwa ni mtoto wa tatu na
wa mwisho katika familia ambayo
haikubahatika kuwa na mtoto wa kiume.Dada
mkubwa wa Veronika aliyeitwa Loniki hivi
sasa anafanya kazi katika shirika la ndege la
British airways ,ameolewa na anaishi nchini
Uingereza.Mtoto wa pili kuzaliwa katika
familia hii ni ni binti mrembo sana Sarah
ambaye aliwahi kushika nafasi ya tatu katika
kinyan?anyiro cha kumsaka mrembo wa
taifa.naye amekwishaolewa na ni afisa
mahusiano wa benki moja mpya kabisa nchini
iitwayo African meckat bank.Mtoto wa tatu na
wa mwisho ni Veronika ambaye bado
hajaolewa ,ila alikuwa katika hatua za mwisho
za kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na
mchumba wake Patrick.Ni hivi karibuni tu
amehitimu shahada yake ya kwanza ya
biashara katika chuo kikuu cha dar es
salaam.Yeye ndiye msimamizi mkuu wa
miradi yao yote ya familia kwa sasa.
*********************************************
*********************
?basi nikwambie mpenzi nilisahau kukwambia
toka mapema kuwa dada Loniki alifurahi sana
kusikia kuwa tunataka tukafanye shopping ya
harusi yetu nchini Uingrereza,nakwambia
alifurahi huyo na akaahidi kuwa yeye na
mumewe watagharamia safari nzima ya
kwenda na kurudi na gharama zote za
manunuzi.Amesisitiza kuwa tusitumie hata
shilingi yetu.Kwa maana hiyo wiki hii nataka
niende tena kufuatilia yale maombi yetu ya
viza pale ubalozini.Nadhani kama Mungu
akijaalia basi ndani ya wiki mbili zijazo
tutakuwa tumeshakamilisha taratibu zote
zinazotakiwa.?
Alisema Vero huku akijiegemeza karibu zaidi
na kifua cha Patrick.Muda huo ilipata saa
mbili za usiku na bado walikuwa wakipunga
hewa safi baada ya mlo wa jioni.
?Wow! Hongera sana Vero kwa kuwa na ndugu
wakarimu na wenye upendo wa hali ya juu
sana kama ulivyo wewe.Tena umeongea
kuhusu Loniki nimekumbuka na zile CD
alizonitumia wiki iliyopita.Unajua sijatazama
hata moja.Hebu twende ndani nikaitazame ile
CD mpya ya Jack bauer.?
Alsema Patrick huku akijiinua toka pale
walipokuwa wameketi na kuelekea sebuleni
.Vero naye akakusanya vitu vyote
vilivyokuwapo hapo chini naye akaingia ndani.
?Vero mbona ile CD ya Jack bauer siioni
hapa?au Andrew aliichukua?Aliuliza Patrick
baada ya kuitafuta CD ile bila kuiona.
?Yawezekana Andrew atakuwa aliichukua kwa
sababu siku ile aliing?ang;ania
sana.Nakumbuka kuna CD alizichukua hapo
nadhani na hiyo nayo ilikuwapo.?Akasema
Vero
Patrick akalifunga kabati ,akaelekea katika
friji akafungua na kujimimia Juice katika glasi
.Vero alikuwa ameketi sofani akitazama
Luninga.
?basi nakwambia Patrick ,Miss Tanzania ya
mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa
sana kwa sababu mabinti ni warembo kupita
maelezo.Mhh???..?
Alisema Vero huku amekodoa macho yake
katikaLuninga kubwa iliyokuwamo humo
sebuleni.
?kwani fainali za miss Tanzania ni
lini??Patrick akauliza
?Ni jumamosi ijayo na itafanyikia pale
Diamond Jubilee.Kutapambwa na onyesho kali
la machozi band,vile vile wana Fm academia
na wasanii wengine kibao.Nataka kesho
nikakate tiketi zetu za V.I P ili tusikose nafasi
siku hiyo?Alisema Vero
Akiwa na juice yake mkononi Patrick
akajisogeza taratibu kuelekea mahali alipokaa
Veronika .kabl;a hajafika sofani alisimama
akapiga funda la juice kisha akaelekeza
macho yake katika luninga
?Naitwa Neema jastin ni mrembo toka kanda
ya kaskazini.Ni miss Arusha.napendelea sana
muziki wa dini,kusoma na michezo mbali
mbali.Nategemea kuja kuwa mwanamitindo
wa kimataifa.Iwapo nitachaguliwa kuwa miss
Tanzania nitajikita zaidi katika kuwasaidia
watoto yatima kwani naelewa mateso na
machungu wanayaoyapata kwa kutokuwa na
wazazi wao.Naombeni kura zenu namba
yangu ya ushiriki ni ishirini.?Alikuwa ni
mrembo wa Arusha akijinadi katika kipindi
maalum cha kuwatambulisha washiriki wa
kinyang?anyiro cha kumsaka mrembo wa
Tanzania kilichorushwa moja kwa moja na
televisheni ya Taifa.
?Du! Si mchezo?Aliguna Patrick huku
akisogelea zaidi Luninga
?nimekwambia Patrick warembo wa mwaka
huu si mchezo .Hebu kaa uangalie jinsi watoto
walivyobomba?Alisema Vero
?Naitwa Happy kibaho.Ni mrembo wa wilaya
ya Ilala .Napendelea sana muziki laini,kusoma
hadithi ,magazeti,kutazama luninga,na
wanyama.nategemea kuwa mwanasheria.Iwa
po nitachaguliwa kuwa miss Tanzania
nitaelekeza nguvu zangu zote katika
kuwasadia vijana wajasiria mali ikiwa ni
pamoja na kuwatafutia wafadhili,nitaitumia
kofia yangu kuiomba serikali ielekeze nguvu
zake zaidi katika kuwasaidia vijana hawa
katika kuwapatia mitaji na kuwatafutia
masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha ili
kupambana na ongezeko la vijana wasiokuwa
na ajira.Ninaomba kura zenu ili niweze
kulitwaa taji hili la miss Tanzania kwani nina
vigezo vyote vya kulitwaa taji hili .Namba
yangu ya ushiriki ni 6.?
?Whaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.............
...........?Patrick Alipiga ukelele mkubwa
?Nooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!..I cant
?????????alishindwa kuendelea glasi
aliyoishika ikamponyoka na kuvunjika
.Taratibu nguvu zikaanza kumwishia
akadondokea sofani kisha akapoteza fahamu.
?Patrick ,Patrick what?s wrong!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
!!!!!!!!!!!!!!!.........?
Alihamaki Veronika huku akimsogelea Patrick
pale sofani na kumtingisha.
?Patrick darling what?s wrong with you?
Alizidi kuuliza Vero huku akimtingisha.
?Oooooh!Nooooooooooo!!!!!!!!Wake up
Patriick?Alipiga ukelele baada ya kugundua
kuwa Patrick hakuwa na fahamu.Vero
akataharuki asijue afanye nini.hakukuwa na
mtu yoyote wa karibu ambaye angeweza
kumsaidia .Alitoka kutaka kwenda kuwaita
majirani ,akafika mlangoni na kurudi tena
ndani mpaka sofani alipolala Patrick.
?Patrick ,Patrick dear what?s wrong with
you.Whats?s wrong Patrick!!!!!!!!!!!!!!?Vero
aliongea peke yake huku machozi
yakimtiririka.Pale pale akapata wazo la
kumpeleka Patrick hospitali.Kwa nguvu zake
zote akamuinua Patrick na kumpakia garini
,akakimbia kufungua geti kisha akaingia garini
na kuondoka kwa kasi ya ajabu pasina
kufunga mlango wowote wa nyumba.
Mpenzi msomaji endelea kufuatilia riwaya hii
katika sehemu ijayo?
 
ENDELEA.............
Ilichukua kama nusu saa hivi toka Andrew
apate taarifa ya ugonjwa wa patrick,kuwasili
pale hospitali.Akiwa na mpenzi wake Vick
walishuka garini na kukimbia kuelekea
mapokezi.Mara tu baada ya kuingia hapo
mapokezi walilakiwa na sura yenye kusawajika
ya Vero.Alipowaona Andrew na Vick wakiingia
humo hospitali Vero aliangua kilio ambacho
kiliwachanganya zaidi
?Where is Patrick???Andrew akauliza huku
akijikaza lakini ni wazi alikuwa akitetemeka
?Calm down Vero tuambie Patrick yuko
wapi??Aliuliza tena Andrew .Vick
akamkumbatia Vero huku naye machozi
yakimtoka.
Andrew alimfuata nesi aliyekuwa mapokezi na
kumuuliza juu ya hali ya Patrick.Hakuridhika
na jibu alilolipata ,kwa kasi akakimbia hadi
katika ofisi ya Dokta Heneriko lakini
hakumkuta.Taratibu akatoka humo ofisini
jaso likimtiririka na kurudi mapokezi.tayari
Aloicy kaka yake Patrick alikwisha wasili hapo
hospitali akiwa ameongozana na mke wake
nao wote waliungana na Vick katika
kumbembeleza Vero.
Andrew akawasalimia kisha akamvuta mkono
alois wakasogea pembeni kidogo.
?Hebu niambie Andrew kitu gani
kinachoendelea hapa na Patrick yuko wapi ?
Aliuliza Alocyhuku naye jasho likimtiririka
?Brother Aloic hata mimi mpaka muda huu
sielewe chochote kwani toka nimefika hapa
muda mfupi uliopita sijaweza kuongea lolote
na Vero.Ila kwa maelezo niliyoyapata toka
kwa nesi ni kwamba Patrick yuko katika
chumba cha huduma ya kwanza akipatiwa
matibabu.Nasikia ni mstuko ndio uliopelekea
akapoteza fahamu?
Mara dokta Heneriko akatokea.Nesi
aliyekuwapo mapokezi akamtambulisha kwa
akina Andrew.
?Dokta hawa ni ndugu zake na Patrick
wamefika saa hivi na walikuwa wakitaka
kupata taarifa juu ya maendeleo ya mgonjwa
wao?
Dr henry akawasalimu wote halafu
akawaomba Alois na Andrew wamfuate ofisini
kwake..
?Vijana wangu kwanza poleni sana kwa
matatizo ?
?Ahsante sana dokta tumeshapoa?Walijibu
kwa pamoja
?sasa vijana wangu nimewaiteni hapa ili
tuongelee zaidi suala la ndugu yenu..Patrick
aliletwa hapa kwangu usiku huu akiwa
amepoteza fahamu.Kwa haraka nikisaidiana
na madokta wenzangu tumejitahidi kumpatia
huduma ya kwanza na mpaka sasa maendelo
yake ni mazuri.Tumejitahidi kurekebisha
mapigo ya moyoyaliyokuwa juu sana na kwa
sasa yako kawaida.Taratibu anaanza kurejewa
na fahamu zake ingawa bado anahitaji
kupumzika zaidi kwani bado fahamu hizarejea
vizuri.Maendeleo yake ni mazuri na baada ya
muda mfupi ujao basi atarejea na fahamu
zake zote.?
Alois alishusha pumzi nzito kwa kusikia
taarifa ile ya dokta.akatoa leso na kujifuta
jasho lililokuwa likimtirirka kwa kasi muda
huo.
?Thanks God?Alisema Alois huku ameinua
mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu
?kwa hivi sasa bado ataendelea kuwapo katika
uangalizi maalum mpaka hapo hali yake
itakapokuwa nzuri kabisa.Tatizo lililompata ni
mstuko wa moyo.Ni tatizo la kawaida
kutokea.Ila hali yake itakapokuwa nzuri
tutamshauri aonane na daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo ili aweze kumfanyia
uchunguzi zaidi katika moyo wake ?
Baada ya kupata maelezo ya kutosha toka
kwa dokta,Aloicy na andrew waliridhika kabisa
na dokta akawa shauri waende kupumzika
mpaka kesho .aloicy alikubaliana na wazo hilo
lakini akashauri andrew awarudishe Vero na
Vick nyumbani wakapumzike.Yeye atabaki
pale kuangalia hali ya Patrick inavyokwenda.
Wakati wakiendelea kujadili mama yake Vero
akatokea.Akawasalimu wote aliowakuta hapo
kisha kwa wasiwasi akataka kujua juu ya hali
ya Patrick.alipewa maelezo na mafupi ya hali
ya mgonjwa halafu akaomba aonane na dokta
Heneriko,akaongea naye na kupewa kwa
muhtasari juu ya hali ya Patrick na maendeleo
yake na akahakikishiwa uangalizi wa hali ya
juu.
?Ok jamani sasa utaratibu gani unaoendelea
hapa?
Aliuliza Bi stella Rugi mama yake na Vero.
?Tumepanga kuwa Andrew awarudishe
nyumbani Vero na vick wakapumzike ,mimi
nitaendelea kubaki hapa hapa na kufuatilia
hali ya mgonjwa?Alisema aloicy
?Vizuri ,basi msipate shida ,Vero na Vick
nitaondoka nao mimi,halafu Andrew nenda
kule kwa Patrick ukahakikishe usalama .Aloicy
utaendelea kubaki hapa kumwangalia
mgonjwa .Nitakuwa nakupigia simu mara kwa
mara ili kujua maendeleao ya mgonjwa sawa
baba eenh?Alisema mama yake Vero
?sawa mama tumekuelewa .?Andrew na aloicy
waliitika kisha wote wakatawanyika na
kumwacha Aloicy hapo hospitali
Saa saba usiku Patrick akarejewa na fahamu
zake kamili.Kitu cha kwanza kuhisi ni harufu
kali ya dawa.akageuza shingo kutazama
pande zote akatambua kuwa pale alikuwa
hospitali.Taratibu akavuta kumbukumbu za
nyuma na mara akakumbuka kitu
kilichopelekea yeye kuwepo pale.
?I saw her.Real I saw her.she?s alive?Alijikuta
akitamka maneno haya huku jasho
likikimtiririka na mapigo yake ya moyo
kwenda kasi .
* * *
Muuguzi aliyekuwa akimuangalia Patrick
aliingia ndani na kumkuta tayari Patrick
amerejewa na fahamu na amekaa
kitandani.Haraka akaenda kumwita daktari.Dk
heneriko alikuja kwa kasi na kumpima
akagundua kuwa bado mapigo ya moyo wa
Patrick yalikuwa juu sana.
?Lazima kuna kitu kinamsumbua huyu si
bure?Aliwaza dokta Heneriko.
?Patrick ?Dokta akamwita baada ya kumaliza
kumfanyia vipimo.
?naam dokta?Aliitika Patrick kwa sauti yenye
kukwaruza.
?Pole sana ?
?Ahsante sana dokta?
?Patrick kijana wangu usijali utapona tu hali
yako inaendelea vizuri .Unahitaji kupumzika
sasa mpaka hapo asubuhi tutakapochukua
tena vipimo vingine?
?Sawa dokta.?
?Ok pumzika Patrick na iwapo utahitaji kitu
chochote nesi yuko hapo nje na atakuwa akija
hapa mara kwa mara kukuangalia.Tena
nimekumbuka kaka yako yuko nje muda sijui
kama ungependa kumwona??Akasema dokta
heneriko.
?Yes dokta naomba uniitie..?
