Mishahara serikalini kulipwa dirishani

I don't believe that they mean what they say,I guess there must be something which is behind the agenda! Siamini kama hiyo ndo trully a solution!!!
 
Wazo kwa wafanyakazi.GOMENI KUCHUKUA HIZO PESA
 


Mkuu mke wangu yuko njiani toka Arusha masomoni kuja Dar kwa ajili ya hako kaposho. Ina bidi akifika aende kwa mwajili akasign kitambulisho baada ya kutoa picha yake halafu aende mnazi mmoja dirishani.
Mlango wa wizi uko hapo penye kupata kitambulisho. Wale watumishi feki wanaweza pia kuwasilisha hizo picha kwa kushirikiana na direct supervisors wao. Suala la utumishi feki sio suala la mtu mmoja. Linahusisha watu zaidi ya wawili.
 
Tusipende kulaamu tu. Sasa wewe system ipi ya kutambua mtumishi hewa bila kuiambia?
Hawa kweli amnazo mbona kuna very cheap and easy IT system ya kubaini watumishi hewa,hivi Serikali aina watu wa IT wakawashauri haya majua?
Masikini Tanzania

Tu
 

Ukiona hivyo ujue serikali imefilisika, huyo waziri asitudangaye, huu sio wakati wa Nyerere ambapo ni yeye tu aliyejua kila kitu. Serikali sasa inatumia mfumo wa maisha ya masikini wa hand to mouth!!
 
Naona kama sio njia mwafaka ya utatuzi wa tatizo, lakini labda ni miongoni mwa njia za kufaya utafiti wa kuzuia wanyakazi hewa. Sababu ya kwanza ni kwamba hao wanaoitwa wafanya kazi hewa hawajilipi mishahara wenyewe, bali wanalipwa na hao hao walioko katika mfumo wa kuandaa na kulipa mishahara; pili kuna wafanya kazi walioko vyuoni ndani na nje ya nchi ambao kisheria wanalipwa mishahara sasa watalipwaji hao kupitia dirishani? Tatu, ni kwa watumishi kupewa pesa mkononi anaweza kuvamiwa na kuibiwa hata kama atapewa cheque, bado atapoteza muda wa utumishi kwenda kupanga foleni benki.
 
I agree wit u 100%.... where r we going wit these kinda people...! Ni Ghasia tupu hii
 

Hapa ndipo huwa nachoka kweli na serikali hii. Yaani sijui sometimes maamuzi haya huwa wanayatoa wapi. Hivi kama wanaochonga dili hizi ni wahasibu je hawaoni kuwa upuuzi huu wa kulipia madirishani ni mchezo wa kiwendawazimu?. Kama wahasibu na watendaji wameweza kula dili na banks ili kutoa mishahara hiyo pindi inapoingizwa kwenye fictitious accounts je wanashindwaje kula dili na watu wa mtaani kuja kupokea pesa hiyo dirishani as employees?.

Hili zoezi la kuwatambua wapokea mishahara hewa siyo la kuota na kuja na idea mfu kama hii. Hivi serikali inashindwa kuzifanyia idara zake na mashirika human audit?. Hata mwanafunzi wa mwaka wa pili wa uhasibu atakwambia jinsi ya kumkamata muongo katika transactions.

Hivi serikali inashindwa vipi kuanzisha database ambayo itakuwa linked katika wizara zote na kutoa ID numbers kwa wafanyakazi wote ambazo zitahusisha uchukuaji wa biometrics zao kama Photo IDs na kuzi update after every two years. Ikulu ingekuwa na kitengo maalum cha ku-deal na hii database na kuwasajili wafanyakazi wote wa serikali katika medical database kama ile ya vizazi na vifo ni corrupt lkama ilivyo sasa, say unawasajili katika database unayoiita hiospital records inayokuwa linked na hospitali kuu za mikoa wanayofanyia kazi na mtu akihamishiwa mkoa wowote anahamishiwa moja kwa moja katika data base ya hospitali ya mkoa huo kutoka central database ya IKULU. kuweka utaratibu kuwa mtu akifariki ndugu hawatapata stahili za marehemu mpaka watakapopata number maalum toka wizara ya afya ambayo namba hiyo itatumwa electronically kwenye data base ya IKULU na sehemu zote zinazohusika kutangaza kifo. IKULU isiwe makazi ya Rais tu tunaweza kupafanya mahali pa uaminifu kwa kuajiri watu wenye integrity waliobobea kwenye fani ya IT kudeal na wizi huu wa majina ya uongo. Yaani wao wakilala wakiamka wanafikiria hilo tu.

