Misikiti, Makanisa kubomolewa Kimara kesho 16/10/2017

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
By Jackline Masinde,Mwananchi jmasinde@mwananchi.co.tz

Nyumba za ibada 24 zinatarajiwa kubomolewa kesho na Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Kimara hadi Kiluvya.

Ubomoaji wa nyumba hizo za ibada ni mwendelezo wa uboamoaji wa nyumba takribani 1300 za wakazi wa maeneo hayo zinazodaiwa kujengwa ndani ya mita 121.5 ya barabara hiyo.

Nyumba zaidi ya 1000 zimebomolewa mpaka sasa hali inayosababisha baadhi ya wananchi kulala nje kutokana na kukosa makazi .

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo kwa njia ya simu Mhandisi wa Tanroads Kimara ambaye anasimamia

ubomoaji huo ,Jonson Rutechula amesema kesho watakuwa na kazi maalum ya kubomoa nyumba za ibada tu.

“Tumewaambia viongozi wa misikiti na makanisa, waondoe vitu kesho tunakuja kubomoa.Tutabomoa makanisa 14 na misikiti 10 kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya”amesema

Amesema shughuli ya ubomoaji wa nyumba imekamilika kwa asilimia kubwa ,zimesalia nyumba za ibada tu.”Kama unavyoona karibu ubomoaji wa nyumba za makazi umekamilika tulibakiza nyumba za ibada”amesema

Ameongeza kwamba “Kesho tutabomoa makanisa 14 na misikiti 10 kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya na tutaanza kazi hiyo asubuhi”amesema Rutechula.

Hata hivyo mwandishi wetu alitembelea Kanisa la Mtakatifu Maria Parokia ya Kimara na kukuta baadhi ya waumini wakitoa vyombo nje na walipoulizwa baadhi ya viongozi waliokuwepo kanisani hapo walikataa kuzungumza .

“Sisi siyo wasemaji, kama unataka habari njoo kesho na kamera zako uchukue matukio lakini pia mtafute Paroko yeye atakwambia nini kinaendelea maana sisi si wasemaji”amesema mmoja wa waumini hao
 
Niliuliza hivi wabomoaji (mwendesha tingatinga) huwa anakuwa na hali gani akitimiza hui wajibu? Niliambiwa tu anakuwa 'under influence'

Ubomoaji huu katika hali ya kawaida hauwezi kukuacha salama, unaweza kuwa umelala zikakujia picha za akina mama na watoto wakililia nyumba zao!
 
Kama watu wanatembea na wake za watu, tena wanawakunja kisawasawa hadi wanatia mimba na hawaumii roho.. sembuse hiyo kazi ya kubomoa nyumba Kwa tingatinga tena penye ulinzi na mshahara?...watu wakatili sana kaka!
 
33d831035f5241ad02165bd47a2e6597.jpg

Haya wazee WA Matungucha bar kwishineyi
 
Niliuliza hivi wabomoaji (mwendesha tingatinga) huwa anakuwa na hali gani akitimiza hui wajibu? Niliambiwa tu anakuwa 'under influence'

Ubomoaji huu katika hali ya kawaida hauwezi kukuacha salama, unaweza kuwa umelala zikakujia picha za akina mama na watoto wakililia nyumba zao!
mkuu mshana jr anasema ili upate kazi ya dereva wa bomoabomoa lazima uwe na roho mbaya,chuki,uwe huna nyumba n.k
 
Niliuliza hivi wabomoaji (mwendesha tingatinga) huwa anakuwa na hali gani akitimiza hui wajibu? Niliambiwa tu anakuwa 'under influence'

Ubomoaji huu katika hali ya kawaida hauwezi kukuacha salama, unaweza kuwa umelala zikakujia picha za akina mama na watoto wakililia nyumba zao!

Mkuu;
Mbona hiyo sio kitu?? Niliona ITV yule mmama kule Chunya akishika kijinga cha moto naye akaiwasha nyumba moja huku wamama wenzie wakiingia ndani ya hiyo nyumba inayoungua kujaribu kuokoa baadhi ya vitu vyao. Je, yule alivaa moyo gani??
 
Kama watu wanatembea na wake za watu, tena wanawakunja kisawasawa hadi wanatia mimba na hawaumii roho.. sembuse hiyo kazi ya kubomoa nyumba Kwa tingatinga tena penye ulinzi na mshahara?...watu wakatili sana kaka!
Ha ha ha haaaaaaa,
Voted as Best Comment of this Week
 
Afadhali Wakatoliki nao wapate kibarua cha kujenga makanisa. Tangu Muitaly awaachie majengo wamebweteka, sisi Walutheri ambao hatukurithi chochote tumejipiga piga weee hadi sasa tuna majengo makali kuliko Roman Catoliki ambalo kiuhalisia ndio kanisa kubwa.
Sie KKKT tumeshazoea kujenga, hatushtushwi na bomoa bomoa. Hata wakibomoa makanisa yote, tutachangishana tena tuanze moja... Kujenga ndio imekuwa kama hobby yetu kwa sasa. Kazi kwao hao ambao wamezoea vya kupewa...
 
Mungu Akusamehe kwani hujui uyasemayo. Nyumba ya Ibada ni sehemu Takatifu, imewekwa Wakfu! Usijisifu kuwa wewe ni Mlutheri, usisikie uchungu Kanisa la Katoliki au Misikiti inapodhalilishwa na kubomolewa. Kumbuka Ukuu wa Mungu, hatustahili hata kulitaja Jina Lake! Kama kweli unamjua Mungu Aliyeumba vyote jifikirie uombe Toba! Kabla hujarusha madongo kwangu, hata mimi pia ni Mlutheri! Lakini kwangu mimi Mungu Ni Pendo!
 
Afadhali Wakatoliki nao wapate kibarua cha kujenga makanisa. Tangu Muitaly awaachie majengo wamebweteka, sisi Walutheri ambao hatukurithi chochote tumejipiga piga weee hadi sasa tuna majengo makali kuliko Roman Catoliki ambalo kiuhalisia ndio kanisa kubwa.
Sie KKKT tumeshazoea kujenga, hatushtushwi na bomoa bomoa. Hata wakibomoa makanisa yote, tutachangishana tena tuanze moja... Kujenga ndio imekuwa kama hobby yetu kwa sasa. Kazi kwao hao ambao wamezoea vya kupewa...

Ni kweli usemalo
 
Back
Top Bottom