Dokta Heneriko akafungua mlango na kutoka.
Aloicy muda huo alikuwa amesinzia katika
sofa lililoko mapokeziMara akastuliwa na
sauti ya Dokta Heneriko.
?Aloicy ,Patrick amekwisha rejewa na fahamu
zake kamili kwa hiyo unaweza kwenda
kumwona.Ila tafadhali usijaribu kumuuliza
chochote kuhusiana na kilichopelekea yeye
kupoteza fahamu.Ongea naye maongezi
mengine ya kawaida.sawa??
?sawa dokta?Alijibu Patrick huku akifikicha
macho yaliyojaa usingizi.Nesi aliyekuwepo
mapokezi akampeleka hadi katika chumba
laimokuwa amelazwa Patrick.
?Vipi brother unajisikiaje kwa sasa?Alisema
Aloicy
?Sasa hivi sijambo brother najisikia
vizuri.nashukuru kwa kuja kuniona?
?Usijali Patrick kwa sasa endelea
kupumzika.bado unahitaji mapumziko ya
kutosha.Mimi niko hapo mapokezi tutaonana
asubuhi?
?Ok brother?
* * *
Baada ya kulia sana hatimaye kiusingizi
kikaanza kumchukua na taratibu akajikuta
akianza kulala.Hazikupita hata dakika kumi
toka aanze kusinzia simu yak ikaanza kuita
na kumstua toka usingizini.Alipoiangalia simu
yake ilikuwa imeandika jina Aloicy.Aliogopa
kuipokea simu ile akabaki akiiangalia
ikiiendelea kuita.Mikono ilikuwa ikimtetemeka
.Alihofia pengine simu ile inaweza kuwa
imebeba ujumbe mbaya kuhusu Patrick.Simu
iliita ikakatika ,ikaanza kuita tena.Akaamua
kuipokea.
?Haloo?Aliita Vero
?Haloo shemeji vipi?Ilkuwa ni sauti ya upande
wa pili wa simu ambayo Vero aliitambua
moja kwa moja kuwa ilikuwa ya Aloicy.
?safi shemeji vipi kwema huko?Alisema vero
huku mapigo yake ya moyo yakienda kwakasi
isiyo ya kawaida.
?Huku kwema tu shemeji.Nataka
nikufahamishe tu kuwa Patrick tayari
amekwisha rejewa na fahamu zake na
nimetoka kuongea naye muda si mrefu.Kwa
hivi sasa anaendela kupumzika.kwa hiyo
shemeji yangu unaweza ukalala kwa amani
sasa.?
Vero akashusha pumzi ndefu akakaa kimya
kwa sekunde kadhaa kisha akamuaga Aloicy
na kukata simu.Alipokata simu akaanza tena
kulia kwa kwikwi..Vick ambaye alikuwa katia
usingizi mzito akaamka baada ya kustushwa
na kilio cha Vero.
?Vero nini tena?
?Patrick anaendelea vizuri.aloicy amenipigia
simu sasa hivi na kunifahamisha.?
?sasa kama hajambo unalia nini?
?Huwezi jua Vick ni jinsi gani nisivyopenda
kumuona Patrick akiumwa kwa jinsi
ninavyompenda..Ninalia kwa mateso
ninayoyapata juu yake.?
Vick alimbembeleza vero hadi akanyamaza
kisha akajilaza kitandani na kuanza
kutafakari.juu ya tukio zima..Alikumbuka
qwalikuwa sebuleni wakiangalia luninga
ambapo warembo wanaotarajia kuwania taji
al miss Tanzania walikuwa wakijinadi .alivuta
picha na kumuona Patrick akiwa katka friji
akijimiminia maji katika glasi ambapo muda
huo Miss arusha neema japheti aliikuwa
akijinadi.Alikumbuka kumuona Patrick
alivyovutiwa ghafla na kipindi hicho cha
warembo.Toka Neema hakumbuki ni mrembo
gani aliyefuatia kujinadi ila anachokumbuka
ni kwamba Patrick alipiga ukelele mkubwa wa
kama anashangaa kitu halafu akaanguka.
?Ni dhahiri ni mstuko ndio uliomfanya Patrick
aanguke na kupoteza fahamu .Lakini je ni kitu
gani hasa ambacho kilimstua Patrick kiasi
cha kupoteza fahamu?Je mstuko huu una
uhusiano wowote na kipindi kile tulichokuwa
tukiona?Lakini hapana Patrick nimekuwa naye
muda kwa mua mrefu sasa na tabia yake
ninaifahamu vizuri.Kuhusu wanawake siwezi
kumsemea vibaya hana tabia hiyo ya kuwa na
wanawake wengine nje ya mahusiano
yetu.Nina uhakika na hilo.Sasa ni kitu gani
alistuka ?any way siwezi kupata jibu kwa sasa
mpaka hapo atakaponiambia yeye mwenyewe
kwani nina hakika hawezi kunificha kitu
chochote.?
Alikuwa akiwaza Vero na taratibu usingizi
ukamchukua akalala.
************************************************
Saa kumi na mbili asubuhi iliwakuta Vero
,Vick na mama yake vero hospitali.Hali ya
Patrick ilikuwa ikiendelea vizuri .alfajiri hiyo
tayari alikwisha hamishwa toka katika
chumba cha uangalizi maalum na kuwekwa
katika chumba cha mapumziko ya kawaida.
Wakiongozwa na aloicy ambaye alilala hapo
hospitali walielekea moja kwa moja chumbani
na kumkuta Patrick tayari amekwishaamka.B
ila kupoteza muda Vero akamkumbatia na
kumpiga mabusu mfululizo.
?Pole sana my dear.Unajisiaje kwa sasa?
?Najisikia vizuri sana?
alijibu Patrick huku akijinyoosha nyoosha pale
kitandani.baada ya kusalimiana kilifuata
kipindi cha vicheko na utani wa hapa na pale
kisha Vick na mama yake Vero wkaomba
waondoke kwa ajili ya kwenda kujiandaa na
mishughuliko ya siku.
Vero alimwinua Patrick na kumpeleka bafuni
ambako alimwogesha na kumrudisha tena
chumbani ,akamwandalia kifungua kinywa
.Patrick alijisikia faraja kubwa kwa jisni binti
huyu alivyokuwa
akimuhudumia.
************************************************
?Andrew kwa kipindi kirefu sasa umekuwa ni
msiri wangu mkubwa.Mambo yangu mengi
ambayo sihitaji mtu mwingine kufahamu wewe
wayajua.Urafiki wetu ni zaidi ya
undugu.Naomba sana kile nitakachokuambia
hapa usimwambie mtu yeyote yule.Itabaki
kuwa siri yako mpaka pale muda muafaka
utakapofika.?
Patrick aliongea taratibu huku akijiweka vizuri
sofani.Ni siku ya kwanza tangu ameruhusiwa
kutoka hospitali kwa sababu ya mstuko
uliopelekea apoteze fahamu.Andrew rafiki
mkubwa wa Patrick alikuwa kimya akiwa na
shauku kubwa ya kutaka kulisikia lile ambalo
rafiki yake alikuwa tayari kumwambia.
?I saw Happy ?alisema Patrick kisha akatulia
na kuyaacha maneno yale yamwingie Andrew.
?what? aliuliza Andrew kwa mshangao
?I saw Happy ?
Patrick alirudia tena kisha akainamisha
kichwa chini na kuzama katika mawazo
mazito.andrew aliinuka na kuanza kuzunguka
zunguka mle chumbani huku akionekana
dhahiri alikuwa meshtushwa mno na kauli ile
ya Patrick.
 
ENDELEA................
?Umemuona wapi??andrew akauliza huku
amejishika kichwa.
?Nimemuona kwenye Luninga .Kulikuwa na
kipindi cha kuwanadi warembo wanaoshiriki
kinyang?anyiro cha kumsaka mrembo wa Taifa
.Happy ni miss Ilala.?
?are you sure? Andrew akahoji
?yes I?m sure na ndio kitu kilichonifanya
nikapata mstuko na kupoteza fahamu?
Andrew alivuta pumzi ndefu ,akainuka
akaanza kuzunguka zunguka humo ndani
kisha akakaa.Vijana hawa wote kwa sasa
walikuwa katika wakati mgumu sana.Ni
Andrew pekee aliyefahamu kilichokuwa
kikiendelea kati ya Patrick na Happy na ndio
maana alichanganyikiwa asijue afanye
nini.Alimuonea huruma sana Patrick kwa
wakati huu mgumu alionao.
?Vero aligundua chochote ?Andrew akauliza
tena
?sidhani kama aligundua kitu chochote.sidhan
i kama alihisi chochote kwa wakati ule?
?Ok kwa hiyo tufanye nini sasa? Andrew
alihoji.
Patrick akainuka na kwenda katika friji
akjimiminia maji baridi kwenye glasi akapiga
fuda kubwa kisha akavuta pumzi ndefu na
kusema.
?Nataka kuonana na Happy ?
Kimya cha sekunde kadhaa kikapita hapo
sebuleni kisha Patrick akaendelea
?Nataka kabla ya kuonana naye kwanza
tumfanyie uchunguzi anaishi wapi, anafanya
kazi gani,ana mchumba au hana,na chochote
kile tunachoweza kukifahamu kuhusu
yeye.Uchunguzi huu nataka uwe wa siri na
yeye Happy asiweze kufahamu kuwa
anachunguzwa.Ikiwezekana tunaweza hata
kuajiri mtu wa kuifanya kazi hii niko tayari
kumlipa kiasi chochote cha pesa
anachohitaji.Nakukabidhi kazi hii Andrew nina
imani itafanyika ipasavyo.Tuko pamoja?
?Nimekuelewa Patrick lakini suala hili haliwezi
kuathiri maandalizi ya harusi yako ambayo
tayari yamekwishaanza??
?Hahahahaa usihofu kuhusu hilo my friend.I
know what I?m doing ,ok??
?Una maana gani Patrick unaposema unajua
unachokifanya ?Ninafahamu kuwa ndoto zako
za siku nyingi ni kuwa na Happy katika
maisha yako na kwa sasa umekwisha kuwa na
uhakika kuwa yupo na kwa wakati wowote
unaweza kumuona .Nina wasiwasi sana na
huu ujio wa Happy katikati ya maandalizi ya
Harusi yako unaweza kutibua kila kitu.
?Kwa ajili ya Happy niko tayari kwa lolote
linaloweza kutokea.I must fight for her.all
these years I?ve been hurting myself thinking
about her na mpaka sasa nimeshindwa kabisa
kuifuta kumbukumbu ya Happy moyoni
mwangu.Siwezi kuendelea kuutesa moyo
wangu Andrew.I have to face her.? Akasema
Patrick
?Patrick nafikiri unahitaji kufikiri zaidi kuhusu
suala hili, si suala jepesi kama unavyolifikiri.
Ni suala ambalo linagusa hisia za watu wengi
.Hi?..?
Andrew hakuendela Patrick akadakia.
?Andrew no body?s gonna change my
mind.That?s my decision and its
final.Nilivyoamua nimeamua.Nitapambana
kadiri ninavyoweza ili kumpata Happy .I love
her and I know that she loves me too.?
?Patrick miaka mingi imepita tangu
mpotezane na Happy na kwa sasa bado kama
mwezi mmoja na nusu hivi ufunge ndoa na
Vero ,ndoa ambayo sehemu kubwa ya
maandalizi yake yamekamilika.Huoni kuwa
utakuwa unamyima haki zake Vero kama
ukihamishia mawazao yako yote kwa Happy .?
Nina imani Vero anakupenda kwa dhati ya
moyo wake na nina imani vile vile hata wewe
unampenda Vero sasa kwa nini utake kumtesa
hivi mtoto wa watu?
?Andrew unayasema haya yote kwa sababu
huwezi kuingia katika viatu vyangu na kuona
nini kilichomo ndani.Nina imani kubwa hata
wewe ungekuwa mahala pangu kwa sasa basi
ungeweza kufanya kama mimi
ninavyofanya.Please Andrew naomba msaada
wako katika hili.Ni lazima nionane na Happy
hivi karibuni.?
?Nimekuelewa Patrick lakini bado moyo wangu
una wasiwasi sana juu ya kinachoweza
kutokea.hapo mbeleni.nafahamu kuwa endapo
utaingia matatizoni basi ni sote tutakuwa
tuko katika matatizo.Tatizo langu ni lako na
lako langu ndio maana tunahitaji sana
kushauriana kwa kina kabla ya kufanya
jambo.?
?Andrew najua una wasiwasi mwingi kuhusu
mimi na Vero.Hilo ni kubwa linalokuumiza
kichwa.Hata mimi sijisikii vizuri kumtesa Vero
binti aliyeyatoa maisha yake kwangu.Binti
anayenipenda kwa dhati ya moyo wake.Ni vero
huyu huyu ndiye aliyeirudisha tena furaha
ndani ya moyo wangu na kuliondoa wingu zito
la ukiwa lililokuwa limenifunika.Nampenda
Vero lakini sina jinsi ni lazima nionane na
Happy .?
Andrew aliinuka kitini akaiendea friji na
kujimiminia mvinyo baridi akanywa mafunda
kadhaa kisha akamgeukia Patrick.
?Ok Patrick kwa sababu umekwishaamua basi
hatuna budi kufanya hivyo.Mimi nitaianza
kazi hiyo kesho.Nitamtafuta mtu ambaye
ataifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa.Usijali
kuhusu hili rafiki yangu?
Patrick alifurahi akainuka na kumkumbatia
rafiki yake
.
*********************************
Saa kumi na mbili za jioni Veronika alirejea
katika shughuli zake na kumuaga mama yake
kuwa alikuwa akaienda kumwangalia Patrick
anaendelaje.Ni siku ya tatu sasa toka Patrick
atoke hospitali.Hali yake haikuwa ikiendelea
vizuri sana.Muda mwingi alikuwa akionekana
ni mtu mwenye mawazo mengi sana.Hali hii
ilimpa wasiwasi mwingi Vero kiasi cha
kumfanya awe karibu naye kila wakai ili
kujaribu kumchangamsha na kumrudisha
katika hali yake ya kawaida.
Ingawa Patrick alijitahidi kwa kila jinsi ili Vero
asione hali hii ya unyonge lakini mara nyingi
alishindwa na kujikuta akitoa machozi.Vero
aliigundua hali hii na kwa kiasi kikubwa
ikamuongezea udadisi juu ya kinachoendelea
.alijua ni lazima liko jambo ambalo
linamchanganya Patrick .
?Haloo sweetie?Alisema Vero baada ya kuingia
ndani kwa Patrick
?Haloo vero, you are back?akasema Patrick
Vero akamfuata Patrick kitandani
akamkumbatia na kumpiga busu zito.
?Unaendeleaje mpenzi?
?Naendelea vizuriMungu ananisaidia
sana.Muda si mrefu nitapona kabisa?
Baada ya kujuliana hali Vero alimwandalia
Patrick Juice kisha yeye akaelekea jikoni
kufanya maandalizi ya chakula cha
jioni.Patrick alipata faraja kubwa baada ya
Vero kuwasili Ni wazi Patrick husikia furaha
kubwa moyoni awapo na Vero.
Ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa
bado alimpenda sana Vero lakini kwa ghafla
Happy ametokea na kuanza taratibu
kuzihamisha hisia zake.
Chakula kiilpokuwa tayari kikawekwa
mezani,wakala kisha wakapumzika na baadae
wakaelekea kulala.
?Vero dear tayari umekwisha kata tiketi za
kuingia Miss Tanzania Jumamosi?Patrick
akauliza
?Tayari mpenzi Nimekwishaziandaa .Je
utaweza kweli kwenda na hali hii?Naona
kama hali yako inazidi kudhoofika siku hadi
siku?
?Usijali mpenzi wangu lazima nihudhurie hata
iweje.Nina imani ndani ya siku mbili tatu
zijazo hali yangu itakuwa shwari?
Vero akanyamaza kimya akajaribu kuvuta
kumbukumbu nyuma siku ile Patrick
alipoanguka na kupoteza fahamu alikuwa
akitazama kipindi cha wagombea wa miss
Tanzania .Hakutaka kukubaliana kuwa kuna
kitu chochote kinachoendelea baina ya Patrick
na mashindano yale.Alijitahidi kuilazimisha
akili yake ikubaliane na taarifa ya daktari
kuwa Patrick alipoteza fahamu kwa sababu ya
uchovu mwingi uliokuwa ukimkabili kiasi cha
kuufanya ubongo wake ushindwe kufanya
vizuri kazi yake.
?Lakini pamoja na taarifa ile ya daktari lakini
kuna kitu kiko moyoni mwa Patrick ambacho
kinamyima raha na na kuisumbua akili yake
namna hii.Ni kwa sababu hiyo tu ndiyo maana
amepoteza furaha yote aliyokuwa nayo
kabla.Chakula chenyewe mpaka
abembelezwe.mara kadhaa nimemfuma
mwenyewe kwa macho yangu akilia.Ingawa
anajitahidi sana kuificha hali hii lakini
nimekwishafahamu .Anyway nitajitahidi
kumuuliza ili anieleze kama kuna jambo lolote
linalomsibu.?
Veronika alizama ghafla katika mawazo.
?Unawaza nini mpenzi wangu?Patrick akauliza
?Nothing.Siwazi chochote zaidi yako.Unajua
Patrick hali yako kwa sasa inanipa wasiwasi
sana.Tangu umetoka hospitali umebadilika.Ni
kitu gani kinakusumbua mpenzi hebu
niambie.Hali hii inanifanya hata mimi nihisi
kama vile ninaumwa pia.Au kama kuna kitu
nimekukosea niambie Patrick ili nijirekebishe.T
angu tumeanza mapenzi yetu sijawahi hata
siku moja kukuona katika hali hii?
Vero akashindwa kujizuia akaanza kulia kwa
kwikwi.
Patrick akamvutia Vero kwae akambusu na
kumwambia
?Usihofu kitu baby hakuna kitu kingine
kinachonisumbua .Kama daktari alivyosema
kuwa natakiwa kupumzika sana .Uchovu ndio
uliopelekea tatizo lile kutokea.?
Alisema Patrick huku akizichezea nywele laini
za Vero.
?Hapana dear najua lazima kuna kitu
kinachokusumbua akili na hutaki kuniambia?
?Wow my dear angel ,wewe ndiye maisha
yangu.Wewe ndiye uliyeyashika maisha
yangu.Nimekukabidhi funguo za moyo
wangu.Wewe ndie mfariji wangu,wewe ndiye
furaha yangu,wewe ndiye kila kitu kwangu
sasa kwa nini nikufiche kitu?Hakuna kitu
nimewahi kukuficha wewe mpenzi wangu na
haitakuja tokea nikawa na tatizo nikashindwa
kukwambia.Sasa nisipokwambia wewe
nitamwambia nani tena??
Patrick alijitahidi kumtoa Vero wasiwasi
aliokuwa ameanza kuwa nao juu yake na mara
moja akaazimia moyoni kubadilika kitabia ili
Vero asije akaendelea kumdadisi.Taratibu
akaanza kurudi katika hali yake ya kawida ya
ucheshi na uchangamfu mkubwa kitu
ambacho Vero alikifurahia sana.
********************************
Ni jumamosi angavu ndani ya jiji la Dar es
salaam,jiji lililojaa kila aina ya pilika na
purukushani.Jua lilikuwa likielekea magharibi
na kulipisha giza lichukue nafasi yake.Jioni
hii iliwakuta Patrick na Veronika wakiwa
katika pilika pilika za kujiandaa kuelekea
katika kinyang?anyiro cha kumsaka mrembo
wa taifa katika ukumbi wa Diamong jubilee.
Patrick ndiye aliyekuwa katika pilika pilika
nyingi zaidi jioni hiyo.Siku hii ilikuwa ni moja
kati ya siku zake kubwa kabisa katika maisha
yake.Ni siku ambayo aliamini ingemkutanisha
tena na kiumbe ampendaye kwa dhati ya
moyo wake.Alikuwa ndani ya suti nzuri ya
gharama kubwa.Suti hii huwa anaivaa kwa
nyakati maalum kama hizi.Hakika alikuwa
amependeza vilivyo kijana huyu.Wakiwa
katika harakati z a kumalizia kujiandaa simu
yake ikaita.Alkuwa ni Andrew.
?Haloo Andrew?
?Hallo Patrick vipi mko tayari?aliuliza Andrew
huku akicheka kichinichini.
?Tupo tayari Andrew na muda wowote toka
sasa tunaweza kuanza safari ya kuelekea
ukumbini?
?Ok Patrick sisi tayari tumekwishajiandaa na
muda wowote tutakuwa njiani kuelekea huko
na tutawasubiri nje ya ukumbi ili tuingie
pamoja.Ila ndugu yangu nakuomba kitu
kimoja katu usihamaki.Wala usionyeshe aina
yoyote ya mstuko pindi utakapomuona Happy
.Najua tu lazima kunaweza kutokea na kitu
kama mstuko flani hivi ila tafadhali naomba
ujaribu kujizuia kwa sababu pale tutakuwa
tuko na Vero na Vick kwa hiyo wanatakiwa
wasihisi kitu chochote.Mimi nitakuwa macho
kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote
kitakachoharibika ?
?Usihofu Andrew nalifahamui hilo na niko
makini nalo sana.naelewa leo ni siku ya
kipekee maishani mwangu.Ni siku ya
kihistoria katika maisha yangu hivyo siwezi
kuiharibu.?
Baada ya kumaliza kujiandaa na kuhakikisha
kuwa wako safi wakaingia garini na kueleka
Diamond Jubilee.
********************************
Ukumbiwa Diamond jubilee ulikuwa umefurika
watu pasi mfano.Pamoja na ukumbi kufurika
watu bado watu walikuwa wakimiminika
ukumbini hap kwa lengo la kushuhudia
mchuano wa kumtafuta mrembo wa Taifa
atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya
dunia.
Patrick,Vero,Andrew na Vick waliwahi sana
kuingia ukumbini na kuchukua moja kati ya
meza za mbele kabisa.Patrick moyo ulikuwa
ukimdunda sana usiku huo,.Andrew
alilifahamu hilo na hivyo akawa makini sana
katika kuakikisha kuwa hakuna kitu
kitakachoharibika .Toka wameingia ukumbini
Patrick alikuwa kimya .
?Patrick are you ok?Vero liuliza baada ya
kuona Patrick yuko kimya sana.
?Yes I?m ok Vero usihofu.?
Mara muongoza shughuli akatokea jukwaani
na kuanza kutangaza.
?Mabibi na mabwana mliohudhuria
mashindano haya makubwa ya urembo nchini
napenda kuwakaribisha sana katika usiku huu
wa pekee kabisa kwetu sote.Ni usiku wa pekee
kwa sababu leo tutaandika historia mpya
kabisa katika mashindano ya urembo hapa
nchini na ulimwengu kwa ujumla.Kwa mwaka
huu kamati nzima ya Miss Tanzania
imeazimia kufanya mabadiliko makubwa sana
na nyie wote mlioko hapa ndio mtakaokuwa
mashahidi wa kile kitakachotokea usiku wa
leo.Nasema karibuni sana katika usiku huu na
tujumuike sote mimi naitwa Mc Thora kwa
wale ambao hawanifahamu..
?Mabibi na mabwana kabla hatujaendelea
mbele na ratiba yetu ningependa kwanza
kumkaribisha jukwaani mkurugenzi mkuu wa
Masimulizi entertainments ambao ndio
wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa
mwaka huu Mabibi na mabwana makofi kwa
Mr Petit.s Woris?
Petit woris mkurugenzi wa Masimulizi
entertainments akapanda jukwaani akiwa
amevalia nadhifu sana.
?viongozi mbali mbali mliohudhuria
mashindano haya usiku huu, ndugu
watazamaji mabibi na mabwana asalaam
aleikhum.Ni furaha ilioje kwetu sisi kama
Masimulizi entertainments kudhamini
mashindano makubwa kama haya ya urembo
hapa nchini.Kama wote mnavyoshuhudia
mashindano ya mwaka huu yamekuwa na
utofauti mkubwa mkilinganisha na mengine
yaliyopita hukonyuma..Kwa mwaka huu
nathubutu kusema maandalizi yake yamekuwa
mazuri ,zawadi zimeboreshwa na ushindani
miongoni mwa washiriki umeongezeka mara
dufu.Kwa kuwa ni mara yetu ya kwanza
kudhamini mashindano makubwa kama haya
bado kunaweza kuwa na kasoro kadhaa
ambazo nina imani kwa kushirikiana na
wadau wote wa urembo hapa nchini
tutasaidiana kuzitatua.Nina imani bado
tutaendelea kudhamini na kuandaa
matamasha mengi na makubwa zaidi hapa
nchini ili kuzidi kuukuza wigo wa burudani
hususani sanaa hii ya urembo.Mwisho kwa
niaba ya uongozi na wafanya kazi wote wa
Masimulizi entertainments napenda kuwatakia
wote utazamaji mzuri wa mashindano haya
usiku huu.Ahsanteni sana.?
Baada ya kumaliza akarudisha kipaza sauti
kwa muongoza shughuli kisha akashuka
jukwaani.
?mabibi na mabwana huyo alikuwa ni
mkurugenzi wa Masimulizi entertainment
ambao ndio wadhamini wakuu wa
mashindano haya kwa mwaka huu..Mabibi na
mabwana kwa mujibu wa ratiba yetu
kinachofuta kwa sasa ni kuwatambulisha
majaji ambao ndio watakaofanya kazi kubwa
na ngumu ya kutuchagulia mrembo mwenye
sifa ya kuwa mrembo wa taifa kwa usiku
huu.Majaji tulionao usiku huu ni
saba.Ningeomba jaji utakaposiia jina lako
likitajwa usimame ili watu wakufahamu.Wa
kwanza ni Mr Ernest Namesha,wa pili ni
ndugu Mecky ,tunaye pia Mr Boniventure
Gregory,anayefuatia ni Mr Samweli
Nathaniel,tunaye pia dada yetu mpendwa
usiku huu naye ni dada Esther msethi,pia
tunaye Mrs Coletha brown,tunaye vile vile bi
Susan Abrahams na wa mwisho ni ndugu
Jacob Lyimo.Hawa ndio majaji wetu ambao
watakuwa wakifanya kazi ngumu ya
kumchagua mrembo wa Taifa usiku huu wa
leo.?
?mabibi na mabwana baada ya kuwafahamu
majaji wa mchuano huu wa leo sasa naomba
niwalete kwenu warembo wote 26 katika show
maalum waliyoiandaa ?
wimbo ukaanza kupigwa na warembo
wakaanza kutoka huku wakicheza kwa staili
yenye kuvutia sana.makofi nderemo na vifijo
vikatawala ukumbini.Patrick alielekeza macho
na akili yake yote jukwaani na bila kukosea
alimuona Happy ambaye alikuwa amependeza
kupindukia Jasho likaanza kumtiririka akatoa
kitambaa na kujifuta.Alikuwa kimya kabisa.
Baada ya show ya warembo kumalizika
ziliendelea burudani mbili tatu toka kwa
wasanii mbali mbali kisha muongoza shughuli
akapanda tena jukwaani.
?Mabibi na mabwana baada ya kupata
burudani hizo za kukata na shoka sasa
naomba niwalete kwenu warembo wote 26 ili
muwatambue.Watapita hapa jukwaani mmoja
mmoja .?
Warembo wakaanza kutoka nyuma ya jukwaa
na kuanza kupita mbele ya watazamaji.Kido
go Patrick atamke kitu baada ya kusikia jina
la Happy likitajwa .Happy akapita jukwaani
huku kelele za shangwe zikisikika.Happy
alikuwa akionekana kama malaika usiku
huu.alikuwa amependeza vilivyo.Kila mtu
aliustaajabia uzuri wa binti huyu mwenye kila
sifa ya kuwa mrembo wa Taifa na dunia.Kelele
zile za mashabiki zilizidi kumchanganya
Patrick na kumfanya ahisi kuchanganyikiwa
.Andrew alikuwa makini sana kwa lolote
ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa
amani kati yao.
Baada ya kupita jukwaani kujitambulisha kwa
mashabiki zikafuata burudani za aina yake
toka kwa wanamuziki.Kisha Muongoza
shughuli akarejea tena jukwaani.
?mabibi na mabwana mambo yanazidi
kupamba moto.Mambo ni bam bam na kama
nilivyowaeleza toka mwanzo kuwa Masimulizi
entertainment wameleta mageuzi makubwa
katika mashidano ya mwaka huu .Kwa sasa
napenda kuwaleta kwenu warembo wote 26
wakiwa katika vazi la ufukweni.Mhh hapa
pana kazi kweli kweli .mabibi na mabwana
hebu tuwashangilie hawa warembo wetu
watakapokuwa wakipita jukwaani katika vazi
la ufukweni.?
Warembo wakaanza kupita jukwaani wakiwa
katika vazi la ufukweni.Siyo siri walikuwa
wamependeza vilivyo.Baada ya kumaliza
kupita na vazi la ufukweni zikafuata tena
burudani halafu warembo wote wakapita tena
kwa mara nyingine na vazi la ubunifu.Kelele
zilikuwa kubwa sana kila walipopita warembo
Neema wa Arusha na Happy wa
Ilala.Warembo hawa walionekana kuchuana
vilivyo.Kisha pita na vazi la ubunifu
muongoza shughuli akapanda jukwaani.
?mabibi na mabwana tayari tumewashudia
warembo wetu 26 wakipita hapa mbele yetu
wakiwa katika mavazi tofauti tofauti.Kwa
sasa ule wakati mliokuwa mkiusubiri kwa
hamu kubwa unaelekea kuwadia.Kwa hivi
sasa tutakwenda kuwafahamu warembo 10
bora ambao wameonekana kufanya vizuri
zaidi .Naomba sasa nimkaribishe Mrs Coletha
brown ili aje atutangazie wale warembo wetu
kumi waliofanya vizuri zaidi.Karibu sana
mama.?
Mrs Coletha brown akapanda jukwaani akiwa
na karatasi yenye majina ya warembo kumi
waliofanya vizuri na ambao wataendelea na
mchuano.
?mabibi na mabwana napenda kuchukua
nafasi hii kwanza kuwapongea waandaaji wa
mashindano haya ambayo kwa mwaka huu
yameboreshwa kwa kiwango cha juu kabisa.
