The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Ufadhili katika miradi ya sanaa (Artistic projects) kwa kiasi kikubwa hukuza utamaduni wa jamii husika na Taifa kwa ujumla.
Hivyo katika ukuzaji wa utamaduni wa jamii husika, taasisi zilizojikita katika uwanda wa sanaa (artistic discipline) hazina budi kuhakikisha zinatafuta fedha kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kufadhili utekelezaji miradi ya sanaa (Artistic Projects)
Ruzuku kwa ajili ya miradi ya sanaa (artistic projects) hutolewa kwa
- Msanii mmoja mmoja (Individual artists)
- Mashirika yanayojishughulisha na sanaa (arts organizations)
Ufadhili kwa Taasisi zinazojishughulisha na sanaa, kwa kiasi kikubwa hujikita katika
- Kuiwezesha taasisi kiutendaji (organization operations)
- Uendelezaji kwa Taasisi (organization development).
- Utekelezaji wa mradi (project assistance)
- Hakikisha programu ya ruzuku inaendana na lengo la mradi wako.
- Hakikisha mradi wako umejikita katika mojawapo ya eneo katika uwanda wa sanaa (artistic discipline); ambayo hujumuisha;( visual arts, dance, music/band, theater/performing arts, writing story, media arts & interdisciplinary arts, etc)
- Hakikisha wazo la mradi wako (project idea) pia limejikita katika uwanda wa sanaa, hivyo mradi wako utapaswa kuhusiana na usafiri (travel), utengenezaji wa kazi za sanaa (creation of new arts), ujengaji wa uwezo (capacity building) n.k
- Zingatia kiwango chako cha uzoefu katika sanaa (level of experience) na chagua ufadhili unaoendana na kiwango chako cha uzoefu. Katika sanaa uzoefu hupimwa kutokana na mafunzo (training) ambayo msanii husika amepitia, pia muda aliotumia katika kuitumikia sanaa (apprenticeship)
The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
Kwa huduma ya;
- Uandishi wa michanganuo ya miradi (socioeconomic, political and artistic project proposals)
- Uandishi wa mipango mkakati (strategic plans) kwa ufanisi wa kampuni/biashara yako.
- Utoaji wa semina katika usimamizi wa miradi na mpango mkakati.
Karibu.