Misikiti, Makanisa kubomolewa Kimara kesho 16/10/2017

Misikiti, Makanisa kubomolewa Kimara kesho 16/10/2017

mjomba magu analeta mabadiliko ya kweli.. sio yale ya kuzungusha mikono..

ingekuwa awamu za nyuma wenye hela wangehonga ili nyumba zao ziachwe.. ila awamu hiii unaanzia wapi kuhonga?
 
33d831035f5241ad02165bd47a2e6597.jpg

Haya wazee WA Matungucha bar kwishineyi
Matungucha inabaki bana...ipo upande Wa pili au
 
Mungu Akusamehe kwani hujui uyasemayo. Nyumba ya Ibada ni sehemu Takatifu, imewekwa Wakfu! Usijisifu kuwa wewe ni Mlutheri, usisikie uchungu Kanisa la Katoliki au Misikiti inapodhalilishwa na kubomolewa. Kumbuka Ukuu wa Mungu, hatustahili hata kulitaja Jina Lake! Kama kweli unamjua Mungu Aliyeumba vyote jifikirie uombe Toba! Kabla hujarusha madongo kwangu, hata mimi pia ni Mlutheri! Lakini kwangu mimi Mungu Ni Pendo!
Usiwe na wasi wasi ndugu, Yesu Kristo yeye mwenyewe alitoa ruhusa ya kuvunjwa kwa hekalu pale aliposema, livunjeni hili hekalu nami nitalijenga ndani ya siku tatu. Yesu Kristo awasaidie wakatoliki wasiwe na mikono ya birika katika kuchangia ujenzi wa hekalu la Bwana ili likamilike ndani ya siku tatu!
Yesu Kristo na wafuasi wake wa kweli hawaogopi kuvunjwa kwa hekalu kwa kuwa UPO UWEZO WA KULIJENGA TENA NDANI YA SIKU TATU!
Ref haya maandiko: Yesu atoa kibali cha kuvunjwa kwa hekalu.
Yoh 2:19 Yesu akajibu akawambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha!
 
Mungu Akusamehe kwani hujui uyasemayo. Nyumba ya Ibada ni sehemu Takatifu, imewekwa Wakfu! Usijisifu kuwa wewe ni Mlutheri, usisikie uchungu Kanisa la Katoliki au Misikiti inapodhalilishwa na kubomolewa. Kumbuka Ukuu wa Mungu, hatustahili hata kulitaja Jina Lake! Kama kweli unamjua Mungu Aliyeumba vyote jifikirie uombe Toba! Kabla hujarusha madongo kwangu, hata mimi pia ni Mlutheri! Lakini kwangu mimi Mungu Ni Pendo!
Mkuu usishangae ila ogopa kuwa hapa ndio tulipofikia kama nchi. Kwamba mwenzake anapoumizwa na ila yuko salama anafurahia

Ila kitu nachojiuliza hapa tumefika lini
 
Afadhali Wakatoliki nao wapate kibarua cha kujenga makanisa. Tangu Muitaly awaachie majengo wamebweteka, sisi Walutheri ambao hatukurithi chochote tumejipiga piga weee hadi sasa tuna majengo makali kuliko Roman Catoliki ambalo kiuhalisia ndio kanisa kubwa.
Sie KKKT tumeshazoea kujenga, hatushtushwi na bomoa bomoa. Hata wakibomoa makanisa yote, tutachangishana tena tuanze moja... Kujenga ndio imekuwa kama hobby yetu kwa sasa. Kazi kwao hao ambao wamezoea vya kupewa...
Una matatizo somewhere. U can easily start an arguement in an empty room!
 
Kwa hili Magufuli ,Lukuvi na serikali yao hawanasalama,vilio vya wanyonge na waliobomolewa makazi yao kwa amri zao,na kisha Nyumba za ibada, na baadae Makaburi,Lazima Laana iwaandame,na mamlaka yao waliyotunukiwa kama dhamana kwa waja wa Muungu wanavyoyatumia vibaya, HILI HALITOPITA SALAMA,LAZIMA MUUBA ATAONESHA UKUU WAKE
 
Hii ni Nyumba ya baba yangu Makondeko kaishi hapa kwa miaka 40 had I Leo,hata hiyo Tanrod haikuwepo,hiyo mipaka ya Barabara imemkuta akiwapo kwa miaka 33
 
Hii ni Nyumba ya baba yangu Makondeko kaishi hapa kwa miaka 40 had I Leo,hata hiyo Tanrod haikuwepo,hiyo mipaka ya Barabara imemkuta akiwapo kwa miaka 33
Ardhi ni Mali ya serikali na custodian ni Rais wa JMT mkuu. Kwa hiyo wanapohitaji ardhi yao kwa matumizi ya aina yoyote serikali Ina Haki ya kuitwaa. Tukeshe tukiomba.
 
Ewe Mola were ndie mfalme wa kweli nawe ndiwe muadilifu,hufunzwi namna ya kuhukumu,lakini tunakuomba ili watawala jeuri watambue uweza wako usiowezwa na kiumbe,Hukumu
 
Niliuliza hivi wabomoaji (mwendesha tingatinga) huwa anakuwa na hali gani akitimiza hui wajibu? Niliambiwa tu anakuwa 'under influence'

Ubomoaji huu katika hali ya kawaida hauwezi kukuacha salama, unaweza kuwa umelala zikakujia picha za akina mama na watoto wakililia nyumba zao!
Ulishawahi kuuliza masahibu ya kazi ya mtu anayenyonga!!!?

kawaida tu ni sehemu ya kazi yao
 
this is sad,

mie nawalaumu hao WAPANGA MJI waliokuwepo zamani,

hawakujua MJI, Unakua??????
 
Back
Top Bottom