Habari wana MMU?
Naam, mwisho wa mwaka ndio huo na festival season yakaribia.
Huwa napenda kusafiri kipindi hiki, ila kwa sasa naona nimeishiwa plans.
Naomba kwa uzoefu wenu mnipe ushauri wa maeneo ambayo mnaona yanavutia na yatatufaa mimi na laaziz wangu twende kupumzika. Iwe ni ndani ya nchi au nje ya nchi ni sawa.
Natanguliza shukrani kwenu.
.....what exactly are you looking for, maana kupumzika kuna kupumzika "jumla" mfano kule Pwani Mchangani beach resorts Zanzibar...wewe ni kula, kulala na swimming (ukitaka) au,....
Kujipumzisha ukiburudika na NATURE, mfano Game Lodges...(Game Drives)....au,
Kujipumzisha miji mikubwa (Nairobi, Dubai, London, etc) shopping included....au,
Kujipumzisha ukiwa na family & friends, hii yaweza ikawa mnafikia Hotel, lakini mna uwezo wa kuwatembelea 'old flames' 😉
Kuna mbuga za wanyama kusini kama selous, kuna saadani, kaskazini (tarangire, manyara, ngorongoro na serengeti, hii inaweza kuwa round trip). Unaweza pia kwenda ruaha na mikumi. Kama unapenda nature na hali ya hewa iliyotulia kwa kipindi hichi cha joto, unaweza kwenda kupumzika lushoto ama udzungwa (camping is the best).
Kigoma pia kuna nice gombe reserves. Ingia tz tourist board kuna details nyingi za options zilizopo.
asante. Huko nilishaenda, ila na mpenzi wa zamani! Naona tabu kurudia na laaziz sasa!
Napenda zaidi kuexplore natural things na kufurahia uumbaji wa Mungu. Offcourse ndani yake kunakuwa na siku za kupumzika kabiiiisa kama ulivyosema beach, etc.
Ukapumzike kwa kazi gani ya maana uliyolifanyia hili taifa?
mwaga details mwalimu kama una uzoefu na lushoto tutafaidika wengi, sio muanzisha thread tuu......LUSHOTO ndo mpango mzima!kitu sauti za ndege tuuuuuuuuu!