Miradi ya barabara kibao imekamilika bongo!!!!

Miradi ya barabara kibao imekamilika bongo!!!!

Miradi ya barabara kibao imekamilika bongo

Mrema alisema kuwa miradi minane ambayo imekamilika na inasubiri kufunguliwa na Rais ni Kyamyorwa-Buziyarombo, Mbwemkulu-Mingoyo, Sam Nujoma Road, Daraja la Ruvu, Tarakea-Rongai-Kamwanga, Kidahwe-Uvinza, Kisili-Buhigwe, na Uvinza-Malagasi.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM

Sijaangalia vitu vingine, lakini hiyo ya rangi nyekundu sio ya lami.....au ni mchanganyiko wa lami na changarawe?

Asante Roy kwa kushitukia huo usanii kuhusu hizo barabara, mimi nimeongezea moja ya bluu.

Inaonekana Rais wetu huwa anadanganywa mno na Watendaji wake. Hizo barabara ni mbovu kuliko na zimekuwa hivyo tangu enzi za Adamu na Eva!

Kinachoshangaza zaidi ni kauli kuwa haitajwi ni kiwango cha changarawe au lami ila tunaambiwa zimekamilika. Mimi nadhani ni vema Rais awe mjanja na ajitolee kufunguamwenyewe hizo barabara ili ajionee mauza-uza ya Serikali yake.
 
Binafsi nimeendesha gari kutoka Dar mpaka

Inawezekana wengine wanatazama screen na kupinga tu bila kwenda huko kuona na kudhani CCM itang'oka kirahisi kwa kuchangia na kupiga vita ufisadi kwenye magazeti na mtandao tu! watu waingie chaka na kufukua madudu mengi zaidi na kwenda kwa wananchi ambao achilia mbali computer na magazeti, hata tv hawajawahi kuona. Hao ndio noma kwani wako wengi na ndio silaha ya CCM ukimaliza huko town kwepesi. Town watu hawana imani na rahisi kurubunika.

very true..., ukiwapa vitenge na masweta 't-shirt'... = ushindi wa kishindo as they call!......bado safari ni ndefu.
 
..............Mkuu Ogah, tupo ukurasa mmoja lakini je kumuondoa mkurugenzi mkuu bila kusafisha idara ni tija?? Tukumbuke kuwa kuna idara ndogo nyingi ndani ya TANROADS ambazo zina majukumu tofauti katika kutayarisha, kusimamia na kukagua miradi anuai. Hivyo, lawama kwa Mkurugenzi Mkuu pekee zisiwe kwamba aondoke bali afanye mabadiliko na kuweka watu wenye kumudu majukumu yao kuliko ilivyo sasa.... tusisahau vilevile mambo ya "10%", "political inteference", "who knows who" etc etc etc

.............!!

Morani75,

nina ka-experience kidogo cha mambo ya procurement through financial institutions................mambo aliyoyafanya Mrema kama Mrema tangu aingie TANROADS......kama tunawapeleka akina Mramba and Yona to Court kwa sababu ya kukataa ushauri.....ambapo baadaye nchi imeingia hasara.........basi huyu Mrema ilitakiwa awe wa KWANZA kufikishwa kortini......jamaa ametuingizia hasara kubwa sana na bado....anataka Rais akafungue barabara zilizo substandard......damn!!.......procurements zilizofanywa under Mrema's.........Mramba and Yona case ni cha mtoto!!

Kwanza tangu aingie ameivuruga sana TANROADS.....kwa hiyo Yes....TANROADS yote inabidi kukarabatiwa.......
 
Miradi ya barabara kibao imekamilika bongo
Na Mwandishi Maalum,


Mrema alisema kuwa miradi mikubwa ambayo inasubiri kutiwa saini ili utekelezaji uanze ni Same-Mkumbara, Mkumbara-Korogwe, Kigoma Lusahunga na ujenzi wa barabara za Tanga mjini.

Alisema kuwa miradi iliyoko katika hatua ya manunuzi ni Tabora-Nyahua, Mkata-Handeni, Korogwe-Handeni, Handeni-Mziha, Mwigumbi-Maswa-Bariadi-Lamadi Bariadi-Lamadi, Dodoma-Babati, Sumbawanga-Mpanda, Sumbawnga-Kanazi, Sumbwanga-Mpanda-Kanazi-Kizi-Kibaoni, Kyaka-Kayanga-Bugene, Sumbawanga-Matai-Kasesya, Barabrara za Kuzungumza Mkoa wa Dar es Salaam (ring roads) ambao ni mradi maalum, na Kitumbi, Segera-Tanga.

Mingine ni Tunduma-Laela-Sumbawanga, Tunduma-Kana, Tanga-Horohoro, Songea Mbinda, Songea-Namtumbo ambayo yote itagharimiwa chini ya msaada wa MCC wa Serikali ya Marekani.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Hizi in red si zilikamilika miaka michache tu iliyopita (enzi za Mwinyi/Mkapa)? kulikoni?
 
Hizi in red si zilikamilika miaka michache tu iliyopita (enzi za Mwinyi/Mkapa)? kulikoni?
Mkuu Cynic,
Hizo barabara ni za zamani, kinachofanyika sasa ni ukarakarabati mkubwa (kwa maana zimechoka), pia wanafanya kupanua baadhi ya sehemu ili kuongoza ufanisi wa upitaji wa magari na usalama wa watumia barabara. Kama umepita barabara ya Chalinze Segera siku za karibuni utaona kuna mkandarasi anafanya kazi za aina hiyo.
Kwa mtazammo wangu, dhamira ya serikali katika uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara haina shaka.....

 
Ni kweli kwamba miradi mingi ilianza awamu ya tatu. Na enzi zile za Pombe Magufuri kasi ilikuwa kubwa na miradi mingi ilikuwa iishe 2006. Lakini kutokana na uwezo mdogo na ubabaishaji wa awamu ya nne miradi hiyo wanayoisema imepitiliza kama miiaka miwili sasa. Hiyo haitakiwi kuwa mchumi kuona ni kiasi gani hawa jamaa wametutia hasara kwa kushindwa kumalizia hiyo miradi in time. On top of that kuna miradi ambayo ilitakiwa iishe about two years ago mapka leo haijaisha. Mfano ni barabara ya Dar-Lindi na Dodoma Mwanza. Nasema hivyo kwa kuwa Rais alipotembelea Huku bondeni aliahidi kuwa by the end of 2006 mtu ataweza kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Mwanza mpaka Mtwara. Je hilo limetimizwa?????
Kweli
 
Back
Top Bottom