Misaada: To hell with it!!

Kwako mkuu NN,
Ni imani yangu kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu asingependa kuombaomba. Hii inatokea pale tuu inapobidi.

Swali la kwanza ingekuwa kwanini misaada na la pili tunasidiwa nini.

Kwa maoni yangu, Tanzania kwasasa haiwezi kujiendesha bila misaada, hivyo tutafakari Mara mbili tunaposema "to hell with misaada". Kumbuka misaada ikikata basi wanaoumia ni wananchi wa kawaida (kumbuka tunasaidiwa mpaka ARVs).
Hakuna mtu yeyote atakupa misaada bila masharti, hata ww huwezi fanya hivyo. Swali, je, tumeonewa?
 
Arv 's wakisema tunazuia kutupa mtaani itakuwa balaaa

Ova
 
Hivi mikopo yenye riba nayo ni misaada?
Hapa imeongelewa misaada na sio mikopo. Unatumia kichwa kipi kuwaza? Ht hyo mikopo yenye riba, kama n jambo rahis c waende wakajope?
"He who feeds u controls u" OVA
 

Kufunga mkanda - austerity hakujawahi kukuza uchumi, dawa ni kuongeza mapato. Nikupe mfano hapo nyumbani kwako ukijinyima bia na kula nyama kwa mwaka mzima kutaongeza income? jibu ni hapana kwa kuwa matumizi yanaongezeka kila siku watoto waliokuwa shule ya msingi wanaenda sekondari, waliokuwa sekondari wanaenda vyuo, wazee wako wanazidi kuugua na kuzeeka. So you find at the end of the day austerity measures don't grow the economy of any country.
 
Misaada inalemezana sana... na haswa hiyo misaada ikiwa ina masharti magumu...

Tukizoea misaada, mwisho wa siku tunaona kama vile ni haki yetu kupewa, ikifikia hapo, anayetupa anatufanya anachotaka...


Cc: mahondaw
 
Ndo maana nasema kwamba ‘tunaweza’.

Tatizo tu ndo sijui ni nini hasa...hatujiamini? Hatuna ubunifu? Hatuna akili?

What is lacking in us?

Watoa misaada wamelazimisha akili zetu zione mambo katika huo muktadha.

Sio mashirika yanayojiita ya maendeleo wala ya misaada yanatusaidia kiuhalisia, wanatengeneza mazingira waonekane wanatusaidia lakini kimsingi kazi wanayoifanya hata wenyewe hawawezi kujivunia nje ya miripoti za mikaratasi mingi.

Wanabadili mikao tu, mara MDG sasa hivi sijui SDGs, zote hizo tusitegemee zitaleta tija.

Nimewahi kuuliza, kama wao wamekua kwa miongo mingi Afrika wakisaidia kupambana na umaskini na kutusaidia, mbona hakuna hata nchi moja wanaweza kuitolea mfano kwam a waliisaidia na sasa iko vizuri haihitaji msaada? Umaskini unaongezeka, vurugu kila siku, demokrasia inafifia, utawala bora unazorota...inamaana wameshindwa kufanya wanachosema wanakifanya.

Kocha mwenyewe asipoleta vikombe na ushindi watu wanamtimua.

Hii misaada inaweza kuwa inasaidia( sina uhakika). Lakini imekuuzwa mno kuliko uhalisia.
 
Afrika tunakosa uongozi na usimamizi wa mambo. Hilo ndio tatizo kubwa.

Hayo mambo yakikaa vizuri hautasikia ufisadi, wala upotevu wa rasirimali zetu kizembekizembe.

Tutatumia vizuri tulichonacho, tutakaa kutafakari na kupanga, aina gani ya misaada tunahitaji na ipi hatuhitaji, nambo yapi tufanye na yapi tusifanye. Tutawajenga wananchi wetu kujitambua na kuelewa tunaelekea wapi.

Tatizo letu sio misaada.
 
Hata ukiwa na rich people. Shida hata hao rich people wanakuwa na hofu kama hizi nchi zinaleta mikwala. Angalia nchi kama Iran .. Saivi imewekewa vikwazo vya biashara. Yaani ni shida tupu. Kuendelea kwa nchi za Africa na Asia ni Mungu pekee.
 
Tatizo siyo msaada, tatizo ni pale unaposhindwa kuutumia vizuri

MIsaada hii imekuwa ikitolewa kwa miongo mitano sasa na ilikuwa haiendi kule inakokusudiwa.

JPM ameamua hio misaada iwe inaenda huko.

Kwa kuwa watu walikuwa wakiila hiyo misaada, leo hii hawaoni zile fedha maana hazipo.

Licha ya hiio mleta mada amesema jambo la maana sana.

Je, hao wanaotusaidia wao walisaidiwa na nani?
 

Fwatilia Urusi na wenyewe walivyotaka kujenga nchi upya waliwakamata matajiri wakwelpa kodi, hakuna chuki tabia ya wafanya biashara ni wahongaji wakubwa, mfumo uliojengwa ni watoa rushwa na wapokea rushwa, nchi zote zilizoendelea mifumo yao ni makini Sana, lazima kila mtu kujua chanzo chake cha mapato.

Hapa Kwetu tofauti biashara nyingi haziko kwenye mfumo unaeleweka chanzo cha tajiri na utajiri wake viwekwa wazi, hakika tutashuhudia madudu ya kupokea na kutoa rushwa,Taifa na aina hiyo lazima litakuwa na makundi ya watu waliozoe kupata mapato kwa njia za mkato.
 

Urusi siyo mfano bora, Vladimir Putin is a mere dictator, kila mpinzani wake wa kisiasa huwa anapewa msukosuko unjustifiably. Kama una mfano bora mwingine leta.
 
Ni aibu kubwa sana kunyimwa misaada kwa sababu za uhalifu dhidi ya ubinadamu , hii maana yake ni kwamba mnanyimwa misaada kwa vile viongozi wenu ni wakatiri mithili ya wanyama wa mwituni , ni fedheha kubwa sana kwa nchi
Kinachotakiwa ni kutumia dplomasia na sio ubabe. itakuwa ni kosa sana kutumia ubabe ka Mugabe. Wanadiplomasia wasaidia katika hili hakuna haja ya jeuri na ubabe kwa kisingizio cha uzalendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…