Mabibi na mabwana kazi yetu usiku wa leo
imekuwa ni ngumu sana .Warembo wote wako
katika hali ya ushindani wa hali ya juu
mno.Lakini tumeweza kuwapata wale kumi
ambao ni bora zaidi na ambao nitawataja hivi
punde.Nambari 12 Nelea shulo,nambari
9Saida abdi,nambari 4 Upendo
timelo,Nambari 20 Neema i,Nambari 11 Esther
stevens,Nambari 6 Happy ,nambari 22
Elimeena kimuo,nambari 26 bahati
udhoka,nambari 16 Winifrida mwasajuki,na
mwisho ni namba 13 genevieve alphonse.?
Kelele za kushangilia zikasikika
ukumbini.Warembo waliofika hatua ya kumi
bora wakajipanga mstari.wakapiga picha ya
pamoja kisha zikafuata burudani .baada ya
burudani mc akapanda tena jukwaani.
?Mabibi na mabwana bado tunaendelea na
mchakato wetu wa kuifikia ili hatua kubwa
kabisa ambayo kila mmoja wetu aliyeko hapa
ana hamu ya kuishuhudia.Kila mmoja
anatamani amfahamu mrembo wetu mpya wa
Taifa.Kwa sasa tutaenda kuwatafuta wale
watano bora ambao kutoka kwao tutampata
mrembo wetu.Atapanda tena Mrs Coletha kuja
kututangazia warembo watano bora .?
mrs Coletha akapanda tena jukwaani akiwa
ameongozana na watu wawili wa miraba
minne wanaomlinda.
 
ENDELEA................
?mabibi na mabwana kama nilivyowaambia
kuwa kazi yetu leo imekuwa ngumu sana hasa
kutokana na jinsi warembo wote walivyo na
vigezo vya juu mno kiushindani.Lakini pamoja
na wote kuwa na ushindani wa juu tumeweza
kufanikiwa kuwachuja na kupata wale watano
ambao wameonekana kuwa ni bora zaidi.
Warembo waliopita hatua ya tano bora ni
mrembo nambari 16 Winifrida
mwasajuki,nambari 20 Neema i,nambari 13
Genevieve alphonse,nambari 26 Bahati udhoka
na mwisho ni nambari 6 Happy .?
Kelele kubwa zikasikika zikishangilia.Kila mtu
pale ukumbini alikuwa ameridhika na kazi
waliyoifanya majaji.Hakukuwa na aina yoyote
ya upendeleo.Baada ya kuwatambua warembo
wote waliofanikiwa kuingia hatua ya tano
bora hatimaye kikafuata kipindi cha
maswali.Ni Happy kibaho tena ndiye aliyejibu
swali vizuri zaidi na kuwafanya watu wote
ukumbini kumshangilia kwa nguvu.Kila mtu
alikuwa akiamini kuwa Happy ni lazima
angeibuka kuwa mrembo wa Taifa.Patrick
jasho lilikuwa likimtiririka mwilini.alijitahidi
kwa kila alivyoweza ili asiweze kuonyesha hali
yoyote ya utofauti pale mezani.Baada ya
kipindi cha maswali kumalizika ikafuata
burudani moja kisha muongoza shughuli
akapanda jukwaani.
?mabibi na mabwana ule wakati uliokuwa
ukisubiriwa na kila mtu hapa ukumbini naona
sasa umewadia.huu ni wakati wa kumtambua
mrembo wetu mpya wa Taifa.Napenda
nichukue fursa hii kuwashukuru sana majaji
kwa kazi ngumu waliyoifanya usiku huu kwa
kutuchagulia mrembo mpya wa Taifa.Kabla
sijamkaribisha jaji mkuu kuja kutangaza
mshindi wa shindano hili napenda
kumkaribisha mrembo anayemaliza muda
wake ili aweze kuongea machache na
kuwaaga rasmi kabla hajalivua taji la Miss
Tanzania.?
Helen Daudi mrembo anayemaliza muda wake
alipanda jukwaani huku akishangiliwa
vilivyo.Alipewa kipaza sauti na kusogea
mbele.
?mabibi na mabwana ,wageni
waalikwa,waheshimiwa majaji ,waandaaji na
wadhamini wote wa mashindano haya habari
za usiku.Napenda kwanza kabisa kumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha mimi
kutimiza moja ya ndoto zangu nayo ni kuwa
mrembo wa Tanzania.Nawashukuru vile vile
wazazi wangu na ndugu zangu kwa kunipa
moyo toka katika hatua za awali za
kinyang?anyiro hiki hadi nilipobahatika
kuchukua taji.Mabibi na mabwana kulivaa taji
la Miss Tanzania ni mzigo mkubwa.Nimeshuh
udia mimi mwenyewe uzito wa taji hili kubwa
la urembo hapa nchini.Yapo mengi ambayo
unapaswa kulifanyia taifa hili ukiwa kama
mrembo wa Taifa.Kuna mazuri na magumu
yake.Zipo changamoto nyingi ambazo
yakubidi upambane kufa na kupona ili uweze
kushinda.Napenda kuishukuru kamati nzima
ya Miss Tanzaina kwa ushirikiano mkubwa
walionipa katika kipindi chote nilichokuwa
nimevaa taji hili.Sintaweza kumtaja mmoja
mmoja lakini napenda niwashukuru wote kwa
ujumla.Napenda niwashukuru vile vile wadau
wote wa sanaa hii ya urembo hapa nchini kwa
sapoti yao kubwa waliyonipa.Wamenisaidia
sana kuifahamu sanaa hii ya urembo
vizuri.Nawashukuru pia wananchi wote wa
Tanzania kwa kunikubali Nawapenda wote na
ninaahidi kushirikiana na mrembo atakayevaa
taji hili usiku huu katika yale yote mazuri
niliyokuwa nimeyafanya kwani kulivua taji hili
si mwisho wa kuendeleza yale yote
niliyokwisha yafanya wakati niko na
taji.Mwisho kama binadamu kuna wakati
naweza kuwa nimemkosea huyu na yule kwa
namna moja au nyingine.Napenda kuchukua
nafasi hi kwa dhati kabisa kuwaomba
msamaha wale wote niliowakosea.Tu
sameheane na kuanzia usiku huu tuanze
maisha mapya.Ahsanteni sana.?
Alimaliza kutoa machache mrembo huyu
akarudi katika kiti chake cha heshima huku
akishangiliwa na watu.?
?naam mabibi na mabwana huyo alikuwa ni
mrembo anayemaliza muda wake.Na sasa ule
wakati tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu kubwa
ndio umewadia.Ni hivi punde tutaenda
kumfahamu mrembo wetu mpya.Naomba sasa
nimwite Mr Jackob ili aweze kututajia
washindi wetu.?
Mr jacob akapanda jukwaani.
?Mabibi na mabwana kama alivyotangulia
kusema Mrs Coletha brown kuwa mchuano wa
leo ulikuwa mgumu sana.Tunamshukuru
Mungu kuwa tumeweza kumpata mrembo wa
taifa licha ya kuwa na wakati mgumu hasa
kutokana na kila mrembo alivyokuwa
amejiandaa.Mabibi na mabwana nitaanza
kuitangaza nafasi ya tatu hadi moja.?
Alitulia kidogo kisha akaendelea.
?Nafasi ya tatu imekwenda kwa mrembo
nambari 16 winifrida mwasajuki?
alitulia kwanza na kumpisha mrembo huyu
apite mbele huku akishangiliwa.
?nafasi ya pili imekwenda kwa mrembo
mwenye nambari 20 Neema Jaffa?
Kelele za shangwe zikasikika.Neema binti
mwenye ngozi nyeusi yenye kung?aa akapita
jukwaani akiwa ndani ya tabasamu kubwa.
?Na sasa mabibi na mabwana ni nafasi
yakwanza.Nafasi ya kwanza imekwenda kwa
mrembo mwenye nambari 6 Happy Kibaho .?
Tangu ukumbi wa Diamond jubilee ujengwe
hakujawahi kutokea shangwe kubwa kama hii
ya usiku huu ya kuushangilia ushindi wa
Happy .Mrembo huyu alifanikiwa kuzikonga
nyoyo za watu vwengi.
Patrick alishindwa kujizuia hisia zake
akainuka na kushangilia kwa nguvu sana.
Jukwaani Happy machozi yalikuwa
yakimtoka.Hakuamini kama ni yeye ndiye
aliyetangazwa mshindi wa shindano hili hasa
kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo
miongoni mwa washiriki.Watu walikumbatiana
na kupeana mikono ya hongera kuashiria
kukubaliana moja kwa moja na maamuzi ya
majaji ya kumchagua Happy kuwa mrembo wa
Taifa.Kila mmoja aliamini kuwa Happy
alistahili kulitwaa taji lile.
Baada ya kama dakika kumi hivi za hoi hoi na
nderemo muongoza shughuli akapanda tena
jukwaani.
?mabibi na mabwana nafikiri hoi hoi hoi na
nderemo hizi zote ni kuonyesha jinsi gani wote
kwa pamoja tunavyokubaliana moja kwa moja
na maamuzi ya majaji.Happy kibaho ndiye
miss Tanzania wetu mpya.sasa kinachofuata
ni mrembo anayemaliza muda wake kulivua
taji na kumvisha mrembo mpya.?
Zoezi hili likafanyika huku likishangiliwa kwa
nguvu sana.na baada ya zoezi hili kukamilika
muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.
?mabibi na mabwana tukio linalofuata sasa ni
la kumkabidhi Miss Tanzania funguo za gari
lake.Tunamuomba mkurugenzi mkuu wa
Masimulizi entertainment ambao ndio
wadhamini wakuu apande jukwaani na
kumkabidhi Miss Tanzania funguo hizo.?
Petty woris mkurugenzi wa Masimulizi
entertainment akapanda jukwaani na bila
kupoteza muda akamkabidhi Happy funguo za
gari ambalo ni zawadi ya mshindi wa
kwanza.Akiwa katika tabasamu pana sana
alipita jukwaani huku akizipunga funguo
hewani .Kelele za kushangilia zilisikika.
Baada ya zoezi hilo zikafuata burudani mbili
kisha mashindano yakafungwa rasmi na
taratibu umati wa watu ukaanza kuondoka
maeneo hayo ya Diamond jubilee kila mmoja
akiwa amesuuzika vilivyo na ushindi wa
Happy kibaho.
Happy sasa alikuwa akipiga picha na watu
mbali mbali huku akisongwa na waandishi wa
habari wakitaka kufahamu mawili matatu
ingawa mkurugenzi wa Miss Tanzania
alijitahidi kuwazuia kwani Happy angefanya
mkutano na waandishi wa habari hapo kesho
lakini haikusaidia kitu.
Patrick ambaye alionekana kuchanganyikiwa
kadiri muda unavyosonga alitoa simu yake na
kuanza kubonyeza namba kisha akajitenga na
akina Andrew ambao kwa sasa walikuwa
wamesimama wakijiandaa kuondoka.Patrick
aliitumia njia ile ya kujifanya anapiga simu ili
aweze kuondoka mahala pale bila kutiliwa
mashaka kwani lengo lake kuu lilikuwa
kujaribu kupata nafasi ya kuonana na Happy
.Andrew alielewa mara moja nini kilichokuwa
kikiendelea akawaomba akina Vero na Vick
waondoke mahala pale waelekee katika
magari.Lengo lilikuwa kuwatoa wasiwasi
akina Vero.
Patrick sasa alikuwa akipigana vikumbo na
waandishi wa habari ambao walikuwa
wakichukua picha na kumuuliza Happy
maswali mawili matatu.Alijitahidi sana
kupenya na hatimaye akajikuta yuko mahala
ambako anaweza kumuona Happy kwa
ukaribu.Jasho lilikuwa likimtiririka na moyoni
alikuwa na wasi wasi mwingi lakini hii
haikukumkatisha tamaa ya kuonana na Happy
.Alikwisha azimia hivyo.Alijisogeza taratibu
na hakuna mtu yeyote aliyeweza kuwa na
shaka naye kuwa si mwandishi wa habari tena
toka katika chombo cha habari kikubwa hapa
nchi au nje ya nchi kutokana na muonekano
wake.
?Hongera sana Happy madame
Tanzanie?Alisema Patrick wakati huo akiwa
uso kwa uso na Happy .Happy kwa wakati huo
hakujua aliyekuwa akiongea naye .Alijua wote
ni waandishi wa habari.Lakini neno lile
?Madame Tanzanie?linamstua na kumfanya
ainue uso wake na kumtazama vizuri mtu yule
aliye mpa salamu ile.Kwanza alihisi sauti ile
ni kama si ngeni masikioni mwake .mbele yake
alikuwa amesimama kijana nadhifu akiwa
ndani ya tabasamu lenye kuonyesha aina
Fulani ya wasi wasi.macho yake yakakutana
na macho ya Patrick na kwa kasi ya umeme
kumbukumbu ya ghafla ikamjia kichwani
?Noooooo!!!!!!!!!!! Pa???..t?????.?
Akaanguka na kupoteza fahamu.
Kizaa zaa cha ghafla kikatanda hapo
ukumbini.Kwa sekunde kadhaa ikatokea
taharuki kubwa.Kila mtu akapatwa mstuko
kwa kitendo cha Miss Tanzania kupoteza
fahamu ghafla.
Haraka haraka walinda usalama wakamwinua
na kumkimbiza katika gari la wagonjwa
ambalo lilikuwa nje tayari kabisa kwa dharura
kama hii.Kwa kasi ya ajabu gari lile
likaondoka kuelekea Hospitali.
Watu waliokuwa bado wako ukumbini
hawakuamini kilichotokea ghafla vile
.Waandishi wa habari wakalichukua tukio lile
kama lilivyotokea.
Patrick nusura akili imruke kwa kitendo cha
Happy kupoteza fahamu.Taratibu alihisi
kuishiwa nguvu lakini tayari Andrew alikuwa
ameshafika ,akamshika mkono na kumtoa nje
ya ukumbi .
 
Saa kumi na moja asubuhi miss Tanzania
Happy alizinduka.akaangaza huku na huku
akatambua kuwa alikuwa hospitali.Taratibu
akaanza kukumbuka kilichotokea na kumfanya
awepo pale hospitali mida ile.Akalikumbuka
tukio zima lililotokea usiku wa jana.
? that?s him?I saw him..? Happy akajikuta
akiongea mwenyewe kwa sauti na kuwastua
watu waliokuwemo mle chumbani.Miongoni
mwa watu waliokuwa wakifuatilia kwa karibu
hali ya Happy ni mdogo wake Margreth
.Alikuwepo pia mkurugenzi wa Miss Tanzania
pamoja na watu wengine kadhaa.Mara tu
waliposikia kuwa ameamka mkurugenzi wa
Miss Tanzania alimwita daktari ambaye
alikuja na kumpima.Baada ya vipimo vyote
kuonyesha hakuna tatizo zaidi ya mstuko wa
kawaida daktari alimuomba Happy aendelee
kupumzika na asibughudhiwe.Daktari
akawaomba wote waliokuwa pale Hospitali
kwa ajili ya Happy waende kupumzika na
kumwacha mgonjwa apumzike kwani bado
alihitaji mapumziko ya kutosha.Ni margreth
pekee ndiye aliyebaki ili kumsaidia dada
yake.Baada ya watu wote kutawanyika Happy
akageuza kichwa na kumwita margreth.
