Miradi ya wanafunzi ICT na Engineering iegemee kwenye kilimo....(agritech innovations)

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Kilimo kinaajiri 70%+ ya watanzania...
Kuna matatizo lukuki kwenye kilimo ukiachana na budget ambayo iliyopita walipata 3% ya walichokiomba ICT na Engineering fields hasa wanafunzi ambao wengi wanauwezo mkubwa waelekeze miradi yao ya mwisho wa mwaka kutatua matatizo kwenye kilimo chetu inawezekana.

Kujua inawezekana tutembelee wavuti /tuvoti za wanafunzi au young researchers Israel wanavyokinyoosha kilimo kwa technologies.

Karibu kwa maoni mzalendo na mpenzi wa kilimo na technology
 
Wazo zuri tatizo uwezeshaji wa serikali nilipokua chuo nilitengeneza site niliyoita kilimochetu ili kufanikisha link kati ya wakulima na wachuuzi,kuna tatizo kubwa sana kwa wakulima kwanza wakosa taarifa sahihi kulima kilimo cha kisasa,cha pili wakulima wengi wanalima mazao bila uhakika wa soko,yaani mtuampata shamba ana mtaji anaingia kulima viyunguu kisa vinalipa sana.

Jambo kubwa serikali inahitaji kuwekeza sana kwenye teknolojia kupitia ICT haswa kwenye kilimo ili wakulima wapate taarifa sahihi za kilimo,masoko kwa wakati sahihi.mkulima akijua bei ya tenga la nyanya sokoni leo hatalanguliwa na dalali...
 
Ni hoja nzur ila uwezeshaji mdogo
Kwenye kufanya projects za mwaka wa mwisho huwa naona wanawezeshwa tatizo ni link Kati ya hizo projects na jamii baada ya kuwa tested na kuonekana zinafanyakazi.
Nadhani nguvu kubwa ni kuwezesha hiyo miradi iwafikie walengwa isibaki kwenye makabati kwenye offisi za maDR na maProfs huko.
 
Ni hoja nzur ila uwezeshaji mdogo
Kweli mwanafunzi anapewa Tsh 300k kukamilisha hiyo Project unategemea itatatua changamoto zaidi ya kuwa Mradi wa mfano tuu.Hata hivyo Mbona Watafiti/Maprofessa wengi wanakuja na tafiti lakini zinaishia kabatini
 
Back
Top Bottom