Mirathi kwa watoto nje ya Ndoa

Madikizela

JF-Expert Member
Jul 4, 2009
675
439
MAHAKAMA TANZANIA YASEMA HAKUNA MWANAHARAMU, ILA KUNA WAZAZI HARAMU TU.

Kuna hukumu-rejea ilitolewa tarehe 28/5/2020 na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kupitia Mh. Jaji Mlyambina.

Ni hukumu ya kesi ya mirathi no. 50 ya mwaka 2016 (ina maana kesi ilichukua miaka 4 kwisha).

Ishu ya msingi katika kesi hiyo ni kuna mume wa mtu alifariki bila ya kuacha wosia. Aliacha mke ambaye alikuwa amemuoa kwa ndoa ya kikristo na watoto wa ndoa hiyo, na wengine wa michepuko (nje ya ndoa).

Watoto wa nje ya ndoa wakaweka pingamizi la mirathi maana walikuwa wameenguliwa wasipate kitu na msimamizi wa mirathi hiyo ambaye ni mtoto wa ndoa.

Wakati wa uhai wake, marehemu alikuwa anawasomesha watoto hao (ambapo wengine tayari walikuwa ni watu wazima), vyeti vyao vya kuzaliwa vilikuwa na jina la marehemu kama baba mzazi, na alishawatambulisha kwa mama yake na ndugu zake wengine.

Mahakamani mama na dada wa marehemu walitoa ushahidi kwamba wanawatambua hao watoto kama watoto wa marehemu.

Upande wa wa kwenye ndoa walikataa DNA test kufanyika kupima kama hao ni watoto wa marehemu.

Katika hukumu yake, Mahakama ikatumia sheria zifuatazo:

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa
2. Sheria ya Mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3. Sheria ya Mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa mtoto haki ya "ku-enjoy" mali ya mzazi wake.
4. Mikataba ya kimataifa kuhusu haki za mtoto ambayo Tanzania imeridhia.

Katika majumuisho yake, Mahakama ikasema, "Watoto hawana hatia maana hawachagui kuzaliwa au kwamba watazaliwa wapi. Msemo wa "kitanda hakizai haramu" maana yake ni hakuna watoto haramu. Ila kuna wazazi haramu."

Kwa hiyo mama za watoto wa nje ndoa ndo wakatambuliwa kwamba ni wazazi haramu na hawastahili kurithi mali ya marehemu. Ila watoto wa nje ya ndoa wakaingizwa katika orodha ya warithi, ambayo ilijumuisha na mjane wa marehemu na mama wa marehemu.

Pia ikaonekana mtoto wa ndani ya ndoa kusimamia mirathi hiyo haitakuwa vyema, ikateua Kabidhi Wasii Mkuu (yaani serikali) awe msimamizi.

------------------------------
Kwa kuwa hii ni hukumu-rejea kwa sasa hii ndo tafsiri ya sheria nchini Tanzania, mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo na Mahakama ya Rufaa, au mpaka Bunge litakapotunga sheria tofauti na tafsiri hii ya mahakama.

Je wewe unaonaje? Mahakama iko sahihi, au tuendelee kufuata misimamo ya kidini ambayo inawabagua watoto wa nje ya ndoa na watoto wanaozaliwa kabla ya ndoa?

Hukumu hii inapatikana hapa:

https://tanzlii.org/tz/judgment/hig...me-mwimbe-other-prob-admincause-no50-2016.pdf

Sent from my HUAWEI VNS-L31 using JamiiForums mobile app
 
Sheria za Dini zenye kuleta dhuluma, ubaguzi na ukandamizaji katika jamii hazifai. Pia nchi inaongozwa kwa Sheria za nchi na siyo Sheria za Dini zinazokandamiza baadhi ya watu katika jamii(watoto na Wanawake).

Mahakama ipo sahihi kabisa kwa sababu baada ya kutungwa kwa Sheria ya mtoto ya mwaka 2009, hatuna watoto was nje ya ndoa. Watoto wote ni sawa mbele ya Sheria.

Kadhalika, katika ya JMT inatoa haki ya Kila mtu kumiliki Mali so kwanini tuwanyime watoto kwa sababu ya uroho wa Mali?

Watoto ni malaika, hivyo basi, Wanahaki ya kumiliki Mali ya baba mama yao bila kujali hali zao.
 
Tuzae wisely.

