Uchaguzi 2020 Mkakati wa kumg’oa Mwenyekiti Halmashauri ya Siha waiva. Sasa kung’olewa rasmi kesho, vita ya Ubunge yawa sababu

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Mpango wa kumg’oa mkiti wa halmashauri ya Siha waiva,sasa kung’olewa rasmi kesho .

- Vita vya ubunge vyatajwa kama sababu ya kung’olewa

Mwandishi wetu, Siha

Mkakati wa kumvua madaraka Mwenyekiti wa halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro,Godson Ngomuo uliokuwa ukiratibiwa hivi karibuni na baadhi ya vigogo wa serikali sasa umeiva na kesho huenda akavuliwa madaraka.

Mkakati huo ambao ulikuwa ukiratibiwa na Mkuu wa wilaya ya Siha,Onesmo Buswelu,mkurugenzi wake ,Ndaki Stephano,mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghirwa ,mbunge wa jimbo hilo na naibu Waziri wa afya,Dk Godwin Mollel pamoja na baadhi ya madiwani kwa sasa umekamilika na kesho atavuliwa madaraka.

Hatahivyo,tayari mpango huo umeibua mvutano mkubwa ndani ya Ccm wilayani Siha kufuatia uongozi wa chama hicho kutobariki uamuzi huo kwa kuwa unalenga kukigawa chama na kuibua makundi hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

4926F627-41D9-4065-8A6F-8A870F92D66F.jpeg


Taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kikao cha kumpigia kura ya kutokuwa na imani Mwenyekiti huyo kinatarajiwa kuanza majira ya saa nne asubuhi baada ya madiawani 17 kati ya 27 kutia sahihi barua ya kumvua madaraka Ngomuo.

Hatahivyo,baadhi ya madiwani waliotia sahihi wameeleza kulazimishwa na vyombo vya dola kumwaga sahihi zao kwa masharti kwamba asiyetia sahihi atashughulikiwa na hatorudi kwenye nafasi yake.

Itakumbukwa ya kwamba halmashauri ya Siha ni miongoni mwa halmashauri zilizokuwa Chadema kabla ya madiwani zaidi ya 20 pamoja na Mbunge kuhamia Ccm hali iliyopelekea Kuwa chini ya chama tawala.

Taarifa za uhakika kutoka wilayani humo zimeeleza kuwa hatua ya kumvua uenyekiti Ngomuo inasukumwa kisiasa na mbunge wa jimbo hilo Dkt Mollel kwa kuwa Mwenyekiti huyo anatajwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Siha mwaka huu.

Baadhi ya madiwani wanaotajwa kuzunguka na barua hili kupata sahihi za madiwani ni pamoja na Solomon Mmari,Claudia Muro pamoja Witness Riwa ambapo walipewa gari la serikali kutoka halmashauri ili kuzunguka tangu Mei 20 mwaka huu kusaka saini hizo.

Hatahivyo,taarifa hizo zimedai jana Juni 3 mwaka huu Dkt Mollel pamoja na mkuu wa wilaya hiyo ,Buswelu walifika katika ofisi za Ccm wilayani Siha na kukutana na uongozi wake ambapo waliwataka wabariki uamuzi wa kumvua Mwenyekiti huyo.

9A95DC9F-CEDA-4C91-A1F4-1E9D7B69BD90.jpeg


Taarifa zinaeleza uongozi wa wilaya ulikataa kubariki maamuzi hayo huku wakiomba ushahidi wa tuhuma anazokabiliana nazo Ngomuo huku wakidai suala hilo litaibua mpasuko mkubwa hali iliyopeleka Dk Mollel na Buswelu kuondoka kwa hasira.

“Walikuja jana hapa Ccm wilaya kuomba baraka za kamati ya siasa wilaya katika zoezi hilo lakini katibu aliwagomea na kuwaambia wataibua makundi na mpasuko lakini aliwaomba ushahidi wa tuhuma ndipo wakachukia na kuondoka kwa hasira “kilisema chanzo cha habari

Baadhi ya wanachama wa Ccm wilayani humo wamekuwa wakihoji uamuzi huo kipindi hiki huku wengine wakihoji kwamba kumekuwa na uharaka gani wa kumvua madaraka Mwenyekiti huyo kipindi hiki ambapo mabaraza ya halmashauri yanatarajiwa kuvunjwa wiki ijayo.

Hatahivyo,tayari Chama cha kimetajwa kuanza mkakati wa kumshawishi Mwenyekiti huyo ahamie ndani ya chama hicho na apewe nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge wilayani Siha.

Mwisho
 
Chadema kwa kujitungia maneno bana, we are not buying your dramas,, kwendeni zenu huko
 
Mwaka huu magamba yatavurugana balaa! Ni vita ya walionunuliwa vs wenyeji
 
Hakika dhambi ya usaliti haitowaacha katu Lema aliwahi kutamka kwamba mkimaliza kuwashughulikia wapinzani wakiisha mtaanza kushughulikiana nyie kwa nyie Ccm maana upinzani utakuwa umeisha ndio kinachotokea Siha na hili jimbo litaenda Chadema mchana kweupeee maana historia huyu Dkt Mollel alikuwa Ccm alivyokatwa akahamia Chadema akashinda ubunge dhidi ya Agrey Mwanri na sasa kapata mpinzani wake mkiti wa halmashauri na yeye anasubiri tu wakimvua uenyekiti Chadema wanamchukua na kumsimamisha kwenye ubunge hesabu zinakamilika Chadema oyeee hawatumii nguvu kubwa 🤪🤪🤪🤪
 
Waache tu Ila Kama unefanya kaxi ya uhakika utachaguliwa tu uzuri wananchi washajua Mollel aiingia bei
 
Back
Top Bottom