Kama wanaweza kufanya hivi katika majeshi kama polisi na JWTZ, kwa kutumia namba zao na ikiwa askari anafariki basi within few hours taarifa zake zinakuwa zimefikia vikosi vyote nchini kwa nini wasitumie utaratibu huu kwa wafanyakazi wa serikali kuu?, au za mitaa?. Kulipa watu dirishani hakutaondoa wafanyakazi hewa bali ni kujidanganya kwa watawala kuwa wamedhibiti hali. Unless wizi huu unawanufaisha viongozi wenyewe, this is not the best way forward. Wizi wa mishahara kwa malipo ya wafanyakazi hewa ulikuwa mkubwa kipindi cha mishahara ya dirishani na mkubwa kipindi cha mishshara ya bank.
 


Hakuna kitu hapo, wezi na watumishi hewa kwa mtindo huu wataendelea kuwepo tu na huenda wakaongezeka. Waziri anawaamini vipi hao wanaolipa watumishi kupitia dirishani? Maana hata kipindi cha nyuma watumishi walipokelea pesa dirishani lakini cha kushangaza hata pesa ya marehemu iliendelea kutoka na ilikuwa ikichukuliwa kwa watu kusaini na kuikomba.

Namshauri Ghasia atafute washauri wazuri na sio hao waliomshauri hili la dirishani.
 

hongera mhasibu,nakuona ulivyopangilia madini na vito vya thamani,mipete vidole vyote,...nakushauri uhamie halmashauri ya jiji la mwanza, pale kuna wafanyakazi marehemu wa tangu 2009 bado naona salary slip zao nadhani bado wanalipwa! Njoo utajrike.
 
.......hii ni biashara haramu ya hazina, wasiyeyushe watumishi wao!!!!!!
 
Ni ukata uliowafikisha hapo na hivyo ni visababu tu vya kudanganyia ili wajikopeshe mishahara ya watu.
 
Dah!!! end will justify the meaning...... :juggle:
 
haya mambo yataanza mwezi januari, wakuu
 
Ama kweli tumethubutu, tumewezwa, tunarudi nyuma kwa kasi!
Ndo vizuri wafanyakazi wapate machungu ya kupishana mishahara, wa mbele yako anapewa hela kwenye vahasha ya A4 afu zako zinaelea kwenye wallet. Na hizo za wafanyakazi hewa ziliwe juu kwa juu kama kawa!
 
“Utaratibu wa kuwalipa watumishi madirishani utakuwa wa muda tu, angalau miezi miwili tu. Nia ni tuwatambue, tusiowaona, tutawaondoa kabisa,”

Hiki ni kituko, utadhani Hawa mwenyewe physically atasimamia hilo zoezi hapo dirishani ili aone burungutu la pesa inayobaki. Sasa atajigawa sehemu ngapi? Kama kuna watu watamsaidia kusimamia hilo zoezi si ndio hao hao wamekua wakisimamia mahudhurio ya wafanyakazi kazini - hao ndio wanaowajua wafanyakazi hewa - infact hao ndio wafanyakazi hewa.
Danganya toto, Hawa wala hana mpango ama uwezo wa kutatua tatizo - kubania nafasi watu wengine ukijua fika huna uwezo kutatua matatizo ama kuongoza huu ni ufisadi pia.
 
hii imekaa vyema sana maana kuna watu wengine walishastaafu kuacha kazi au kufariki wajanja wachache wanaendelea kuwapokelea mishahara yao kiulaainiii big up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…