Mipango ya UKAWA imekuwa mizito sana, Dr Slaa rasmi kesho Jangwani

Status
Not open for further replies.
dr. Amesema mkome kumsemea, kasema muda ukifika ataongea mwenyewe!
Yaani heshima yangu kwa dr. Slaa imeongezeka, huyu mzee ana msimamo na sitegemei kuwa atatokeza kesho! Ukawa sio saizi yake, akajenge nchi na tingatinga!

acha unafki dr. Slaa hajawahi kuondoka cdm. Na kesho atakuwepo
 
Duh huyu Dr naye anaboa yaani Dr mzima anasusa kama kabinti? Aah anajishushia heshima si ajitokeze Tu anaogopa mini?
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa atakuwepo Kesho katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zitakazofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo taarifa zaidi zimeeleza kuwa idadi kubwa ya vigogo wa CCM watajiunga na Ukawa

Moodykabwe umeshakuwa mtu mzima sasa naomba mniache kabisa sijatoa taarifa za kwamba nitakuwapo kwenye uzinduzi huo. wala hatujafanya makubaliano na mtu yeyote kwamba nitahudhuria uzinduzi huo! Mind your business!! Ha ha ha haaaaaaa! Nimeitohoa kama kazee kalivyomwakia Yericko Nyerere siku moja hapa uwanjani!! Sasa Mkuu unatoa taarifa kama nani? Kasipotokea Mkuu tutaaibika sana!!
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa atakuwepo Kesho katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zitakazofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo taarifa zaidi zimeeleza kuwa idadi kubwa ya vigogo wa CCM watajiunga na Ukawa
Mwambie aje na magunia ya OMO ,ndoo za Jiki na brash za chuma kwa ajili ya kumsafisha bwana mkubwa ,kwa kazi ilivyo ngumu itabidi mumuwekee swimming pool pembeni la kuoga akitoka kujaribu kumsafisha asiye safishika,sijui sera mtaeleza muda gani kwani kuna kumsafisha aliye mchafu halafu ndio sera,na hata sera bado hamna ,mbona mwaka huu mnalo.
 
Dr. Slaa alishaandika hapa kwamba yeye akihitaji kuzungumzia lolote atazungumza yeye na kwamba ana mwili wa nyama hivyo anaumizwa na uzushi. Kwamba uzushi wowote ataukanusha fasta. Subiri ushushuliwe kama fulani...
 
Gia za kitoto za kujaza watu.Hamjambo kwa uongo na utapeli.Mnajua hamna kitu kama hicho.Subirini mkitoka kesho tuwaponde na tutumie taarifa hizi mnazopost kuthibitisha mlivyo matapeli wa kisiasa.Kesho si mbali ujue.


Mkumbuke tu kutowaita watu fools,

Mathew 5:22

But I tell you that anyone who is angry with a brother or sister will be subject to judgment. Again, anyone who says to a brother or sister, 'Raca,' is answerable to the court. And anyone who says, 'You fool!' will be in danger of the fire of hell.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa atakuwepo Kesho katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zitakazofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo taarifa zaidi zimeeleza kuwa idadi kubwa ya vigogo wa CCM watajiunga na Ukawa

Join Date : 16th August 2015
Posts : 4
Rep Power : 0
Likes Received:
Likes Given:
4
0
 
Dr Slaa ni mwelevu sana siyo mpumbavu kama mnavyodhani nyiye malofa

Hata jana mlianza kuropoka lowasa kaingia mitini kwenye mkutano wa wanawake lakini baadaye? Haha siasa za mwaka huu za UKAWA hazitabiriki mkuu njoo UKAWA ule raha haha
 
Tunataka Sera, hata aje slaa au nani, tumetosheka na maigizo yenu

Sawa Mkuu tumekusikia njoo usikilize sera,si unaona huko upande wenu,Mgombea analalama na kulaumu Serikali iliyopita haikufanya kitu kabisa japokuwa na yeye alikuwa ni miongoni mwa hao watendaji wakuu😀😀
 
Ccm wameshakubali kabisa kwamba akili ndogo haziwezi kuongoza akili kubwa. Wakae pembeni, akili kubwa UKAWA waongoze nchi ili wajifunze maendeleo ya maneno hayana nafasi kwa Tanzania tena!.

Nenda zako ccm!
 
Kutokuwepo kwa Dk Slaa kumedhihirisha uwepo wa pengo kubwa ndani ya Chadema. Pamoja na kuwepo ukawa lakini uratibu wa Chama kuanzia kura za maoni na kuteua wagombea kumekuwa dhaifu sana.
Tayari udhaifu mkubwa umeanza kujionyesha katika kampeni za ngazi mbalimbali, hususani urais. Na udhaifu huu unachangiwa na Viongozi karibu wote wa kitaifa kugombea ubunge.
Mwanya wa udhaifu huu utatumiwa vilivyo na CCM. Dk Slaa alikuwa Mratibu hodari sana. Mapungufu hayo yanayosababisha baadhi ya wagombea wa udiwani na ubunge kupitia CCM wapite bila kupingwa pengine yasingekuwepo kama angekuwepo Dk Slaa.
Nimeambiwa kuwa Viongozi na wagombea wa ukawa wengi walikuwa wanatarajia kupata ruzuku kutoka kwa Lowasa. Walipoona hakuna kitu kama hicho wameanza kukata tamaa na baadhi yao wanauza majimbo kwa CCM. Na uuzaji wenyewe ni kutokupiga kampeni kwa bidii kwa sababu wanaogopa wakijitoa waziwazi watashughulikiwa na wananchi.
Kama hali itaendelea hivi CCM inaweza kushinda bila kuchakachua kwa sababu ukawa hawafanyi mambo kimkakati. Na sitashangaa wakiishia kuweka mawakala katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.
 
DSC09731.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom