Misafara ya JK kero Morogoro Road

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
1,195
Kwa siku mbili mfululizo, Jumamosi na leo Jumapili JK amekuwa akipita barabara ya Morogoro na msafara wa magari yapatayo 20, na kutusababishiea kero kubwa sisi watumiaji wa barabara hii. Naambiwa huwa anakwenda Chalinze. Hivi huyu Rais hawezi kutulia akafanya kazi za kulijenga hili taifa?
 

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,893
2,000
Haoni faida ya kukaa na watu ambao hawajamchagua ndio maana anaenda kujifariji chalinze walipomchagua kwa kishindo
 

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,578
0
Zile helicopter walizonunua kwa ajili ya kampeni si zinaweza kuwa mbadala wa kwenda Chalinze au mganga kamwambia zinaweza kuanguka?. Maana gharama ya magari 20 inaweza kabisa kutosha gharama ya helicopter moja na serving ikawepo
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522
2,000
Zile helicopter walizonunua kwa ajili ya kampeni si zinaweza kuwa mbadala wa kwenda Chalinze au mganga kamwambia zinaweza kuanguka?. Maana gharama ya magari 20 inaweza kabisa kutosha gharama ya helicopter moja na serving ikawepo
Hizo helikopta za kampeni hazikununuliwa na CCM. Nasikia zilikodishwa na kampuni ya dhahabu Barrick. Labda sasa wamezirudisha Afrika kusini.
 

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,893
2,000
kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa ningekuwa mshauri wake ningemshauri atulie kwa kuwa watu hawampendi, so wanaweza kumfanya chochote ili wapate kufanya tena uchaguzi wa urais
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,523
2,000
Kwa siku mbili mfululizo, Jumamosi na leo Jumapili JK amekuwa akipita barabara ya Morogoro na msafara wa magari yapatayo 20, na kutusababishiea kero kubwa sisi watumiaji wa barabara hii. Naambiwa huwa anakwenda Chalinze. Hivi huyu Rais hawezi kutulia akafanya kazi za kulijenga hili taifa?

Ndo tukome kuchagua Rais Mkwere..usikute hapo anaenda kuna mtoto wa shangazi yake anatolewa /anachezwa ngoma
 

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
1,195
Hata mimi alinikera magari mengi yamejaza wapambe. Ni gharama kiasi gani wanatumia hawa watu kwene msafara mmoja? Kwani lazima magari mengine yasimame?
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,024
2,000
Magari 20 msafara wa Kikwete kwenda Chalinze? what a waste!!

Angalia motorcade ya waziri mkuu wa uingereza: magari maatatu tu ukichanganya na lile la polisi.

 
Last edited by a moderator:

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,598
2,000
wakuu... nadhani suala hapa si kuchagua mkwere... some didnt vote for him na ameshinda.

Labda ni kumshauri kwamba shida tulizo nazo ni nyingi mno asituongezee hizo za kumpisha njiani kwani zinaongeza simanzi na hasira kwa CCM
 

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
751
500
Magari 20 msafara wa Kikwete kwenda Chalinze? what a waste!!

Angalia motorcade ya waziri mkuu wa uingereza: magari maatatu tu ukichanganya na lile la polisi.Kwa hakika imetulia, hembu washikaji waione hiyo na kuwashauri akina mzee OT, kwani si lazima kuwa na magari zaidi ya 3 hapa town ktk msafara. Sasa hao ni nchi ya Dunia ya Kwanza wanamsafara kama huo, sie wa dunia ya tatu tuna misafara mara 15 zaidi, na huyu ni kiongozi mmoja, wakiongozana watano, ndipo utakapo ona mziki wake. Kazi kwelikweli.
 
Last edited by a moderator:

Bob

JF-Expert Member
Sep 10, 2007
289
225
Tunamruhusu kwa sasa atumie Helicopter ya jeshi. Ni amiri jeshi mkuu, nahisi bado hajaamini.
 

Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,857
2,000
Sio utani huyu bwana na mkewe wanakera sana.
Can you imagine hata Salma akienda Chalinze anapita kwa msafara wa magari si chini ya 5 na escort kali ya polisi?
Mimi sikuwahi kumuona Anna Mkapa au Siti Mwinyi akifanya haya anayofanya huyu mama.
 

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,356
1,500
Jamani ni nchi yetu, ni mama yetu mwacheni apewe anachostahiki, 5yrs tumtarajie mwingine
 

ifolako

Member
Nov 8, 2010
98
0
Na wewe chukua la kwako uendeshe mbona mwenzio Gwajima ana msafara kushinda Mizengo Pinda?Wivu tuu umekujaa!
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,528
2,000
kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa ningekuwa mshauri wake ningemshauri atulie kwa kuwa watu hawampendi, so wanaweza kumfanya chochote ili wapate kufanya tena uchaguzi wa urais

ana ulinzi usioonekana aliowekewa na sh.yahya hamunfanyi chochote ngo,labda musubiri sh.yahya afe.
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
Jamani ameingia tumwache afanye kazi yake sasa! Tusikae na kulalamika tuuu! :tape::tape::tape::tape::tape::tape:
 

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
0
Jumamosi (13 Nov) nilipishana nao pale vigwaza, nilishuhudia mbwembwe za msafara huo ? Anyway ni wakati wake, but the convoy looks costly to the nation.
 

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
1,195
Kinachokera zaidi ni kwamba hizi barabara za Dar tayari zina foleni kubwa, sasa trafiki wanapolazimika kusimamisha magari kwa muda mrefu kwa ajili ya misafara isiyo na tija inakuwa kero kubwa sana. Niliongea na trafiki mmoja akanambia hata wao wanaona kero sana kutokana na misafara hii ya kila siku. Huyo trafiki siku hiyo alipaswa kuwa off, akaambiwa aende kazini ili kusubiri msafara wa Rais. Mbaya zaidi trafiki hawa wanalazimishwa kwenda huko barabarani karibu masaa mawili kabla ya msafara kupita, na hulazimika tena kusubiri mpaka arudi kutoka huko alikoenda. Ndio maana wananchi wengi huwa wanasema ovyo sana pale wanapolazimika kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu eti kwa sababu kuna mheshimiwa anapita. Inaudhi sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom