Mishahara vipi

Mshuza2

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
11,224
17,079
Nina wadeni wangu wanadai mishahara bado.. Mlioko serikalini je ni kweli? Isije ikawa nadanganywa.. Pasaka nayo hiyooo.
 
Kama upo hapa nyumbani na umepost mambo ya mshahara muda huu (alfajiri yote hii), kweli hali yako ni taabani.
Kaka binafsi ndio narudi hivyo...si unajua pesa hailali.. Wewe ukilala lala tu.. Huu ndio muda wangu wa kurudi nyumbani.. Ofisi yangu ni ya usiku..
 
Mimi mwenyewe bado sijapata sijui Sikukuu itakuwaje???,Duh!!! Mhe.Rais hili nalo ni jipu hadi Alhamis Kuu inaingia yaani patupu Familia itanielewaje jamani???.
 
Mambo ya uhakiki yanazingua ......huenda mshahara ukatolewa week ijayo yaani baada ya pasaka maana raisi keshatoa agizo kua ole wao watakaolipa wafanyakazi hewa na kazi watakua hawana hivyo wakurugenzi na wakuu wa wilaya wapo kwenye hofu kubwa ya kuhofia kufukuzwa kazi Kwa kulipa watumishi hewa ....haya ni maajabu sana ni jambo Jema lakini lilipAswa lifanyike Kwa utaratibu unaoeleweka.watu wachache wanawakosesha Amani ya roho wengine Kwa uzembe wa wachache .haya ndo Matokeo ya kukurupuka.
 
Watu hoi...Magu kaamua maana hata wale wa wazee wa mitutu wanaolipwaga tar 19 hadi Leo patupu kwa mwezi huu.
 
Bado wanasema kuweni na subira kwa kuwa HAZINA hawajalipa hela yoyote tokea JPM aongee na BOT.Nasikia hata mshahara unaweza kuchelewa sana
 
Back
Top Bottom