Misiba imekuwa gharama sana

Misiba imekuwa gharama sana

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,011
Huku kwetu zamani kwenye misiba watu walikuwa wanaenda na kuni, mahindi na maharage, mbao zinanunuliwa na watu wanashirikiana na seremala wa karibu jeneza linatengenezwa. Pia sehemu zote ardhi ya kuzikia ilikuwa bure.

Leo bila pilau au wali nyama msima unaonekana 'haujanoga 'na watu hawaji na mchele wala nyama. Gharama karibu zote ni wafiwa. Majeneza bei juu. Sehemu fulani za kuzikia zinauzwa. Na kumezuka tabia ya kukodi magari ya muziki ambayo huwa na mike yakitangaza majonzi barabarani na kupiga nyimbo za huzuni. Mbaya zaidi msiba huja ghafla so hakuna michango kama ya harusi hivyo wafiwa huwa na mzigo mzito.

Nini kimetokea? ubepari, mabadiliko ya kawaida au ndiyo masuala ya showoff?
 
Misiba siku hizi Ina Kamati za Mapambo,muziki,vinywaji na vyakula,sare za wafiwa,MC,Video na Picha,Maturubai na Viti,Jeneza na gari la kubeba mwili ...n.k.
Gharama ya shughuli nzima inaweza kufikia mamilioni ya shilingi.

Ilhali misiba ya zamani ilikuwa ni mikeka,waimba kwaya,majirani kujitolea kupika,maturubai yalikuwa yanatolewa bure,jeneza hutengenezwa kwa gharama nafuu...n.k.
Kupanga ni Kuchagua.
 
Hili suala litaisha tu automatically kwa mwendo huu wa JPM kila goti litapigwa
 
kinachoniumiza ni pale mgonjwa alikosa hela ya matibabu ikapelekea kifo aisee acha tu
na hapo ndipo utaona unafiki wa binadamu pale ndugu wa karibu anajitokeza kusema kuwa chakula cha msiba juu yake lakini kipindi cha ugonjwa hakuchangia hata senti. Binadamu tumepotoka kiasi kwamba thamani ya utu imehamishiwa kwenye ufu. Utachangiwa na kuthaminiwa pale tu utakapokufa na si ukiwa hai.
 
Kupanga ni kuchagua,the best thing ni kwamba hakuna anayekulazimisha kuchagua unachochagua,neno langu hapa ni moja tu...FAHARI NI MAMA WA UJINGA.
Point.... Anguko la wengi ni kutaka kuridhisha mitazamo ya binadamu kusahau ya kuwa anaekusifu kwa ufahari ndie huyo huyo atakaekunanga kwa ufukara.
 
na hapo ndipo utaona unafiki wa binadamu pale ndugu wa karibu anajitokeza kusema kuwa chakula cha msiba juu yake lakini kipindi cha ugonjwa hakuchangia hata senti. Binadamu tumepotoka kiasi kwamba thamani ya utu imehamishiwa kwenye ufu. Utachangiwa na kuthaminiwa pale tu utakapokufa na si ukiwa hai.
inaumiza sana any way ndiyo waliyoyachagua hayo
 
na hapo ndipo utaona unafiki wa binadamu pale ndugu wa karibu anajitokeza kusema kuwa chakula cha msiba juu yake lakini kipindi cha ugonjwa hakuchangia hata senti. Binadamu tumepotoka kiasi kwamba thamani ya utu imehamishiwa kwenye ufu. Utachangiwa na kuthaminiwa pale tu utakapokufa na si ukiwa hai.
pale siyo kwamba wanamthamini sana marehemu, ni njia ya kujjionyesha uwezo na kutafuta sifa.
 
Misiba siku hizi Ina Kamati za Mapambo,muziki,vinywaji na vyakula,sare za wafiwa,MC,Video na Picha,Maturubai na Viti,Jeneza na gari la kubeba mwili ...n.k.
Gharama ya shughuli nzima inaweza kufikia mamilioni ya shilingi.

Ilhali misiba ya zamani ilikuwa ni mikeka,waimba kwaya,majirani kujitolea kupika,maturubai yalikuwa yanatolewa bure,jeneza hutengenezwa kwa gharama nafuu...n.k.
Kupanga ni Kuchagua.

Dunia na maisha kwa ujumla vimebadilika sana. Yale maisha ya kijamaa ya enzi ya Nyerere yanatoweka taratiibu!
 
Back
Top Bottom