Misaada: To hell with it!!

Ndo maana nasema kwamba ‘tunaweza’.

Tatizo tu ndo sijui ni nini hasa...hatujiamini? Hatuna ubunifu? Hatuna akili?

What is lacking in us?
Mimi binafsi siamini kwamba hatua hizi kali ni kwa sababu hasa ya demokrasia na ushoga. mimi nadhani Magufuli kwa namna moja ama nyingine, amevuruga maslahi ya nchi za Magharibi, hasa kwenye madini. hiyo ndiyo namba moja, na ndiyo inawaunganisha hawa jamaa. lakini kwa sababu anavuruga pia Demokrasia, na kwa sababu ana dogo mmoja aitwaye Makonda, ambaye amekanyaga "landmine" ya ushoga, basi hapo ndio kabisaa wamepata rallying point. Kwa hiyo watatushukia kweli kweli.

Sasa kuhusu hoja yako kwamba we can just ignore them, hata mimi ningetamani iwe hivyo, maana siasa yetu si ni ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA? Lakini najua siyo rahisi hivyo. Nyerere mwenyewe, na akili zake zote, na jitihada zake zote, try as he did, hakuweza kufaulu. Nyerere aliwagonga head-on kwa kutaifisha mali zao. alipambana nao kwa udi na uvumba. alihamasisha taifa enzi zile, UBEPARI NI UNYAMA, nk., ugomvi wetu na Kenya, enzi za UNYANG'AU ulikuwa extension ya vita dhidi ya UBEBERU. Lakini by the time Nyerere anatoa speech kule kwa Mandela, alikuwa anajua kwamba huwezi kucheza na hawa jamaa. alimshauri Mandela asitaifishe mali za wazungu. mwenyewe alijifunza kwa makosa. And you know what? hawa jamaa wamedefeat Eastern block yote, sisi wametugaragaza vilivyo. Mchina anafanikiwa kwa sababu anakula nao sahani moja. anajua kula na kipofu. na ndiyo alternative pekee iliyopo kwetu kwa sasa.

Sababu gani hasa hawa jamaa ni wagumu? Kwanza wanatumia sana akili, na pia wanajua kutumia akili zetu kwa faida yao. Watanzania wengi wanafanyakazi na ku-add value kwao, na watanzania hao wanaona kwamba "wameukata". Hawa jamaa Wameanza zamani ku-exploit resources za dunia, wamejijenga sana kuliko wengine kiasi kwamba wako mbali mno na wana nguvu sana. Ukoloni umewasaidia kujitajirisha zaidi, na pia biashara ya utumwa iliyochukua miaka 600, imekuza sana mitaji yao. Wanaimiliki dunia kama ya kwao. yeyote anayetaka hasa kuwa -beat in their own game, sharti aanze taratibu akiwa pamoja nao, otherwise watakufinyanga bila hata kukuangalia usoni. Unakumbuka Nyerere walim-silence kwa kuua zao la katani? wakaja na synthetic fiber. simple. nchi kama zetu tunaotegemea mazao kama korosho, pamba, kahawa, ni rahisi sana kuzivuruga. wakitaka. Jamaa wanamiliki vitu vitatu hasa: Finance, Weapons, na ideology. Ndio maana ukicheza na ideology utakutana nao. unatakiwa kuimba nyimbo kama "utawala bora", "Liberal economy" ambazo wameasisi wao. ukianza kuja na vitu vipya watahakikisha kwamba hufanikiwi. silaha kali kuwa nazo mpaka jamaa wakuruhusu. fedha ndio wao wanamiliki. ukicheza tu wanakumaliza. simple. Tujifunza kula na kipofu. hasira tu hazitatusaidia. Hasira za mkizi...
 
Kuna memba mwenzako huwa anapigania kutoingiliwa desturi na ustaarabu wa Zanzibar/Africa kutokea Calgary alipo na inawezekana alipokuzia wanae
 
Nimesoma uzi wako nikakumbuka maneno ya mama wa Zambia anaeitwa Dambisa Moyo, huyu mama ameandika sana kuhusu hii inayoitwa misaada, tumeipokea for 50 years na bado tuko hapa tulipo, na inasikitisha zaidi pale unapogundua kuwa wanasiasa wakubwa na wanaowania kuwa viongozi ndio wenye haya mawazo mgando, akheir tuteseke sisi vizazi vijavyo vitanufaika
 
Alafu haki za zinazominywa ni zipi na tunalinganishwa na nani? Misri? Rwanda? Aisee mzungu ukitaka akubane gusa interest zake
 
Hakuna cha jiwe wala kokoto, very soon mtakua Kama mfinyanzi tu Dadeeeeeki
 

Ana akili sana huyo mdada.
 

Si upo karibu na jiwe (aka baba ubaya)? Mwambie aachane na misaada na tukomae wenyewe tu. Ikibidi tuwatimue mabalozi wazungu wote bila kujali ni wa nchi au UN.
 
Si upo karibu na jiwe (aka baba ubaya)? Mwambie aachane na misaada na tukomae wenyewe tu. Ikibidi tuwatimue mabalozi wazungu wote bila kujali ni wa nchi au UN.

Hanijui simjui [zaidi ya kumwona kwa tivii].
 
Si upo karibu na jiwe (aka baba ubaya)? Mwambie aachane na misaada na tukomae wenyewe tu. Ikibidi tuwatimue mabalozi wazungu wote bila kujali ni wa nchi au UN.
Huyo mjinga hao wazungu ndio wanamvalisha nepi huko aliko!
 
We
We huoni jinsi tunavyoangamia watu wanakamuliwa kodi haswa mpaka watu wanatamni kukimbia nchi. We bwege kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…