?my sister Pole sana?akasema Margreth
?I?m ok magie.? Akasema Happy
?happy what real happened? Akauliza tena
Margreth.happy akanymaza akafikiri kidogo
akasema
? Magie I saw Patrick yesterday?
?Whaaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!?akauliza margreth kwa
mshangao mkubwa.
? Patrick huyu huyu ambaye wote tunaamini
amekufa..? akasema Happy
? Parick is dead..yawezekana uliona mzuka
wake? akasema margerth.
?Hapana Margreth haukuwa mzuka..Nilikuwa
na akili zangu timamu wakati ninamuona
patrick? akasema Happy.Margreth akainuka
pale alipokuwa amekaa akamtazama dada
yake na kusema
? Happy hebu jaribu kumsahau Patrick..he?ll
never come back..he?s gone forever? akasema
margreth..akamtazamatena dada yake na
kumuuliza
?Sister are you ok?...
?Sina tatizo magie ni kweli nilimuona Patrick
jana wakati nikiongea na waandishi wa habari
alikuja mbele yangu na kunisalimu .Alitaja
maneno Fulani ambayo yalinifanya nistuke na
nilipomtazama vizuri alikuwa ni yeye.Nina
hakika ni yeye kwani ni mtu ambaye yuko
moyoni mwangu kwa miaka mingi na kila siku
ninaangalia picha yake hivyo siwezi kuwa
nilimfananisha.Ninaamini nilimuona Patrick
na ndio maana nikastuka hadi kupoteza
fahamu.I?m confused Maggie .Totaly
confused.?
Kimya kikatanda mle chumbani .
?Margreth tafadhali usije mweleza mtu yeyote
juu ya habari hii.?
?Usijali sister siwezi sema?
?Sasa magie naomba unisaidie.?Akasema
Happy .
?Nikusaidie nini Happy?
?nataka kuonana na Patrick?Akasema Happy
huku macho yake yamefunikwa na machozi.
?Pumzika kwanza sister ukitoka Hospitali
tutaongea kwa undani juu ya suala hili.Kwa
sasa bado unahitaji mapumziko ya kutosha
na huhitaji kuwaza sana juu ya suala hili.?
?Thanks Maggie I understand ? Akajibu Happy.
mara mlango wa chumba alimolazwa Happy
ukafunguliwa wakaingia wazazi wa Happy
ambao walikuwa safarini lakini kutokana na
matatizo aliyoyapata mtoto wao ikawabidi
waahirishe safari yao na kurudi Tanzania
haraka.mama yake akamkumbatia huku
machozi yakiwatoka wote .baada ya
kusalimiana Happy akawahakikishia kuwa kwa
sasa alikuwa akijisikia mzima kabisa na
pengine mchana wa siku hiyo angeruhusiwa
kurudi nyumbani.
Wakiwa katika maongezi akaingia muuguzi
akiwa na sinia la dawa.akawaomba radhi wote
waliokuwa mle ndani kuwa alihitaji
kumuhudumia mgonjwa hivyo akawaomba
watoke nje kwa dakika kadhaa.Alipohakikisha
wote wametoka akamkaribia Happy .
?Samahani dada Happy nina ujumbe wako
ambao nimeambiwa ni wa muhimu na nyeti
sana .Aliyenipa ujumbe huu amenionya
kwamba nisikupe mahala penye watu .?
?Nani aliyekupa ujumbe huu?
?simfahamu ila ni kijana mmoja alikuwa
amevaa suti nyeusi na hakujitambulisha jina
lake .yeye alisema ukishausoma tu utakuwa
umefahamu.?
Yule muuguzi akatoa bahasha toka katika
mfuko wake wa koti na kumpatia.baada ya
kumpatia dawa muuguzi yule alitoka na
kumwacha Happy jasho likimtiririka.Hakujua
ni nani aliyeleta ujumbe ule.
Aliishika bahasha ile na kuifungua
taratibu.Ilikuwa ni kadi nzuri iliyomtakia
uponaji wa haraka.Ndani ya kadi ile
kikaanguka kikadi kidogo .Akakiokota na
kukisoma.Nusura apatwe na wazimu baada ya
kuisoma kadi ile.Margreth akaingia na
akastuka sana kwa uso wa furaha aliokuwa
nao Happy.
?Happy kuna nini?Mbona umefurahi namna
hiyo? akauliza margreth kwa mshangao.
?Its Patrick?
?Patrick !!!!!!!!!!!!!!!?
?Yes .Look at this? akasema Happy
akimuonyesha Margreth ile bussines card
?Mhhh?margreth akaguna
Wakati margreth akiisoma ile kadi mlango
ukagongwa na likaingia kundi la
warembo.wote wakafurahi baada ya kumkuta
Happy ni mwenye furaha namna ile.
************************************************
MISS TANZANIA AZIMIA JUKWAANI,HAPPY
KIBAHO MISS TANZANIA MPYA,ZENGWE
LATAWALA UKUMBINI MISS TANZANIA
AZIRAI,Hivyo vilikuwa ni baadhi ya vichwa vya
habari vilivyotanda katika magazeti mengi
kwa siku hiyo.Karibu magazeti yote yalijaribu
kuandika kwa kina juu ya tukio la kupoteza
fahamu kwa miss Tanzania ukumbini,lakini
hakuna hata gazeti moja lililoweza kuandika
au kuufahamu ukweli juu ya tukio lile.
Akiwa katika kibanda cha kuuzia magazeti
asubuhi hiyo Andrew alinunua karibu kila
gazeti lililotoka siku hiyo na kupitia habari ya
Happy .Lengo lake kubwa ni kutaka kufahamu
kama kuna mtu yeyote aliyeweza kumtilia
shaka Patrick kuwa ndiye aliyekuwa chanzo
cha tukio lile la kuanguka Happy
ukumbini.katika magazeti yote hakukuta
habari yoyote iliyomuhusisha Patrick na tukio
lile.
Akatoa simu yake na kumpigia Patrick na
simu ikapokelewa na Vero.
?Hallo shemeji? Akasema Andrew .
?Shemeji mambo vipi?habari za toka jana ?
Andrew akauliza
?Habari nzuri tu shemeji?
?Vipi jamaa bado kalala?
?Ameingia maliwatoni kidogo anakuja sasa
hivi?
Muda huo huo Patrick akatokea Vero akampa
simu na kumwambia Andrew anahitaji
kuongea naye.
?Hallow Andrew habari za asubuhi ndugu
yangu? Akasema Patrick
?Poa Patrick vipi maendeleo yako?
?Nashukuru Mungu Andrew naendelea
vizuri.Hebu nipe habari?
?Habari ni ndefu kidogo lakini kwa ufupi tu ni
kwamba leo sijalala kabisa.baada ya
kuachana pale ukumbini nikamrudisha Vick
kwake halafu nikaanza kufuatilia Happy
alipelekwa hospitali gani.Kwa msaada wa
rafiki yangu mmoja nilifanikiwa kujua mahala
Happy alikopelekwa.Unajua walificha juu ya
hospitali alikopelekwa kwa sababu ya
kuwakwepa waandishi wa habari.Alikuwa
amepelekwa katika hospitali moja ya kanisa
maeneo ya msasani.Mpaka saa kumi na mbili
nilikuwa pale hospitali na ndipo nilipopata
taarifa kuwa tayari Happy alikuwa
amezinduka.Kuna muuguzi mmoja
anafahamiana na Vick pale na ndiye huyo
aliyenipa msaada mkubwa sana.Nilimpa kiasi
Fulani cha pesa yule muuguzi na kumuomba
aipeleke business card yako kwa Happy na
kumwambia apige namba zile zilizoandikwa
katika business card hasa muda wa
mchana.Yule muuguzi akajitahidi na
kuifikisha kadi ile .Baada ya kuhakikisha
tayari ameipata mimi nikaondoka.Kabla
sijafika nyumbani nikaona nipite kwanza
katika kibanda cha magazeti ili nione
magazeti yanasema nini lakini hakuna
chochote kibaya.Kwa hiyo Patrick nina imani
muda wowote Happy anaweza akakupigia
simu.Mimi kwa sasa nakwenda nyumbani
kupumzika tutaonana baadae ila be carefull
brother?
Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akasema
?Sijui hata nikushukuruje Andrew kwa kitu
ulichokifanya ila nasema thanks a lot.Dont
worry I?ll be careful.Bye see you later?
Patrick akakata simu kisha akaelekea jikoni
ambako Vero alikuwa akiandaa stafstahi
.alianza kumsaidia Vero kuandaa mlo wa
asubuhi kitendo ambacho Vero alikifurahia
sana nakuamini tayari Patrick alikuwa
amerudia hali yake ya kawaida.
*******************************
Saa sita kamili mchana Happy akaruhusiwa
kutoka hospitali.akiwa na furaha isiyokifani
huku ameongozana na mama yake pamoja na
mdogo wake kipenzi Margreth bila kumsahau
mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania akiwa
na wajumbe kadhaa wa kamati hiyo pamoja
na ujumbe wa watu toka sean woris
entertainment ambao ndio wadhamini wakuu
wa mashindano hayo walilakiwa na kundi
kubwa la warembo waliokuwa wakisubiri atoke
kwani walikwisha taarifiwa kuwa
angeruhusiwa mchana.Walitumia kama robo
saa kusalimiana na kupongezana vile vile
kupeana pole kwa yaliyotokea. Kisha
akapanda gari na kuelekea nyumbani
kwao.Happy alikuwa ni mwenye furaha sana
mchana huo.Ni margreth pekee ndiye
aliyefahamu siri ya furaha ile aliyokuwa nayo
dada yake.akiwa garini Happy akafumba
macho kana kwamba amelala lakini alikuwa
amezama katika mawazo na mara akajikuta
akitamka kwa sauti.
?Thanks God I found him?
mama yake aliyekaa kiti cha mbele aligeuka
na kumuangalia mwanae bila kusema kitu.
Margreth yeye alikuwa katika lindi la mawazo
na hasa akijaribu kuvuta taswira ya
kinachoenda kutokea huko mbeleni.Anafaha
mu wazi kuwa katika dunia hii Patrick ndiye
mwanaume pekee ambaye Happy anampenda
.Licha ya kupotezana kwa muda mrefu lakini
bado taswira ya Patrick haikufutika moyoni
mwake.Kwa sasa Happy tayari ana pete ya
uchumba ambayo amevishwa na mchumba
wake ambaye ni mmarekani mweusi aitwaye
Mike cambel anayefanya kazi katika ubalozi
wa Marekani hapa nchini.Mike ni kijana
anayependwa sana na kila mtu katika familia
ya akina Happy .Pamoja na kuwa na pete ya
uchumba kidoleni bado Happy ameshindwa
kuifuta kabisa kumbukumbu ya Patrick
moyoni mwake.Kuonekana kwa Patrick ni wazi
kunaweza kusababisha mvurugano mkubwa
ambao ni ngumu kujua hatma yake.Ni wazi
Mike alikuwa akimpenda Happy kupita
maelezo.Hiki ni kitu kilichomuumiza sana
kichwa Margreth.
Baada ya mzunguko mrefu hatimaye
wakawasili nyumbani ambako walilakiwa na
kundi jingine la warembo,ndugu jamaa
marafiki na waandishi wa habari wote
walifika kumpongeza na kumpa pole Happy
.Kisha salimiana na kupongezana Happy
akaomba aachwe kidogo apumzike.
Happy akaoga na kupata chakula kisha
akaingia chumbani kwake kupumzika.Kitu cha
kwanza kabisa ambacho alikifanya ni
kuitazama tena ile business card kwa makini
.akaichukua simu yake na kuandika namba
zile zilizoandikwa pale juu kisha
akapiga.Mapigo ya moyo wake yalikuwa
yakienda kwa kasi ya aina yake.Mikono
ilianza kuloa jasho kwa wasi wasi.Hakujua
angeongea nini baada ya kuisikia sauti ya
Patrick.Hakujua Patrick angekuwa katika hali
gani mara atakapoisikia sauti yake.Wakati
akisuburi kujibiwa na sauti ambayo aliamini
moja kwa moja ingekuwa ni ya Patrick
akasikia kitu ambacho hakukitarajia.Ilikuwa ni
sauti ya mwanamke ndiye aliyepokea simu ile
ya Parick.
?hallow?Ilita sauti ya upande wa pili.
Happy mikono ilimtetemeka,akapatwa na
kigugumizi cha ghafla kilichomfanya ashindwe
kuongea.
?hallow nakusikia?Iliuliza tena ile sauti ya
mwanamke.
Happy akashindwa ajibu nini akabaki
ameiweka simu sikioni.
?Haloo nani mwenzangu?Iliuliza tena..Tayari
Happy chozi lilikuwa likimtoka.Mara akasikia
simu ikikatwa.Kitendo kile kikamuuma
akajitupa kitandani machozi yakimtoka.
?Oooh Lord why me???Why me God?I love
Patrick .Yes ni yeye tu ndiye mwanaume
ninayempenda kwa dhati ya moyo wangu
.Nimetengana naye muda mrefu sana na
sielewi maisha yake kwa sasa.nadhani
anaweza kuwa na mke au girlfriend.Sielewi
kama ninaweza vumilia nikisikia Patrick
anamke.I?m her only girl.Yes I know that.I
know he loves me very much.?
Happy alikuwa kijisemea peke yake kwa sauti
ndogo
?Patrick I?ll fight for you and I must win you
back.You are mine Patrick .I lost you once
and now I?ve found you I?ll never loose you
again?
Happy alikuwa akiongea peke yake maneno
haya huku machozi yakimchuruzika.
Patrick leo huamki?alisema Vero huku
akimtingisha Patrick ambaye alikuwa amelala
tangu alipokula chakula cha mchana.Patrick
akajigeuza na kuangalia saa kubwa ya
ukutani.Ilionyesha ni saa kumi na moja jioni.
?Oh nimelala sana?
?Ni vizuri hata hivyo ukipata mapumziko ya
kutosha?
Happy akaelekea jikoni akaleta juice na
kummiminia Patrick katika glasi.
?Halafu nimekumbuka kuna mtu alikupigia
simu nikaipokea lakini cha ajabu hakutaka
kuongea kitu chochote .Nimemuuliza zaidi ya
mara mbili yeye ni nani lakini hakunijibu.?
Patrick moyo ukamruka.Kijasho kikaanza
kumtoka .akaichukua simu na kuziangalia
namba zilikuwa ni ngeni kabisa
kwake.Hakufahamu zilikuwa ni namba za nani
lakini akahisi huenda Happy ndiye
aliyepiga.Kwa mujibu wa maelezo ya Andrew
ni kwamba alimuelekeza Happy apige mida ya
mchana.Bila kukawia akaipiga ile namba.Simu
ikailiita sana bila kupokelewa,ikak
atika.Akapiga tena mambo yakawa ni yale
yale.Akapiga kwa mara ya tatu simu
ikapokelewa.
