Mishahara serikalini!!

Uongo mkubwa afya cheti 327000 doploma 537000 acha kudanganya watu bwana fanya utafti kabla ya kuleta humu!

Data zipo wazi na huo ndio ukweli.yakupasa utambue kwamba hakuna waraka mmoja unao fafanua mishahara ya watumishi wa umma.kila idara na waraka wake.nadhani lengo la serikali ni wagawe uwatawale(devide and rule).
 
Mbele na Nyumba mwalimu anayefundisha Maarifa na Maadili husahauliwa na wananfunzi wake ambao wanabadilika kuwa ma FISADI kwa mishahara minono.
 
Jambo hili unalolizungumzia haliko sahihi sana mimi nina marafiki zangu zaidi ya watano ambao tulimaliza wote Kidato cha Nne mwaka 1991 na walipata wote Divisio II tena kuanzia pointi 18 lakini walipelekwa kusomea Ualimu,si sawasawa kusema walimu ni "failures" ni matusi kwao! Ni mfumo tu mbaya wa mipangilio ya Mishahara unaowafanya Waalimu waonekane kama wamedharauliwa,ingawa athali zao Waalimu tunaziona kila siku pale watoto wetu wanaposhindwa kujieleza ama kujiamini hata pale unapowauliza swali dogo tu!
 
Kiukwel namna walim wanavyopatkana, halafu kwa jinsi walvyokuwa weng cdhan kama mshahara unaweza kupanda zaid ya hapo hzo kada nyngne wanazalipwa vzr bse wako wachache sasa ukchukua ratio ya mishara ya category nyng haiwez kuendana na ualmu
 
Walimu tushachukuliwa kama ma makondoo tu,tuamke tuachana na akina Mkoba na CWT.Ila 2015 walimu tuchukue hatua!
 
acha kudanganya umma...katafute takwimu sahihi hazina au utumishi.

Weka hizo takwimu zako unazohisi ni sahihi tuzione.


Bandugu, tuache kukashfiana na kusimangana. Kuna mahali nimepata document nzima ya Government ssalary scales, ambapo serikali iliajiri consultant ili kupitia viwango hivyo vya mishahara na kuviboresha.
Nimeambatanisha picha za sehemu ya hiyo document. Kazi hiyo ilifanywa na Crown Management Consultants Limited waliopo Masaki Dar.. Naomba wataalamu wa utumishi wa umma mtufafanulie hizo Government Scales zinaendana na kiwango gani cha elimu?



Kama picha hazitaonekana vizuri naomba u click.
 
Ukiangalia majedwali hapo juu (kwa mfano hilo la tatu), kwenye executive agencies, unaweza kuona tofauti ya kima cha juu cha mtumishi aliye Tanroads dhidi ya yule wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na yule wa Idara ya Taifa ya Takwimu (NBS). Sasa ujiulize, huyo muhudumu wa masjala wa NBS (NBS Scale 1) kama anaishi mjini anaishije kwa sihilingi 167,100/- kwa mwezi?
 
kuna zile calculations za miaka ya degree (credit hours). Pia Worldwide kuna kitu kinaitwa 'rere proffession' kama vile udaktari, uhandisi na sheria. it is unfair unapotaka graduate wa BSc. Horticulture alipwe sawa na BSc. Electric Engineering. BTW, madaraja yalianzia mbingumi ambapo Biblia inasema kuna malaika wanang'aa kama jua na wengine wanang'aa kama vibatari.
 

Ndugu huyo FB! wako nadhani ipo siku atakulisha sumu hivyo chukua tahadhali mapema ya kutembea na maziwa au mavi ya ngombe ili ikifika hapo unywe mapema?? na mbaya zaidi ni kwa walimu wenzangu watuhumiwa wa hili kuendelea kuamini data feki hizi na kuanza kulaani kwa gap kubwa bila tafiti yoyote !! kumbuka politicians wameamua kututumia sie kama ngazi zao na kwa idadi wanaamini wakifanikiwa kutuchonganisha na mfumo watakuwa wametupata, tumuombe mleta mada atupe supporting document!!!!!
 
wasalaam!
kuna tofauti kubwa mishahara katika watumishi serikalini na pensheni pia kutokana na vigezo vifuatavyo
tuki consider other factors remain constant km muda wa utumishi serikali ,vifuatavyo vinachangia katika kupishana mishahara
1.muda uliotumia kusoma mfano diploma wa miaka 3 mshahara wake ni mdogo kuliko diploma wa miaka miwili au degree ya miaka 3 inatofautiana na degree ya miaka 4 au 5 au 6.(ualimu,mipango miji,udaktari mifugo,udakari kinywa,urubani ndege vita nk)
2.cirular wakati unaajiliwa(sheria iliyoanzisha ajila yako,Acts ,gvt notes,order,n.k zilizoanzisha carder yako)
3.aina ya uajili(operational,recruitment ,apointment nk)
5.sheria zilizoanzisha ajira yako(mfano wakala wa serikali;taasissi,mamlaka,)
nawasilisha
 
Sasa hao wanaoscore highly hapa tanzania si wanafundishwa na hao wa div. 4. Acha kashifa kuna vigezo vya kujiunga na vyuo husika sidhan kama wanajichagua vizuri ni wajibu wa Serikali kuweka vigezo stahiki kujiunga na vyuo mbalimbali. Hata kama mtu kapata div. 0 bado anatakiwa kupata haki yake ya msingi kutoka serikalini aandaliwe mazingira mazuri ya kukabili maisha. Ndugu yangu mishahara ya watu waliopata hzo wani wakiwa BOT au TRA mishahara ni tofauti na waliojikaza wakapata wani na kujikita katika fani za ELIMU NA AFYA hapo ndipo shida ilipo kwamba mgawanyo wa keki ya taifa hainufaishi wananchi kwa usawa hubagua na hapo ndipo shida ilipo.
 
Kiukwel namna walim wanavyopatkana, halafu kwa jinsi walvyokuwa weng cdhan kama mshahara unaweza kupanda zaid ya hapo hzo kada nyngne wanazalipwa vzr bse wako wachache sasa ukchukua ratio ya mishara ya category nyng haiwez kuendana na ualmu

Hivi hizo nchi nyingine ambazo waalimu wanalipwa vizuri kishinda hapa Tz wapo wachache!
 
Data zipo wazi na huo ndio ukweli.yakupasa utambue kwamba hakuna waraka mmoja unao fafanua mishahara ya watumishi wa umma.kila idara na waraka wake.nadhani lengo la serikali ni wagawe uwatawale(devide and rule).
Mshahara Afya cheti ni TGSH A1 diploma TGSHB1 sasa kaangalie hiyo mishahara kama inalingana na pesa ulizoandika
 
Weka hizo takwimu zako unazohisi ni sahihi tuzione.

Watanzania mbona wavivu sana. Mwenyewe umeandika hivi: ".....nimeikuta hii kwenye post ya jamaa yangu fb!" Swali ni kwamba hivi jamaa yako ndio chanzo kizuri sana cha habari.

Ndio maana post #2 (Dotowangu) kakujibu hivi: "acha kudanganya umma...katafute takwimu sahihi hazina au utumishi" Maana Hazina na Utumishi ndio utapata mishahara halisi ya hao uwatakao, ndipo utakuwa na fursa ya kuandika. Vinginevyo subiri.
 
  • Hii habari ni yakweli kabisa angalia kwny hii attachment ya salary scale mpya. Pia nakumbuka uzuri yakua kuna mdau aliitupiaga hapa JF.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…