Miradi ya kimkakati ya nishati kuimarishiwa ulinzi

chuchu2020

Member
Jul 18, 2022
5
2
MIRADI YA KIMKAKATI YA NISHATI KUIMARISHIWA ULINZI

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa wamekutana kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuimarisha ulinzi kwenye miradi ya kimkakati inayosimamiwa na Wizara ya Nishati.

Kikao hicho kimefanyika 04 Mei, 2023 Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Faraji Mnyepe, Maafisa kutoka Wizara ya Nishati, Jeshi la Wananchi (JWTZ) pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) .

Waziri Makamba amesema kuwa Wizara ya Nishati inatekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere unaotegemea kuzalisha jumla ya Megawati 2,115.

Ametaja miradi mingine ya kimkakati kuwa ni pamoja na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi (EACOP), Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) wenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 70 pamoja na baadhi ya Miradi ya kusambaza Umeme Vijijini inayotekelezwa na kampuni mbalimbali ikiwemo SUMA JKT Electric Company.

Aidha, Waziri Makamba ameipongeza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa ushirikiano wanaotoa katika kutekeleza na kuimarisha ulinzi kwenye miradi ya kimkakati katika Sekta ya Nishati.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika suala la kuimarisha ulinzi kwenye miradi yote ya kimkakati inayosimamiwa na Wizara ya Nishati.

“Sisi Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa tunawaahidi kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuendelea kulinda na kutekeleza miradi ya kimkakati nchini” amesema Bashungwa.
 
Back
Top Bottom