Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

Kuwa mzuri bila ya kuwa na akili ni sawa na dereva mwenye leseni lakini ajui kuendesha gari
Wewe ulitakaje??
Repucusion ya kuminywa saana ni kupasuka (bust)
imebust hiyo!!
Karibu CDM Bi Mkubwa na mwana. Si haba!!
 
Una chuma dhambi.unajua kesi aliyonayo ni ya kutumia madawa si kuuza
Naona hujanielewa vizuri mkuu rudia kusoma vizuri utaelewa nilichomaanisha.

Labda nikiweka hili bandiko utanielewa:

Ameandika wakili msomi Tundu Lissu.
___________________________________________________
Sio msokoto wa bangi. Hati ya mashtaka dhidi yake inasema Wema amekutwa na gramu 1.08 za bangi. Gramu, sio kilogramu (kumbuka kilogram 1 ni gramu 1000. Sasa Wema anadaiwa kukutwa na gramu 1). Polisi waliokamata 'madawa hayo ya kulevya' walifanya sachi saa tatu usiku. Sheria inayohusu sachi inasema sachi inatakiwa kufanyika kati ya saa moja asubuhi na saa 12 jioni ili, obviously, kupunguza uwezekano wa polisi kupandikiza ushahidi. Tunamsubiri Paul Makonda mahakamani aje atoe ushahidi wa namna alivyojua Wema anatumia madawa ya kulevya mpaka akamtaja hadharani. Asipokuja basi hakuna kesi.!
 
Utakua hujanielewa labada kwa bandiko hili utanielewa:

Ameandika wakili msomi Tundu Lissu.
___________________________________________________
Sio msokoto wa bangi. Hati ya mashtaka dhidi yake inasema Wema amekutwa na gramu 1.08 za bangi. Gramu, sio kilogramu (kumbuka kilogram 1 ni gramu 1000. Sasa Wema anadaiwa kukutwa na gramu 1). Polisi waliokamata 'madawa hayo ya kulevya' walifanya sachi saa tatu usiku. Sheria inayohusu sachi inasema sachi inatakiwa kufanyika kati ya saa moja asubuhi na saa 12 jioni ili, obviously, kupunguza uwezekano wa polisi kupandikiza ushahidi. Tunamsubiri Paul Makonda mahakamani aje atoe ushahidi wa namna alivyojua Wema anatumia madawa ya kulevya mpaka akamtaja hadharani. Asipokuja basi hakuna kesi.!

Nini maoni yako??
 

Maoni ya nini sasa??Lissu amesema case aliyopelekwa nayo Wema. Ameongelea sheria unataka nini??Sasa unataka tutoe maoni gani??Kwamba Serikali imevunja sheria?? Au Lissu anaipa.angalizo polisi kwamba wanashindwa kabala maana wamekiuka sheria za nchi au unataka tuseme Madaraka hulevya??
 
Tukaneni sana Wema lakini uchaguzi wa 2015 aliwasaidia sana ccm kupata kura za nyongeza
Ni wengi wamechangia ila mchango hauwapi mamlaka ya kuwa juu ya sheria. Kwani kakamatwa Wema peke yake. Mbona wengine waliokamatwa hawahurumiwi. Wema ye yukoje. Kama mna huruma hata wengine nao wangehurumiwa. Hili la kutishia watu sababu ya Wema ndo naona ni upuuzi. Kwahiyo ina maana akiwasaidia Chadema 2020 wakaingia madarakani watamuacha afanye anachotaka? Maana naona ndo message unayotaka kututumia hapo!
 
Naona zile audio zinaenda kukanushwa.......
Nimemsikiliza wema pamoja na mama yake vizuri sana na nimegundua kuwa wema ni a spoiled child na anayemharibia sana ni mama mtu.
Msichana huyu amehusika kwenye controversies nyingi ambazo siyo nzuri lakini inaelekea amezilea mpaka kufika hapa.
Mama mtu anadai kuwa mwanawe amewekwa ndani, ameteswa na kupigwa lakini hakuona kiongozi yoyote yule nyumbani kwake [ila alipigiwa na viongozi 3] Hivi alitarajia nini? hivi kweli wema alipigwa na kuteswa? nimeangalia picha zake wakati anatoka ndani wala hakua na dalili zozote za kupigwa ila alikuwa embarassed and fatigued.
Hivi wema anatofauti gani na vijana wengine? Jee angekuwa hana hata chembe ya hatia kwenye sakata la madawa ya kulevya angepewa na mahama mwaka mmoja wa kuwa chini ya uangalizi na kupaswa kuripoti polisi kila mwezi???? Bahati hii wameipata vijana wangapi nchini?
Waswahili wana misemo 'Mwana umeleavyo ndiyo akuavyo' au 'samaki mkunje akiwa mbichi"
Kwa wao kwenda chadema siyo issue na ingekuwa vizuri zaidi kama angeenda huko mapema maana inasemekana huko vyeo vinakwenda kwa kujuana na sitaona ajabu iwapo mbunge mmoja wa kuteuliwa[chadema] aidha akajiuzulu[sic] au akaondolewa na msichana huyu kuchukua nafasi ya ubunge wa kuchaguliwa.
Kinacho uma ni kwamba baba yake wema alikuwa mcha mungu, mpole sana tofauti naye.
Mbona hatujasikia scandal za ndugu zake wengine??
Somo kwa vijana wengine ni kuwa 'Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu'
 
