Misiba mizito Kanda ya Kaskazini: Hizi taharuki zitatuliweje?

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,017
3,655
Kwa siku za karibuni,tumeshuhudia taharuki katika misiba mikubwa eneo hili. Kumekuwa na mivutano ya Kisiasa,Kivyama, Kiserikali na hata kijamii kuhusu taratibu za maandalizi,mazishi, na hata namna ya kufariji (rambirambi) kwa wahusika. Hili si jambo jema hasa ukizingatia sifa ya nchi yetu ya upendo,amani na mshikamano. Je, nini kifanyike kumaliza taharuki hizi ambazo hazijengi utaifa na ustaarabu tuliouzoea?
 
Siasa tu isitufanye tujaribu mshikamano Wa kitaifa, ni hatari sana Kwa umoja wetu. Kumbe waafrika hatujui siasa, bado tunamentality kuwa kumchukia jirani yako kwasababu ana itikadi tofauti ni kujenga taifa imara.
 
Hilo limesababishwa na siasa za hovyo za baadhi ya viongozi wachache wa serikali ya CCM ambao wanataka kuigeuza misiba kuwa mitaji ya kisiasa.

Kumbuka hiyo hali ya sintofahamu ilianzia Arusha kwenye ule msiba wa msiba wa wale wanafunzi wa St Vincent, ambapo huyo RC Gambo alipoamua kwa makusudi kabisa kuwaengua kabisa kwenye shughuli hiyo ya mazishi, wachaguliwa wa wananchi kwenye jimbo hilo ambao ni Mbunge Godbless Lema pamoja na Meya wa jiji hilo.

Tukija kwa upande wa huko Moshi, huyo huyo Gambo ambaye anasemekana kuwa ndiye aliyekuwa amepewa kukaimu kuongoza mkoa huo, aliamua kuhamisha shughuli ya uagaji wa mwili wa Mzee wetu Ndesamburo toka uwanja wa mashujaa na kuupeleka uwanja wa majengo kwa sababu zisizo za msingi.

Mpasuko wa nchi hii unaoletwa na serikali hii ya awamu ya 5 kwa misingi ya itikadi za kisiasa itakuja kuliangamiza Taifa letu, kama hali hiyo isipothibitiwa haraka iwezekanavyo.
 
Muda ukifika yatajiweka sawa na yatakwisha hayo yote huwezi kuyalazimisha wala kuwalazimisha wanadamu kufuata utamadani fulani.
 
Wengine tulijua haya ndiyo wakubwa walitaka,wakidhani walifanya walichofanya basi watawakomesha wana nchi wa Kilimanjaro.

WanaKilimanjari huwa hatuna ubaguzi wamekuwa wanaccm walipo Moshi na Kilimanjaro kujumuika na wenzao.

Shida unapotumia akili ya Chuki na visasi kudhani utajua Upinzani na utafanya watu waipende CCM.

Wameacha kufuatilia wezi wa madini yetu ambao wengine ni Mawaziri wako busy na kuhakikisha msiba usiende inavyotakiwa kuwa.Sasa baada ya Wanaccm kususia msiba haukufanyika??

Huwa tu nasema usipofika kwenye msiba,marehemu hakutaka ufike kumuaga!Yawezekana kwa sababu ya unafiki wa mtu husika Marehemu hakutaka aende kumuaga just like that.

Poleni wanaccm kwa kuwa na Viongozi wasio na upeo wa Taifa.
 
Kwa siku za karibuni,tumeshuhudia taharuki katika misiba mikubwa eneo hili. Kumekuwa na mivutano ya Kisiasa,Kivyama, Kiserikali na hata kijamii kuhusu taratibu za maandalizi,mazishi, na hata namna ya kufariji (rambirambi) kwa wahusika. Hili si jambo jema hasa ukizingatia sifa ya nchi yetu ya upendo,amani na mshikamano. Je, nini kifanyike kumaliza taharuki hizi ambazo hazijengi utaifa na ustaarabu tuliouzoea?
Acha unafki hamna upendo wala amani wala mshikamano start calling a spade a spade
 
Naona upinzani yaani wa Chadema, ndio wanafaa kujibu haya kwasababu wao wanaopenda kuvuruga kila jambo jema na kwa kujifanya hawaelewi mengi.
Kufiwa ni jambo jema..? Suala la kufiwa halina chama jitahidi kuongea kama binadamu anayetambua uchungu wa kufiwa. ..mnajenga chuki hadi msibani. .!!! Wenye akili timamu hawalivumilii hili suala , wanasubiri siku ya nyinyi kusulubiwa kwa njia yankira ifike na tena watakao wasulubu wengi watatoka hukohuko kwenu.
 
Natamani Mtanzania mmoja aitishe maombi kuombea hawa viongozi wanaotuvuruga ili Mungu atoe mwafaka.

Haiwezekani mimi naletewa rambirambi na nimefiwa mwingine anasema hawa wanaokuja kunifariji hawajafuata taratibu. Unless hawajawahi kufiwa, Mungu anawaona, siku yakiwafika naomba kitokee kitu kitakachowafanya wajifunze uchungu halisi wa kufiwa.
 
Back
Top Bottom