?Hallow?Ilikuwa ni sauti tamu sana ya mtoto
wa kike.kabla Patrick hajaongea lolote simu
ikakatika.Patrick akaipiga tena na safari hii
akaambiwa kuwa simu anayopiga haipatikani.
Patrick akaitupa simu kitandani kwa hasira
.Hakuelewa sababu ya kukatiwa simu na
mwanamke yule na mbaya zaidi kuizima
kabisa.alisimama na kuzunguka zunguka
humo chumbani huku Vero akimwangalia.Al
isahau kama Vero alikuwa karibu yake .Vero
ambaye muda wote alikuwa akimtazama
alipatwa na wasiwasi.
?Patrick dear kuna kitu gani kibaya mbona
umebadilika hivyo?
Patrick akastuka na kujilaumu sana kwa
kuonyesha hali ile mbele ya Happy .
?Ah No darling hata mimi nashangaa huyu
mtu sijui ni nani ananipigia simu
haongei,mimi nikimpigia anakata simu na
kuizima kabisa.Mbona ananipa wasiwasi?
?Basi usijali darl unajua kuna wakati mtu
anaweza akakosea namba na akajikuta
akimpigia mtu mwingine bila ya yeye
kujua.Nadhani hata huyu alikosea namba na
ndio maana akaona hakuna sababu ya
kuongea na wewe kwani hauna umuhimu
kwake.?
?hata mimi nafikiri hivyo?akajibu Patrick.
?Relax my dear achana naye huyo
asikusuumize akili bure .kaa bwana tupange
mipango ya harusi yetu.?
Patrick akastuka kwa ndani baada ya kuiskia
habari ile ya harusi.lakini alijitahidi ili Vero
asiweze kuuona mstuko ule.Jasho lilikuwa
likimtoka.
 
hivi ungeandikiwa hvyo na mtu mwengine ungeweza kusoma au ndio makusud?
 
ENDELEA.................
MALANGALI SECONDARI -IRINGA
Ni ijumaa iliyotawaliwa na kiubaridi cha
asubuhi.Hakukuwa na dalili zozote za
kuchomoza kwa jua ingawa mida hiyo ilipata
saa nne za asubuhi.Anga lote lilikuwa
limefunkwa na mawingu.Pamoja na hali hii
lakini shughuli ziliendelea kama kawaida.Kwa
watu wa eneo hili hali hii walikwisha izoea.
Saa nne na dakika kumi basi moja linalofanya
safari zake kati ya Mbeya na Iringa lilifunga
breki katika kijiji cha Mbalamaziwa.Dakika
kama mbili hivi tangu basi lile lisimame
kijana mmoja akashuka akiwa na mabegi
matatu.Ilionyesha dhahiri kuwa kijana yule
alikuwa mwanafunzi.Baada ya kuhakikisha
kuwa mizigo yake yote iko salama basi
likaondoka na kumwacha kijana yule
akiangaza angaza macho kana kwamba kuna
kitu alikuwa akikitafuta.Muda ule ule jamaa
mmmoja akamfuata.
?Vipi dogo unaelekea Malangali?
?Yes brother ?
?Ok gari ile pale ya kuondoka .Tunaondoka
sasa hivi likijaa.?
Jamaa yule kumbe alikuwa ni
dereva.Akamsaidia kubeba mizigo yake hadi
katika gari dogo aina ya Toyota pick
up.Kutoka hapo Mabalamaziwa hadi kijiji cha
Malangali usafiri unaotumika ni huu wa gari
ndogo.Gari lile halikuwa na abiria yeyote
ndani zaidi ya mizigo.
? mbona hakuna abiria yeyote humu??Akauliza
kijana yule
?Usijali dogo watu wapo si unaona mizigo yao
hiyo hapo.We utaona nikipiga honi tu
watakuja.Si unawaona wale wote ni abiria
wengine wanakunywa chai kule na muda wa
kuondoka ukifika basi watakuja..Unaweza
kwenda kupumzika pale kwa yule dada naye ni
mwanafunzi anaelekea huko huko Malangali
wakati tunasubiri watu wawili watatu?
Katika kibanda kimoja kilichokuwa hakitumiki
msichana mmoja alikuwa amekaa akisoma
kitabu chake cha hadithi.Alikuwa amekiinamia
kitabu hali iliyoonyesha kuwa alikuwa
amenogewa sana na kilichoandikwa kitabuni.
?Dada habari yako? Dada yule alistuliwa na
sauti ya kijana yule .Kwa sekunde kadhaa
alikaa kimya akimtazama yule kaka .Sijui ni
kwa nini alifanya vile lakini ni wazi alionyesha
mstuko Fulani.
?Nzuri habari yako?akajibu kwa sauti laini na
y a taratibu sana.Sauti ile ilionyesha kuwa
dada yule hakuhitaji sana kusumbuliwa kwa
wakati ule kwani baada tu ya kuitikia salamu
ile akainama na kuendelea kusoma kitabu
chake.Akiwa pembeni yake alimtazama yule
dada kwa sekunde kadhaa na kugundua ni
kwa nini alikuwa vile.Dada yule alikuwa na
uzuri wa kipekee.Alikuwa mweupe ,mwenye
nywele ndefu zilizorudishwa nyuma vizuri na
kumfanya avutie zaidi.Alikuwa ni
mwembamba na mrefu wastani.Binti huyu
alijaaliwa sura nzuri yenye uzuri wa kipekee.
?Mhh basi hii shule ninayoenda kusoma si
mchezo.Kama kuna watoto wazuri kama
huyu.halafu ana nyodo kweli lakini ngoja
nimuulize maswali mawili matatu akikataa
kunijibu basi nitaachana naye .?akawaza yule
kijana
?dada samahani nimeambiwa na yule dereva
wa lile gari kuwa na wewe unaelekea
malangali .Na wewe ni mwanafunzi pale?
Dada yule akainua uso wake na kumtazama
yule kijana kama alivyofanya mwanzo.
?Ndiyo kwani vipi?akauliza
? nilitaka tu kufahamu kwa sababu mimi ni
mgeni pale ndio mara yangu ya kwanza nafika
huku hivyo nilikuwa nahitaji kuyafahamu
mazingira ya shule yenyewe kabla hata
sijafika?
dada yule akamtazama tena .Macho ya binti
huyu yalikuwa meupe na makali kiasi kwamba
unaweza ukakwepesha macho yako
asikuangalie.
?Wewe unatokea wapi?
?Natokea Mazwi secondary Sumbawanga?
?Uko kidato cha ngapi?Akauliza tena yule binti
?Kidato cha tatu?akajibu yule kijana
?hata mimi niko kidato cha tatu?Akajibu yule
dada.
?Kumbe tuko kidato kimoja??
?Yeah .Ila pale kuna michepuo.Mimi niko arts
na wewe?
?hata mimi niko arts.Vipi unaonaje
ufundishaji wao? Akauliza kijana yule nadhifu
?wanajitahidi kufundisha.Kumetulia na ni
sehemu nzuri kwa kusoma.Mi napapenda
sana?akajibu yule binti
?aisee kumbe nilifanya chaguo zuri?
?hata mimi mwanzoni nilidhani kuwa nilikosea
kuhamia shule hii .Mwanzoni nilipata shida
sana kuzoea lakini mpaka sasa
nimeshazoea?Akajibu yule dada
?Kumbe hata wewe ulihamia?Yule kijana
akauliza
?Yes .Nilikuwa nasoma Mbeya secondary
nikahamia huku.Sikutaka kusoma mjini
nilitaka kusoma mahala tulivu kama huku?
?Umehamia mwaka huu?
?Hapana toka mwaka jana?
Walikwisha anza kuzoeana.Binti yle kumbe
alikuwa mcheshi na muongeaji mzuri.Kwa
upande wake alifurahia sana uchangamfu wa
yule kijana.
?lakini kwa ujumla unaniambiaje kuhusu
mazingira ?kijana yule akauliza.
?mazingira siyo mabaya.Mabweni yapo mazuri
kwa ajili ya wavulana .Sisi wasichana tunalala
hosteli.Ni hosteli nzuri ya kanisa.Wale
wasiopenda kulala hosteli wanapanga vyumba
kijijini.Maisha ni mazuri ukisha zoea ila kwa
wewe nadhani utapata shida kidogo
mwanzoni.? Akasema huku akicheka.
?kwa nini nipate shida?akauliza kijana yule.
?hahhahaha! Basi tu kwa muonekano wako
unaonekana hujazoea shida?akasema huku
akicheka.
Kijana yule naye akacheka sana kisha
akasema
?sasa mimi na wewe nani anayeonekana
hajazoea shida?
?hahahaha ! hata mimi mwanzoni nilipata
shida sana lakini kwa kiasi Fulani kwa sasa
nimeshaanza kuizoea hali halisi ya mazingira?
Kimya kikapita cha kama dakika mbili hivi kila
mmoja akiwaza lake.Yule kijana akauvunja
ukimya.
?Kwani wewe dada waitwa nani?
Binti yule akatabasamu kisha kama
anajishauri vile aseme au asiseme akajikuta
akitamka
?naitwa Happy .Wewe je waitwa nani?
?Mimi naitwa Patrick ?
?Happy nimefurahi sana kukufahamu.Na kama
hutajali nitafurahi ikiwa utakuwa mwenyeji
wangu?
?Hilo tu usijali.Nitakufundisha jinsi ya kunywa
uji na maandazi ya ulanzi?
Wote wakacheka.
?Ulanzi upi?Mbona nasikia ulanzi ni pombe?
?Yes ni pombe tena kule iko nyingi sana ?
?aisee kumbe maisha mazuri huko?
?hahaha ?Happy akacheka.
?Kwani Happy sasa hivi umetoka wapi?
Patrick akauliza.
?Nilikuwa na ruhusa ya wiki moja.Nilikuwa
nimeenda nyumbani mara moja nilikuwa na
matatizo kidogo na leo ndio narudi
shuleni.Twende pale kibandani tukapate chai
unajua niliondoka asubuhi bila hata kunywa
chai? Happy akasema
Wakainuka pale kibandani walikokuwa
wamekaa na kuelekea katika moja ya vibanda
vinavyouza chai .
*********************************
?Haya wale wanafunzi wa Malangali
tumefika.?
Alisema utingo wa lile gari walimokuwa
wamepanda akina Patrick.Yeye na Happy
wallikuwa wanafunzi pekee katika ile gari.
Mida hiyo ilipata saa saba za mchana.safari
ilikuwa ni ndefu kidogo hasa kutokana na
barabara .
?Patrick tushuke?Akasema Happy akiwa wa
kwanza kushuka kisha akaanza kupokea
mizigo ya Patrick. Happy akatoa pesa na
kumlipa yule utingo .
?kata nauli ya watu wawili?
?No Happy nina nauli yangu hapa?akasema
Patrick
?Usijali Patrick just keep it?akasema Happy
huu akitabasamu.
Abiria wote waliokuwamo katika ile gari
macho yao yote yalikuwa kwa binti huyu
mrembo.Kwa muonekano wake alionyesha
dhahiri kuwa alitoka katika familia yenye
uwezo mkubwa kimaisha.wote walistaajabia
uzuri wa binti huyu.
?Poa mrembo karibu tena siku nyingine?
alisema utingo huku akimminyia Happy jicho
moja.
Baada ya gari ile kutimua vumbi na kuondoka
Patrick akageuza shingo na kutazama
majengo ya shule.Idadi kubwa ya wanafunzi
waliokuwa katika mapumziko ya mchana
walikuwa wamesimama wakiwaangalia
.Patrick alishangaa kidogo kwa namna
walivyokuwa wakiangaliwa.Taratibu akaanza
kujiuliza maswali juu ya kuangaliwa kule.Je ni
kwa sababu alikuwa na Happy ?Au ni kawaida
kwa mwanafunzi mgeni kuangaliwa namna
ile?
?Patrick beba begi hilo mimi ngoja nikusaidie
hili hapa.?akasema Happy na kumstua Patrick
?Wow thanks Happy lakini utaweza kulibeba
hilo ni zito sana.Beba hili dogo.?
Wakabeba mabegi yale na kuanza kuelekea
katika ofisi za shule.Ili kufika ofisini ni lazima
upite katikati ya shule.Bado wanafunzi
walikuwa wakiwaangalia na wengine
wakisemezana.Kitendo hiki cha wanafunzi
kuwaangalia kisha kuanza kusemezana wao
kwa wao kilimzidishia Patrick ushawishi wa
kutaka kufahamu kulikoni.
?Happy mbona wanafunzi wanatuangalia
sana ?
?Just ignore them?akasema Happy kwa kifupi.
Wakafika katika ofisi za shule mizigo
ikawekwa chini.
?Hapa ndio ofisi ya mkuu wa shule msaidizi
.Ingia ndani ye ndiye atakayekusajili na
kukupa maelekezo yote.Bye tutaonana baadae
pengine tunaweza kuwa darasa moja?akasema
Happy huku akichanua tabasamu pana na
kuyaonyesha meno yake meupe na mwanya
wa kupendeza katika meno ya juu.
?Nashukuru sana Happy tutaonana baadae?
Happy akaondoka .Patrick akagonga mlango
na kuruhusiwa kuingia.
?Welcome gentleman.where are you from?
Ilikuwa ni sauti ya ukakamavu ya mtu ambaye
Patrick aliamini moja kwa moja kuwa ndiye
alikuwa mkuu wa shule msaidizi.
?From Mazwi secondary school?Patrick
akajibu.
?Ohh Mazwi!How is Mr Yamsebo?
?He?s ok?
Patrick akasajiliwa kisha mwali yule akatoka
nje na kumwita mwanafunzi mmoja na
kumuomba ampeleke Patrick katika bweni la
Shaaban Robert.Mwanafunzi yule akamsaidia
mizigo na kuelekea katika bweni hilo lililo
upande wa juu kabisa wa shule hii.
Pale bwenini akapata kitanda kilichokuwa
wazi akaweka mizigo yake.alijilaza kitandani
huku akijaribu kuwaza jinsi atakavyoweza
kuyakabili maisha mapya ya shuleni
pale..Hakuwahi kusoma katika shule ya bweni
na hii ilikuwa mara yake ya kwanza.
?lakini Happy yupo atanisaidia
kuyazoea.Kama yeye mtoto wa kike amezoea
sembuse mimi ?Ntazoea tu.Halafu shule hii
inaonekana ina wanafunzi washamba sana
kwa nini walikuwa wakituangalia vile wakati
tumeshuka mchana.Au mimi ninaonekana mtu
wa ajabu sana??
Mawazo haya yakastuliwa na sauti ya
mwanafunzi mmoja aliyeingia bwenini humo
kwa kelele.Akamsogelea Patrick na kumsalimu
kisha akaelekea katika kitanda chake
kupumzika.
***************************
Mida ya kama saa kumi na moja jioni Patrick
akaamua kuzunguka zunguka maeneo ya
hapo shuleni.Ilikuwa ni mwishoni mwa wiki
hivyo kulikuwa na pilika pilika nyingi.Ni
wanafunzi wachache tu waliokuwamo
madarasani jioni hii wakijisomea.
Alipofika katika bwalo la chakula akamuuliza
mwanafunzi mmoja yalipo madarasa ya
kidato cha tatu .alitaka kwenda kuyatembelea
na kuangalia mahala atakapo kuwa akisomea.
