Torero
Senior Member
- Dec 22, 2017
- 122
- 138
- Thread starter
- #21
Katiba ya Zanzibar nayo inampa mamlaka Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar wilaya na Mikoa bila ya kumshauri Mtu yeyoteSheria ya 1992
Na.4 ib.3
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge:
Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.
Tangazo la nchi
yenye Mfumo wa
vyama vingi
Sheria ya 1992
Na.4 ib.5
Kuna kitu umenote kuwa katiba
Ya Zanzibar ni batili?.
P
Ni kweli Eneo lote la Tanzania bara na Zanzibar ndio linalofanya Jamhuri ya Muungano. Kama Umenisoma vizuru hoja yangu ni kuwa eneo la Zanzibar linalopakana na Tanzania bara limeanzia wapi linaishia wapi? Ndio hoja ya Msingi ndugu yangu. Hatuna shida na Eneo lote la Mkoa wa Arusha linaeleweka eneo lote la Manyara pia linaeleweka mipaka yake. Shida ipo hapa Eneo la Zanzibar linaishia wapi au limeanzia wapi kwa sababu Zanzibar imepakana na baadhi ya Mikoa ya Tanzania Bara kwa upande wa Baharini mfano Zanzibar imepakana na Mkoa wa Daresalam, Mkoa wa Pwani , Mkoa wa Tanga Mkoa Lindi na Mtwara na kadhalika sasa hapa tunahitaji kuelewa mipaka ya Zanzibar imeanzia wapi na inaishia wapi ??? Kuna Ramani yoyote inayoonyesha mipaka ya mikoa ya Tanzania Bara iliyopakana na Zanzibar? Kama hamna ni kwa nini ? Wakati mikoa yote mipaka yake iko wazi?