Baada ya kujitoa CCM na kujiunga Chadema, hatimaye Dada wa hiari wa wema , Mange amewaomba wabunge wa chadema kufanya mchango kwa kila mwezi ili wema aweze kujikimu wakati akikipigania chama

  • mangekimambi_Mi naomba nitoe nasaha kwa Chadema juu ya Wema mapemaaaa ili baadae tusije kulaumiana.
    .
    .
    Mi natoa ushauri kwa Chadema kuwa wawe serious na kumshikilia huyu mtoto mpaka 2020. She is a huge asset. Wasifanye mistake waliyoifanya kwa Wolper!!Kuna mtu aliedhani kuna siku Wolper atageuka?Wolper alitupa shida mnooooo kipindi cha kampenii, Yani alikuwa ndo kamanda wao namba 1 online.Ila baada ya kampeni kuisha mlimsahau kabisaaa... Ubunge viti maalum mkawapa mahawara na magirlfiend zenu ambao hawakuwa na mchango hata robo ya mchango wa Wolper.Okay basi acheni viti maalum, hata kumpa kifuta jasho Mbowe jamani?
    .
    Ngojeni niwaambieni kitu, tusidanganyane hapa kuwa mtu anaweza kukipenda chama akawa anakufa njaaa ila akakomaa na chama.So Mimi nawaambia Chadema although Wema anaapa Miungu yoooote kuwa kaja kwa roho moja na haitaji pesa, mwisho wa siku hakuna kishawishi kibaya kama njaa.Atajikaza mwaka au miaka miwili ila njaa ikimzidia shetani atamshinda.Na CCM mnawajua mbinu zao.
    .
    .
    So Mimi nawaaambia mapemaaa, Mbowe, Mdee , Easter Bulaya and the rest huyu mtoto 'mumshikilie'.She is going to be a huge asset to you kupata kura za watu wengi mnooo.Njaa isikie kwa mwenzio, so don't take her for granted!
    .
    .
    Nawapeni wazo tu, sio lazma mumuweke kwenye payroll ya chama Ila Baba Sasha, Lema, Professor Jay, Mdee, Easter, Mbowe, Mnyika,mkisema kila mwezi kila mmoja wenu achange laki 3 tu za kumsaidia Wema kujikimu hamtoshindwa.Haki hizo kidogo zitamsaidia kuishi na kujikimu na kukitumikia chama.Mkimwacha akapauka asije after 2 years 'akaimisss' CCM tukaanza kulaumiana Hapa. Njaa ni kitu kingine aiseee!
    .
    .
    Hata Wolper Alivyorudi CCM niliweka posti nikasema tusimlaumu Wolper , tuwalaumu Chadema, hawakumthamini, mtoto wa watu aliwasaidia mno.Asikwambie mtu Hata mtu apende chama vipi mwisho wa siku mkono lazma uende kinywani.
    .
    .
    .
    Mimi mwenyewe sometimes naishiwaga nguvu ya kazi Ila ni vile Magufuli ananiogopesha mnooo na issue ya demokrasia na udikteta so najikaza.Ila sometimes huwa natamani niage.So Trust me najua nachoongelea, msaidieni huyo mtoto.. Mapenzi bila pesa huwa ni Magumu sana, iwe mapenzi na mwanaume au na chama, bila pesa mapenzi hayanogiii..







© 2017 INSTAGRAM


Instagram

Find it for free on Google Play.
 
Kama nia yake ni kutafuta. Mshiko basi arudi ccm... Huku ni mapambano kula kwenu.. Chadema si chaka la wachumia tumbo na madaraka..
Wema ni nani Kwenye siasa za bongo? Eti ana followers 2mill..
 
95% out of 2.5m followers in your instagram account can be your haters..and 5% ya waliobaki wanaweza kuwa nje ya nchi...Bado ni ngumu sana kuamini wema kuhamia CHADEMA kuna faida zaidi ya hasara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…