Yalikuwa ni madarsa yaliyofuatana.Yaani
kidato cha tatu A B na C.Yeye alikuwa
amepangiwa kusoma kidato cha tatu
C.Akayapita madarasa ya A na B akAelekea
katika darasa la C .Mlango haukuwa
umefungwa akingia ndani na mara macho
yake yakagongana na macho ya Happy .
?Happy ?akaita Patrick
?Patrick!Naona umeshaanza kukata mitaa?
Patrick akacheka.
?Enhee hebu niambie unaendelaje?Vipi
umeshaanza kuzoea?Umepangiwa bweni
gani??
Happy akauliza maswali mfululizo huku
akifunika vitabu vyake.
?Nimepangiwa bweni la ShaAbani Robert na
darasa ni hili hili C?
Happy akatoa tabasamu pana sana.
?karibu sana hata mimi ninasoma humu
humu.?
?nafurahi sana kufahamu kuwa tutakuwa wote
darasani.Vipi mbona uko hapa peke yako?
?Nimeamua tu kuja kukaa huku kwa sababu
kule hosteli ninaboreka sana.Mara nyingi
hupenda kuja huku kujisomea
mwenyewe.sipendi kelele.?
?nimeambiwa kuwa kuna maktaba huku
?Patrick akauliza.
?Yes ipo lakini mimi sipendi kwenda mara
nyingi huwa nakuja huku darasani.Sipendi
kusoma na watu wengi.Patrick naomba tuwe
tukisoma wote?
Patrick akatabasamu kisha akasema.
?Usijali Happy tutasoma wote tena nimekuja
na materials ya kutosha?
waliongea mpaka ikafika mida ya saa kumi
na mbili Happy akaomba Patrick amsindikize
kurudi hosteli kwao.Bila hiyana Patrick
akakubali.wakatoka wote darasani wakaanza
kupanda kilima kuelekea hosteli ya akina
Happy .Kila mwanafunzi waliyekutana naye
alikuwa akiwatazama.Patrick akaamua
kumuuliza Happy
?Happy mbona kila mtu tukikutana naye
anatuangalia sana kwa nini?Toka tumefika
mchana naona watu wakitushangaa mno !!
Happy akatabasamu kisha akajibu
?Achana nao hao.Patrick ,Jali mambo
yako.Kamwe usiwasikilize wanafunzi wa hapa
wana mambo ya kipuuzi sana.Unajua wakiona
mtu mgeni sijui wanakuwaje.wewe ukitaka
kuishi kwa amani mahala hapa jitahidi
kufuata kilie kilichokuleta yaani masomo?
Happy akajibu kwa sauti ambayo haikuwa ile
yake ya kawaida.Patrick hakutaka kuuliza
tena kuhusu suala hilo.
?Patrick kesho jumamosi kuna mnada hapo
kijiji cha mbele vipi ungependa kwenda?
?Yes ni vizuri kama nikienda ili nianze
kuyazoea mazingira?
?Ok nitakupitia basi mida ya saa tano ili
tukashinde huko mpaka jioni huwa ni pazuri
sana.Unajua weekend hapa shuleni panakuwa
kimya mno.Halafu kama utapenda jumapili
tutaenda sehemu moja inaitwa stone beach.Ni
pazuri pia.Mi huwa napenda kwenda kutulia
kule siku kama hizi za weekend.?
?Wow usijali Happy tutakwenda?
Hatua chache mbele yao wakaliona geti la
kuelekea hosteli ya wasichana wakaagana na
Patrick akarejea bwenini.
Saa nne na nusu asubuhi siku iliyofuata
alikuja mpishi katika bweni alilokuwa akilala
Patrick na kuanza kumuulizia.
?wewe ndio Patrick? akauliza mzee yule wa
makamo baada ya Patrick kujitokeza.
?Yes ndio mimi?Ptrick akajibu
?Nimeagiziwa na binti mmoja anaitwa Happy
kuwa anahitaji kukuona sasa hivi .Panda na
barabara utamkuta pale mbele karibu na
kanisa anakusubiri.?
?Ok mzee nashukuru?
Mzee yule akaondoka kisha Patrick akavaa
viatu vyake akaondoka kuelekea mahala
alipoagiziwa na Happy .siku hii alikuwa
amependeza vilivyo.alikuwa amevaa kaptura
ya jeans rangi nyeupe,juu akavaa fulana nzuri
yenye mistari ya kijani na nyeupe halafu
akavaa na mkufu wake wa dhahabu
uliomfanya avutie zaidi.Chini akavaa raba
nzuri nyeupe na soksi nzuri .Mwisho kabisa
akajipulizia uturi wenye harufu nzuri .Kwa
ujumla alikuwa amependeza sana kijana
huyu.Wakati akitoka alisikia baadhi ya
wanafunzi waliokuwa hapo bwenini wakifanya
usafi wakinong?onezana.
?alaaa kumbe ndo huyu?
?Du ! bonge la brother lakini maskini .haelewi
?akadakia mwingine.
Patrick hakutilia maanani sana minong?ono ile
akawapuuza na kuondoka zake.Alitamani
sana kuonana na Happy kwani aliamini ni
yeye tu ndiye anayeweza kumfanya akazoea
mazingira yale magumu.Tangu amewasili
bado hajapata rafiki wa karibu kama Happy .
Kwa mbali alimuona Happy amekaa chini ya
mti amejiinamia.Moyo ukafurahi baada ya
kumuona tena binti yule mrembo.Kwa mbali
tu aliweza kutambua utofauti katika
muonekano wa Happy .
?Hi Happy mambo vipi ?
?Poa tu Patrick Vipi mzima? Akasema Happy
halafu akainua macho
Patrick akastuka kisha akauliza
?Happy kulikoni mbona macho mekundu na
inaonyesha ulikuwa ukilia.Unaumwa?
Happy akanyamaza na kuanza kulia kwa
kwikwi.Patrick akajua lazima kuna kitu
kimemsibu binti yule.akatoa kitambaa na
kumpatia
?Chukua hii futa machozi?
Happy akachukua kitambaa kile na kufuta
machozi.
?Niambie Happy kitu gani kimekusibu mpaka
ukawa katika hali hii?
?Patrick naona nitashindwa.?
?kwani kuna nini Happy ?.Niambie kama una
tatizo ili tuone kama tunaweza kulitatua.?
?Patrick nakwambia hapa shuleni mimi nina
matatizo makubwa.Yaani wenzangu
wananichukia sana sijui hata nimewakosea
kitu gani.Mara waseme eti mimi ninaringa
,wanasema eti ninajifanya nina pesa nyingi,eti
ninajifanya mtoto wa tajiri,ndio maana
wamenitenga na hakuna mtu anayetaka hata
kushirikiana nami kitu chochote.Hata kusoma
huwa nasoma peke yangu.Kwa hivi sasa shule
nzima wanajua eti mimi nina ukimwi.Habari
hizo zimesambaa kila mahala na hii ndio
imenifanya nikose hata rafiki.Mimi silijali hilo
kwa sababu ninafahamu mimi mwenyewe
kuwa mambo hayo si ya kweli.Hata baadhi ya
walimu wanaamini hivyo .Kuna siku walikuja
watu wa afya na kuwataka watu wapime afya
zao na karibu wanafunzi wote wakapima
kasoro mimi.Nilikataa kupima kwa sababu
nimekwisha pima toka huko nilikotoka na
zaidi ya yote ninajiamini mimi mwenyewe
kuwa sina.Kwa kipindi hicho walichokuja
kupima watu nilikuwa ninasumbuliwa na kifua
basi baada ya kukataa kupima afya ,
ikawadhihirishia watu kuwa ni kweli nina
ugonjwa huo.Mimi sioni ajabu kwa sababu
hata huko nilikotokea mambo haya yalinikuta
na ndiyo sababu kubwa iliyonifanya
nihame.Huku nako nikakuta mambo ni kama
yale yale .Nilipata taabu mwanzoni lakini
ikafika mahala nikazoea.Nimejaribu kuwa
wazi kuwa mimi sisumbuliwi na ugonjwa huo
wanaodai ninao lakini hakuna anayeniamini
na hasa ukichukulia huu mwili wangu jinsi
ulivyo basi kila mtu anajua
ninaumwa.Namshukuru Mungu kwa sababu
kwa sasa nimekwisha pona lakini hakuna mtu
anayetaka hata kuchangamana nami.Pale
tulipokutana nilikuwa nimetoka tena kufanya
vipimo ili kujua kama ugonjwa ule wa kifua
ulionisumbua kwa muda mrefu umekwisha
kabisa au vipi.na kwa bahati nzuri madaktari
wakanithibitishia kuwa tayari nimepona .Wewe
mwenyewe jana uliona wanafunzi walivyokuwa
wakituangalia wakati nakusindikiza kule
ofisini.wote walikuwa wanakusikitikia wewe.?
Happy akanyamaza na kufuta machozi
yaliyokuwa yakitoka.Patrick akawa kimya
kabisa kumsikiliza.Kijasho kilikuwa
kikimtiririka.
?Kibaya zaidi ni leo asubuhi.Nilikuwa
nimeenda kuoga nikasahau kufunga sanduku
langu .Niliporudi nikakuta pesa zangu zote
karibu laki moja na ishirini na tatu elfu
hazipo.Nimejaribu kuuliza lakini hakuna mtu
yeyote anayejua zimeenda wapi.Ninaelewa hizi
ni njama za wazi za watu wasionipenda.?
Patrick akavuta pumzi ndefu na kumwangalia
Happy kwa makini .alimuonea huruma sana
binti yule kwa matatizo anayoyapata.Sasa
alipata jibu kwa nini wale wanafunzi walikuwa
wakimwangalia sana na hata kusemezana
wao kwa wao kila walipomuona yuko na
Happy .Roho ikamuuma kumuona binti
mrembo kama yule akitoa machozi.Ni wazi
hakustahili kufanywa vile hata kama
angekuwa ameathirika kama wanafunzi hao
wanavyodai..
?Hawa watu wa namna gani ambao
wanawafanya wenzao namna hii?Hivi ndio
tunavyofundishwa kuhusu mapendo kwa
wenzetu?no !! kama wao wako hivi mimi
sijafundishwa namna hii.Wazazi wangu
wamenifundisha kuwa na upendo kwa watu
wote.Lazima nionyeshe mfano kwa watu hawa
na nitaanzia kwa Happy ?Aliwaza Patrick
akiwa na fundo la hasira moyoni.
Taratibu akamuinamia Happy na kumshika
mikono.akamwangalia usoni kwa sekunde
kadhaa kisha akasema.
?Happy usijali ,nyamaza kulia I?m here for
you.I?ll be on your side.Hutalia tena.Hata
kama dunia nzima itakutenga na kusimama
mbali nawe I?ll be there for you.Hata kama
ungekuwa na maradhi hayo wanayosema
unayo nisingeweza kukutenga.?
Happy akapatwa na furaha ya ghafla baada
ya kuambiwa maneno yale akainuka na
kumkumbatia Patrick kwa nguvu.
?Thanks very much Patrick.Nadhani ni Mungu
kakuleta ili uweze kunipa faraja.baba alitaka
kunihamisha na kunipeleka mbali lakini
nilikataa kwa sababu nayapenda mazingira
haya ya huku.Napenda sana kuwa katika
sehemu tulivu kama hii.sikujua kumbe kuna
mtu ana kuja ambaye atakuwa ni faraja
yangu.?
Alisema Happy huku machozi
yakimtoka.hakuamini kwa mazingira yale
kama kuna mtu angeweza kumtamkia maneno
ya faraja kama yale.
?Usijali Happy .Hutalia tena.Usijali kuhusu
pesa zako kupotea.kama ilikuwa ni njama zao
basi wameshindwa.Mimi bado nina kiasi cha
kutosha cha pesa nitakugawia na kiasi
kitakachobaki tutaendelea kukitumia
taratibu.Usijali you are more than a friend to
me.To me you are like my sister.?
?Thanks Patrick.You are more than a brother
to me?akasema Happy
?Thanks. vipi kuhusu ile safari yetu ya
mnadani bado ipo au ndio umeshaifuta?
Patrick akauliza
?Mimi nilikuwa nimeshaifuta kwa sababu hata
kama ningeenda huko ningenunua vitu na
nini?wamechukua pesa zote.?
?Pole sana.sasa hebu nisubiri kidogo hapa
nakuja sasa hivi?
Patrick akamwacha Happy pale na kutembea
kwa kasi kurudi bwenini..akafungua sanduku
lake kubwa na kutoa bahasha Fulani
aliyokuwa ameificha .akaiweka mfukoni
akafunga sanduku lake na kuondoka kurudi
kule alikomwacha Happy .
?Happy chukua hii ni laki moja na nusu
itakusaidia ila kuwa makini sana wasije
wakakuibia tena siku nyingine.?akasema
Patrick wakati akihesabu pesa toka katika ile
bahasha aliyokwenda kuichukua kule
bwenini.Happy hakuamini macho
yake.hakuamini kama katika dunia hii bado
kuna watu wenye moyo wa huruma kama wa
Patrick.
?wow jamani Patrick Naomba kidogo tu sasa
ukinipa hizi zote na wewe je utabakiwa na
nini?
?Usijali Happy bado nina akiba ya
kutosha?Patrick akajibu
?No Patrick siwezi kuchukua zote.?
?Happy kumbuka ulikuwa ukilia kwa kuibiwa
na sasa narudisha kiasi kile kilichokuwa
kimeibiwa ili ufute kabisa suala hilo moyoni
mwako?
Happy akapokea pesa zile.
?nashindwa hata kupata neno la
kukukushukuru litakalokufaa Patrick.Thanks
very much ?
?It?s nothing?Patrick akasema kisha kikapita
kimya kifupi.
?Patrick thanks again unajua nilikuwa nawaza
sana jinsi ya kumwambia daddy kuwa
nimeibiwa kwa sababu si mara ya kwanza na
mwambia hivyo ananitumia pesa Ila kwa sasa
sijui ningesemaje.You are my angel.?
?usihofu kitu Happy muda wowote utakaokuwa
na tatizo usisite kunitaarifu.I will help
you.?Patrick alisema kwa kujiamini.alijisikia
vizuri sana kumsaidia binti yule mwenye
matatizo aliyekuwa ametengwa .
Taratibu wakaondoka mahali pale na kuanza
kuelekea mnadani.
 
We kiboko yaan story yako nilikuwa natoka dar naelekea arusha na bus ndo nimefika arusha sasa na bado sijamaliza...