Mtoto hujacheza naye, hajakufulia nguo, hujamtuma dukani, n.k anakuja kugawana sawa na wale waliokunywesha dawa ukiwa mgonjwa, kukufulia, kukupikia, kuzungumza nawe daily, kukuchekesha, kukutoa stress n.k
 
Sheria za dini yetu hazina reform ndugu. Wenyewe tumeridhika nazo.
Elewa basi hzo sheria zitatumika Kama pande husika zimeridhia nakama hazikinzani na sheria za nchi ikiwemo katiba.Zikikinzana na katiba na sheria zinakuwa invalid
 
Elewa basi hzo sheria zitatumika Kama pande husika zimeridhia nakama hazikinzani na sheria za nchi ikiwemo katiba.Zikikinzana na katiba na sheria zinakuwa invalid
Unaongea kwa mihemko! Moja ya sheria zinazotumika kwenye mahakama zetu ni Sheria za Kiislam, na kwa mujibu wa Sheria za Kiislamu, mtoto wa nje ya ndoa sio mrithi halali wa baba, hali kadhalika baba nae hawezi kumrithi mtoto wake endapo anayetangulia kufa ni mtoto; kwahiyo ni double-edged knife.

Hata hivyo, Waislamu wengi huwa wanajaribu kutumia huo mwanya ili kuwatenga hao watoto wa nje ya ndoa na hapo ndipo mahakama inakuwa na wajibu wa kutaka kufahamu maisha ya marehemu kabla ya umauti wake. Je, marehemu kweli alikuwa anaishi kama mwislamu au hawa warithi halali wanataka tu kutumia huo mwanya hata kama marehemu alikuwa mwislamu jina tu!! Mahakama ikiona marehemu alikuwa mwislamu jina tu, itapiga chini sheria ya kiislamu na kutumia secular law itakayowa-include watoto wa nje ya ndoa.

Lakini kwa upande mwingine kama marehemu alikuwa mwislamu kweli kweli ukiacha na hilo lake la uzinzi basi atakuwa ameacha wosia kwa ajili ya watoto wa nje ya ndoa kwa sababu ndivyo dini yao inawataka. Mimi kuna mshikaji wangu alikuwa kwenye hiyo situation. Alizaliwa nje ya ndoa lakini siku baba yake alipofariki, katika kuchunguza makarabrasha ya marehemu, wakakuta kaacha wosia wa nini mwanae huyo wa nje ya ndoa atapewa. Na marehemu akiacha huo wosia, hakuna wa kupinga provided umekidhi masharti ya kiislamu kwenye kuacha wosia, kwa mfano, mali ya wosia isizidi 1/3 na wosia ni kwa ajili ya wale tu ambao hawana haki ya kurithi kwa mujibu wa dini yao.
 
Bahati nzuri sheria zetu za dini zinasema mtoto aliezaliwa nje ya ndoa halali (mwanaharamu) huyo ni mtoto wa mama yake na harithi chochote kwa baba.
Ndo maana nasema hizi dini Ni UPUMBAVU.

Siamini ata Mungu anaweza kufurahia upumbavu Kama huu.

Mtoto Hana hatia,
hakujizaa Wala kushinikiza kuzaliwa.

Yanini ateseke kwa starehe za wazazi wake.
 
Unaongea kwa mihemko! Moja ya sheria zinazotumika kwenye mahakama zetu ni Sheria za Kiislam, na kwa mujibu wa Sheria za Kiislamu, mtoto wa nje ya ndoa sio mrithi halali wa baba, hali kadhalika baba nae hawezi kumrithi mtoto wake endapo anayetangulia kufa ni mtoto; kwahiyo ni double-edged knife.

Hata hivyo, Waislamu wengi huwa wanajaribu kutumia huo mwanya ili kuwatenga hao watoto wa nje ya ndoa na hapo ndipo mahakama inakuwa na wajibu wa kutaka kufahamu maisha ya marehemu kabla ya umauti wake. Je, marehemu kweli alikuwa anaishi kama mwislamu au hawa warithi halali wanataka tu kutumia huo mwanya hata kama marehemu alikuwa mwislamu jina tu!! Mahakama ikiona marehemu alikuwa mwislamu jina tu, itapiga chini sheria ya kiislamu na kutumia secular law itakayowa-include watoto wa nje ya ndoa.

Lakini kwa upande mwingine kama marehemu alikuwa mwislamu kweli kweli ukiacha na hilo lake la uzinzi basi atakuwa ameacha wosia kwa ajili ya watoto wa nje ya ndoa kwa sababu ndivyo dini yao inawataka. Mimi kuna mshikaji wangu alikuwa kwenye hiyo situation. Alizaliwa nje ya ndoa lakini siku baba yake alipofariki, katika kuchunguza makarabrasha ya marehemu, wakakuta kaacha wosia wa nini mwanae huyo wa nje ya ndoa atapewa. Na marehemu akiacha huo wosia, hakuna wa kupinga provided umekidhi masharti ya kiislamu kwenye kuacha wosia, kwa mfano, mali ya wosia isizidi 1/3 na wosia ni kwa ajili ya wale tu ambao hawana haki ya kurithi kwa mujibu wa dini yao.
Wewe nakuacha,ni mbishi.
 
Back
Top Bottom