Mioyo ya Watanzania inaumia kwa uchungu mkubwa inaposikia habari za Ubadhirifu wa Fedha za Umma

Rais samia ni msafi na mwenye kuendesha serikali yake kwa uwazi,ndio maana unaona hata ripoti ya CAG ikiweka wazi kila kitu kichofanyika ili kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe kulingana na matendo yake .
Kama ndivyo acha tusubiri utekelezaji ila kama tujuavyo mwakani tena ni hadithi hizi hizi miaka nenda rudi
 
Naamini CCM itatoa maelekezo kwa serikali yao kuwachukia hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji wale wote waliohusika katika ubadhirifu wa pesa za umma.

Imetoa maelekezo mara ngapi na moaka leo serikal haijatekeleza. Next year tutarudi na the same story, wanajuana hawa
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona hisia kalia sana, maumivu makubwa sana, uchungu mkubwa sana wa Watanzania huku mitaani kwangu wanapoendelea kusikia na kufuatilia kile kinachoendelea katika bunge letu pale Dodoma juu ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa, wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi, kukata tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya Watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha na kujineemesha huku nyuma kukiwa na kundi la Watanzania wakiteseka hata kupata tu milo mitatu kwa siku moja.

Wakati tunasikia habari za ubadhirifu huo kuna kundi kubwa la vijana waliomaliza vyuo vikuu hawana ajira mpaka muda huu, hawana mbele wala nyuma, wanashindwa kufanya shughuli za kilimo kwa kuwa hata hela ya mbolea ni shida kwao, wamebaki wanahangaika mitaani kufanya vibarua vya kinyonyaji ili tu wapate chochote cha kukimu maisha yao.

Wapo vijana utawakuta wanabeba cement kwa shilingi mia kwa mfuko mmoja wa kilo 50 ili walipe kodi za nyumba, wapo vijana wanabeba zege licha ya kuwa na vyeti safi katika makabati yao, wapo vijana wanadamka alfajiri kwenda kufanya vibarua vya kulima ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

Sasa iweje mtu aliyepata bahati ya kuajiriwa serikalini na kulipwa mshahara na marupurupu manono na mwenye mtaji wa kutosha ashindwe kuridhika na kipato chake mpaka aanze kuiba? Nani katuroga Watanzania? Kwanini hatuna huruma, aibu wala hofu ya mwenyezi Mungu? Nani atazikwa na pesa? Nani kaburi lake litapambwa kwa pesa?

Unaanzia wapi kutafuna pesa za umma mamilioni kwa mamilioni wakati mpaka sasa kuna wakulima hawaelewi hata watapata wapi pesa za kununulia mbolea? Wakati kuna watu wanakosa hata pesa ya kukata bima ya afya ili wapate matibabu wakiugua? Wakati kuna watoto wa maskini wanashindwa hata kupata uji wa lishe? Wakati kuna watoto yatima wanashindwa hata kununua mavazi na kupata milo mitatu ya chakula iliyo bora?

Inatuma ujumbe gani kwa Watanzania wanyonge na maskini? Inawafundisha nini wanajeshi wanaokesha mipakani wakilinda mipaka ya Taifa letu usiku na mchana huku wakiwa wamesaini kiapo cha kifo kwa ajili ya kupigania, kulinda na kutetea Taifa letu? Inatuma ujumbe gani kwa manesi, wakunga, wauguzi wanaokesha mahospitalini kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu katika mazingira ya kujitoa na kujitolea?

Inatoa ujumbe gani kwa walimu huko Mbozi vijijini waliojitolea kufundisha watoto wa kitanzania? Inatuma ujumbe gani kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira? Inatuma ujumbe gani kwa askari polisi wanaokesha katika giza na mvua usiku kucha wakifanya doria na wakipambana na majambazi hatari kwa ajili ya kuyaangamiza ili Watanzania tuwe salama sisi na mali zetu?

Ni vipi Watanzania wataelewa neno uzalendo? Watatafsiri vipi maana ya uzalendo? Pesa hizo si zingelipa wafanyabiashara na wakulima walioiuzia serikali mahindi yao? Si ingeiwezesha serikali kununua mahindi kutoka kwa mkulima na hivyo kumuokoa na kupata hasara? Si ingejenga miundombinu ya barabara,vituo vya afya, usambazaji wa maji safi na salama?

Si ingetolewa hata kama Ruzuku kwa nishati ya mafuta ili yashuke zaidi na zaidi na hivyo kupunguza hata kiwango cha Nauli na gharama za usafirishaji? Si ingetolewa kama mikopo kwetu vijana tukapata hata hela ya mbolea pamoja na mbegu bora za mahindi?

Hatujasikia watu wakitelekeza wagonjwa mahospitalini? Hatujasikia watu wakishindwa kukomboa miili ya wapendwa wao waliofariki hospitalini kwa kukosa pesa ya kulipia huduma za matibabu japo matibabu hayakuokoa uhai wa wapendwa wao?

Mnafikiri ni kwanini inatokea hivyo kama siyo umaskini wa watu kushindwa gharama za matibabu mpaka kuamua kutekeleza wagonjwa wao? Unafikiri kwanini watu wanashindwa kulipa gharama za matibabu ili wachukue miili ya wapendwa wao?