 
RIWAYA : MISS TANZANIA
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nasema Patrick simuachi na nitazidi kuwa rafiki yake wa
karibu.Patrick ni mtu pekee ambaye amenifikisha hapa nilipo
sasa.Nilikwisha kata tamaa kabisa hata ya kuendelea kusoma hapa
lakini ni yeye aliyenipa moyo na kunisaidia katika kila kitu .Amenipa
msaada mkubwa kimasomo.Ni yeye tu ambaye amekuwa nami siku
zote pale ambapo jamii nzima imenikataa.Potelea mbali
watakavyosema na waseme.Mimi sijali .Mbona wao wana wanaume
kila kona mimi siwafuatiliii mambo yao .Kwa nini basi wao wafuatilie
ya kwangu.?.Lakini hata kama ingekuwa ni kweli ,kuna ubaya wowote
mimi na Patrick kuwa wapenzi?Nadhani hata kama nikiamua kuwa na
mpenzi basi ni wazi ni lazima atakuwa ni Patrick .Kwani ni yeye
pekee mpaka sasa hivi ambaye amekuwa ni mtu wangu wa muhimu
sana.Ni yeye pekee ambaye anaweza kunikosesha usingizi kwa
kutomuona.Je ni kweli kuwa hii ni dalili ya kuchipua kwa penzi kati
yetu? Inaweza kuwa kweli kwa sababu sijawahi kuwa karibu na
mvulana yeyote zaidi ya Patrick.Ni yeye ambaye amenifundisha nini
maana ya kuwa rafiki wa dhati.nadhani hizi ni dalli njema.lakini hata
kama nikiamua kumchagua Patrick kuwa mpenzi wangu
nitamwambiaje?Mhh ! ngoja niachane na haya mambo huu si wakati
wake." akawaza happy.
ENDELEA..................................
Kengele ya dharura ikagongwa ikiashiria kuwa na jambo ambalo si la
kawaida.Wanafunzi wote wakatoka darasani kwa haraka kama
inavyotakiwa mara tu inaposikika kengele hii.Kwa haraka haraka
mistari ikapangwa na huku kila mwanafunzi akiwa kimya akisubiri
kusikia ni nini kitakachojiri.Walimu wote walikuwa wamejipanga na
mara akatokea mkuu wa shule.Wanafunzi mioyo ikawaenda mbio
kwani ni nadra sana kwa mkuu wa shule kuonekana katika eneo hilo
la mkusanyiko.Mara zote anapoonekana eneo hilo huwa ni kwa
sababu maalum tu.
?Habari za asubuhi wanafunzi? Akasalimu wanafunzi.
?Nzuri shikamoo mwalimu?
?Wanafunzi nimesimama mbele yenu asubuhi hii ili kuzungumzia
mustakabali mzima wa maendeleo ya shule yetu.kwa siku za karibuni
shule yetu imekuwa na mambo ambayo katu hayafurahishi na
ambayo yanaenda kinyume na maadili mazima ya mwanafunzi.
Kwanza kabisa kumekuwa na vitendo vya ubaguzi.Wanafunzi
mmeanza kubaguana.Mnawanyanyasa na kuwabagua wenzenu
ambao ni wagonjwa.Hivi ndivyo mnavyofundishwa na wazazi wenu
majumbani? Kuna binti mmoja nimepata malalamiko yake kuwa yeye
ametengwa na wanafunzi wenzake eti kisa ni mgonjwa.Hii ni aibu
kubwa kwa shule yetu..Sasa ninasema hivi kuanzia sasa wewe
ukibainika kuwa unafanya kitendo chochote cha kibaguzi adhabu yake
ni kufukuzwa shule.Sintataka kukuona tena katika shule
yangu.Kuweni makini sana na hilo.Jambo la pili ninalotaka
kulizungumza leo ni nidhamu .Kumekuwa na uvunjaji mkubwa sana
wa sheria za shule.Imefikia mahali sasa ambapo mwanafunzi
anaweza akamgomea hata mwalimu .Mwanafunzi anaweza akafanya
kitu chochote anachotaka bila kuogopa.Hivi kweli wewe mwanafunzi
unaweza ukabishana na kutaka kupigana na malimu wako?mwalimu
wako ni sawa na mzazi wako hapa shuleni.Nasema kuwa kuanzia
sasa sheria na taratibu za shule zitafuatwa kwa ukaribu sana.Endapo
utakwenda nje ya taratibu basi tutakushughulikia kikamilifu.Kwa sasa
naomba nitakaowataja wapiti mbele haraka: Patrick Charles,Happy
kibaho.Mwantumu ramadhani.Pius augustinie,Pili Juma,Maria
asey,Steven amanuli na Benson Chiteu.?
Wanafunzi wale walioitwa ,wakajipanga mbele ya alipokuwa
amesimama mkuu wa shule,halafu akaendelea.
?Hawa mnaowaona mbele yenu mnajua wamefanya nini? Akauliza
mkuu wa shule.wanafunzi wote wakawa kimya .Hakuna mtu
aliyethubutu kusema kitu ingaa walkuwa wakifahamu juu ya ugomvi
uliotokea.
?Wanafunzi hawa walioko mbele yenu walivunja sheria za shule kwa
kugombana darasani.Baada ya kukutwa wkipigana mwalimu
aliyewakamata akawapeleka kwa mwalimu wa darasa Patrick na
mwenzake Happy ambao ndio kiini cha ugomvi wakagoma
kuadhibiwa.Kibaya zaidi ni kwamba Patrick alikuwa tayari kupigana
hata na mwalimu wake wa darasa.Sijui jeuri hii mnaitoa wapi ninyi
watoto..Mwanafunzi unataka kupigana na mwalimu wako kweli? Hii
tabia mbaya ambayo katu haitavumiliwa katika shule yetu.Kingine ni
kwamba Patrick na Happy ambao wote ni wanafunzi wa darasa moja
wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kimapenzi wakiwa shuleni
kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za shule.Bodi
ya shule imekaa na imeamua yafuatayo.Moja wanafunzi Mwantumu
Ramadhani,Pius Augustine,Pili Juma,Maria asey ,steve amanuli,na
Benson chiteu watapata adhabu ya kung?oa kila mmoja visiki vitatu
kwa muda wa siku sita kuanzia leo.Wanapata adhabu hii kwa kosa la
kupigana darasani.Hili ni fundisho kwa wengine .Wanafunzi Patrick
charles na Happy Kibaho wao wanasimamishwa masomo kwa muda
wa mwezi mmoja.Hii ni kwa sababu wamesababisha ugomvi
,wamapigana darsani,wakagomea adhabu ya mwalimu na zaidi ya
yote wanajihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakiwa
shuleni.Adhabu hii ni fundisho kwa wanafunzi wengine.Ninasema
kuwa kuanzia sasa tutakuwa wakali mno kwa yeyote yule ambaye
atajaribu kwa namna yoyote kuvunja sheria za shule.Nasema ole
wenu ,ole wenu.? Mkuu wa shule akamaliza na kuondoka
zake.mwalimu wa zamu akawatawanyisha wanafunzi warudi
madarasani.Sehemu kubwa ya wanafunzi walkikuwa wakifurahia
adhabu ile waliyoipata Patrick na Happy .Kwao uilikuwa ni alama ya
ushindi mkubwa.Katika darasa la akina Patrick ilikuwa ni kama
sherehe.Wanafuzi walikuwa wakipongezana.
Happy macho yalijaa machozi.Alikuwa akilia.Hakuamini kuwa kosa
lille lingepelekea yeye na Patrick wasimamishwe masomo.Hakuwahi
kuota kama iko siku atakuja kusimamishwa masomo.Mbaya zaidi
aliumia moyo kwa uongo wa wazi kabisa .Ni wazi ulikuwa ni
ukandamizaji mkubwa.Zilikuwa ni chuki za wazi .Patrick alikuwa
katika hali ya mstuko kutokana na adhabu ile ambayo kwa kiasi
kikubwa haikuwa ya haki.Ulikuwa ni uonevu mkubwa.Walikuwa
wamesingiziwa uongo mkubwa .Ilimuuma Patrick kwa kiasi kikubwa
lakini hakuwa na la kufanya .tayari maamuzi yamekwisha fanywa na
kilichobakia ni utekelezaji.Kwa muda huu mfupi shule hii ilikuwa
imeanza kumchosha.Taratibu akamsogelea Happy na kumshika
mkono.Akatoa kitambaa mfukoni na kumfuta machozi .
?Happy be strong.Najua inauma sana lakini hatuna jinsi.Tusiwape
faida maadui zetu.Wanapotuona tuko na huzuni ni furaha kwao.Let
us act kama vile hakuna chochote kilichotokea.
* * * *
?Patrick ninasikia uchungu sana ..Kusingiziwa kitu ambacho
sijakifanya inauma mno .Inaniuma sana Patrick?Happy akashindwa
kuvumilia akaanza kulia .Ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja za
jioni walipokutana katika hoteli moja kijijini baada ya kuachana
mchana na kila mmoja akaenda kupumzika na kutuliza akili.Happy
macho yalikuwa yamemvimba na mekundu kwa kulia..
?Kinachoniuma zaidi ni wewe kusimamishwa masomo.wewe
hukustahili kwa namna yoyote ile kuipata adhabu hii.Mimi ndio
chanzo cha haya yote.Mimi ndiye niliyekusababishia matatizo haya
.Ni bora ningesimamishwa masomo peke yangu.Nasikitika sana
Patrick .Naomba unisamehe kwa hilo.Haikuwa adhma yangu na wewe
uingie katika matatizo haya .Najua hustahili adhabu hii???????.?
Akasema Happy huku machozi yakimtoka lakiniPatrick akamzuia na
kusema
?Shhhhhhhhhhhhhhhhhhhh????.?Patrick akamfumba Happy mdomo
kwa kidole.
?Happy usiseme hivyo.Ninafurahi kupata adhabu hii .Ninastahili.Ul
ikuwa ni wajibu wangu mimi kukutetea.Nimetimiza wajibu
wangu.Kumbuka niliahidi kuwa nawe katika kila jambo.Niliahidi
kupambana na yeyote yule ambaye angekufanya ulie.Nimefanya
nilivyopaswa kufanya..Usijilaumu Happy ninastahili adhabu hii
.?Parick akasema kwa kujiamini.Akamuangalia happy kwa makini na
kusema
?Happy si hapa duniani tu hata nikiwa Mbinguni sintavumilia kuona
mtu yeyote akikusumbua.Nitapambana naye.?
Kwa mara ya kwanza Happy akacheka kwa kauli ile ya Patrick..Patric
k akatabasamu kwa kuifanya sura ya Happy ikajaa tabasamu tena.
? Umeanza vituko vyako.Mbinguni hakuna uonevu wa namna hii?
akasema Happy huku akicheka
?nimesema hivyo kukuthibitishia kwamba sintakuwa tayari kuona mtu
yeyote yule akikunyanyasa Happy..? akasema patrick na kumfanya
Happy atabasamu tena
?Happy hii ni vita na sisi ni wapiganaji. kuna msemo wa kiingereza
unaosema winners never quit.Na sisi ndio washindi hivyo tusikate
tamaa.Kukata tamaa ni kuwapa ushindi wale wote wasiotupenda,wa
siotutakia mema.Wao wanapamba na sisi lakini sisi tupambane na
muda.tumeelewana??
?sawa Patrick nimekuelwa.nashukuru sana Patrick sijui hata nipate
neno gani la kukushukuru kwa jinsi ulvyojitoa mhanga juu
yangu.Sidhani kama kuna mwanaume ambaye anaweza kufanya haya
uliyoyafanya kwangu.Kama wapo basi ni wachache mno.?
Patrick akatabasamu na kusema...
?Happy utaanzaje kuwaeleza wazazi wako juu ya tukio hili mpaka
wakakuelewa.? Manake kwa mujibu wa barua zilivyoandikwa za
kuwapelekea wazazi mhh ni hatari tupu.?
Happy akakaa kimya kwa muda kisha akasema.
?Patrick hilo suala linaniumiza kichwa kupita kiasi..unajua baba
yangu ananiamini sana na hajawahi kusikia sifa yangu mbaya hata
siku moja .Siku zote nimekuwa mfano hata kwa wenzangu , leo
akisikia nimesimamishwa masomo mhhh !! sidhani kama kutakuwa na
amani nyumbani.Kuna hatari akakataa hata kunipokea kwa jinsi baba
yangu alivyo mkali.Nilikuwa nafikiria niende kujificha kwa shangazi
yangu Morogoro mpaka adhabu itakapokwisha.Shangazi yangu ni
mwelewa na nina imani nikimwelezea atanielewa.Sitaki baba yangu
afahamu kuhusu suala hili.Akijua tu nimekwisha.Wewe je umepanga
nini? Patrick akafikiri kidogo na kusema
?mimi sina tofauti na wewe hata kidogo.Mzee wangu hatavumilia
akisikia nimesimamishwa masomo.Hata mimi nilikuwa ninafikiria
niende mahala nikatulie mpaka adhabu hii itakapoisha.Mwezi mmoja
si mrefu.?
Kimya kikapita Patrick ambaye alikuwa ameinama akiwaza akainua
kichwa na kusema.
?Happy kuna jambo nimelifikiria.Kwa kuwa sisi sote tuna wazo moja
la kutotaka kuzifahamisha familia zetu juu ya adhabu hii tuliyopata
,kwani hata kama ukienda kwa shangazi yako anaweza akamweleza
tu mzee wako na hapo ndipo itakuwa mbaya zaidi. kama ni hivyo kwa
nini basi tusitafute mahala tukaenda kukaa kwa muda wa huo mwezi
mzima mahala ambako hakuna mtu anayetujua,na tutakaa kwa raha
mstarehe huku tukipata nafasi ya kutosha ya kusoma hadi muda wa
adhabu utakapoisha?
Happy akatabasamu lile tabasamu lake adimu sana.
?That?s a good idea Patrick.Wewe una akili sana.Ni wazo zuri Patrick
.Sasa ni wapi ambako unafikiri tunaweza kwenda kukaa kwa muda
huu wote bila ya kufahamika? Akauliza Happy na Patrick akakaa
kimya kidogo akafikiri kisha akasema
?Umewahi kwenda Bagamoyo??Patrick akauliza.
?hapana sijafika huko?
?Basi ninafikiria twende huko.Kule tutapumzika vya kutosha.Hakuna
mtu yeyote anayetufahamu.Tutakaa kwa raha mustarehe.Tutapata
nafasi nzuri ya kujisomea.Tutatembelea sehemu mbali mbali za
kihistoria.Tutajifunza mambo mengi sana tukiwa kule.Usijali kuhusu
gharama bado nina akiba ya kutosha ya pesa na wala hatutapata
shida kwa muda kwa huo wote wa mwezi mmoja.Nafikiri hii
itatusaidia sana kutoka nje ya ulimwengu huu wa watu wasiokuwa na
upendo hata chembe?
Furaha ya wazi ikajidhihirisha usoni mwa Happy .Hakuwa amewaza
jambo kama lile hapo kabla.Huzuni yote aliyokuwa nayo ikayeyuka
ghafla.
? Patrick nashindwa hata nisemeje.You are my Hero.Toka
nimefahamiana na wewe maisha yangu ytamekuwa na furaha
sana.Najihisi niko slama muda wote ukiwa pembeni yangu.Nafurahi
kwa kuwa najua niko na rafiki anayeyenijali na kunithamini.Sina kitu
cha kukulipa Patrick kwa wema wako huu ?akasema Happy.Patrick
akatabasamu.
? Sifanyi hivi kwa kuhitaji malipo Happy.Ninafanya hivi kwa sababu
moyo wangu umenituma? akasema Patrick.Walijhadiliana mambo
mengi hadi ilipotimu saa moja za jioni wakaondoka kwa ajili ya
kwenda kujiandaa na safari ya kesho yake ya kuelekea Bagamoyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…