Jibu ni kwa kuwa ni umaskini ndio unakuwa umechagia hali hiyo. Unakuta familia imeuza kila kitu na kila rasilimali iliyokuwepo nyumbani mpaka kufikia hatua kukosa cha kuuza na hivyo kushindwa na kuishiwa na pumzi ya kuendelea kugharamia huduma za mgonjwa wao.

Kwanini viongozi wetu na wale waliopewa dhamana mnashindwa kutambua haya kwa kuwa waaminifu kwa pesa za umma? Kwanini hamna huruma katika ofisi za umma kwa kuzitendea haki? Kwanini msifanye kazi kwa uzalendo na upendo kwa Eatanzania? Mnajuwa ni kiasi gani tunaumia watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani mnawaumiza na kuwasononesha Watanzania?

Mtu anaiba halafu anaona sawa tu? Sifa tu? Ufahari tu? Hivi mnajua maisha ya Watanzania wanyonge katika kupata milo yao? Mnajua adha za wakulima mashambani? Mnajuwa muda wanaoamka kwenda shambani? Mnajua wengine wanakoswa koswa hadi kung'atwa na nyoka? Mnajuwa wapo vijana wapo tayari kufanya kazi hata kwa elfu tatu kwa siku? Sasa kwanini ninyi hamliziki? Hivi mnaweza kuvaa viatu vya Watanzania wa huku mitaani tukisema tubadilishane viatu? Anayeweza aniambiea.

Kuondoa masikitiko, maumivu, machungu, machozi, kudumisha uzalendo kwa Watanzania ni lazima hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji zichukuliwe haraka sana kwa wale wote waliohusika moja kwa moja au kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Kutokufanya hivyo italeta picha mbaya kwa Watanzania na kuiweka serikali katika wakati mgumu wa kutokuaminika machoni pa Watanzania na kukosa ushirikiano kutoka kwa Watanzania, lakini pia itashusha morali ya kazi kwa watumishi wengine kama vile wanajeshi, manesi, wauguzi, waalimu, nk, wanaofanya kazi kwa uzalendo na kujituma kwa ajili ya Taifa letu.

Tusiwakatishe tamaa Watanzania kwa ajili ya watu wachache walioamua kuwa waroho na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu. Tuwafute machozi Watanzania kwa kuwachukulia hatua hawa wabadhirifu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Leo umeongea mambo ya msingi na maana.

Ukweli nikwamba wanaofanya ubadhilifu wa mali za umma wapo mufumo ,Mtu asiye kwenye mifumo hawezi iba pesa ,kwani anakuwa Hana hiyo access .

Wizi mkubwa unao fanyika na watendaji wa serikali ni wa kalamu , Miradi inaandaliwa budget ya kuijenga na kumaliza ,Lakini ajabu kunatengenezwa hesabu za Uongo na haohao tulio waamini kusimamia miradi na kuchota mapesa watakavyo.

Kwahivo wizi na ufisadi hautaisha kabisa kama katiba mpya hsijapatikana itakayo dhibiti baadhi ya mianya iliopo sasa. Katiba ita wapa nguvu wananchi kuchagua watu makini wanao waamini kusimamia Mali za nchi.

Watu hao watatokana na vyama mbalimbali na wale wasio na vyama ,hii inaitwa uongozi mseto , mwizi akiiba anaonekana na kila mtu na kuchukuliwa hatua haraka.

Kinyume na sasa mwizi anaonekana na hachukuliwi hatua yeyote kwani ni chama kimoja ,na wanaonekana aibu na kuogopana kwani kila mtu anafikiri naye atabanwa kwenye mambo yake.
 
Imetoa maelekezo mara ngapi na moaka leo serikal haijatekeleza. Next year tutarudi na the same story, wanajuana hawa
Uwe na subira tu utaona moto utakaokwenda kuwaka kwa wezi wote na mafisadi. Nafikiri uliona Tayari waziri wa Tamisemi ameshaanza kukunjua makucha kwa wezi na wazembe kwa kuwasimamisha kazi ili wafunguliwe na kujibu mashtaka yanayowakabili.
 
Si kweli, watanzania bado hawajaona uchungu, Tanzania haijapqta uhuru mwaka 2022, ni toka 1961(Tanganyika)

Hizi habari za ufisadi si mpya, kila mwaka taarifa ya CAG inasema kuhusu ufisadi, na watanzania wapo kimya wanafurahia tu.
Serikali huwa inachukua hatua madhubuti kwa wezi wote na ndio sababu watanzania wanaendelea kuwa na imani na serikali yao katika kuwashughulikia wezi na majizi ya pesa zetu.
 
Una uhakika? Kama ndio weka majina hapa ya watu waliochukuliwa hatua, anza na taarifa za CAG
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona hisia kalia sana, maumivu makubwa sana, uchungu mkubwa sana wa Watanzania huku mitaani kwangu wanapoendelea kusikia na kufuatilia kile kinachoendelea katika bunge letu pale Dodoma juu ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa, wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi, kukata tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya Watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha na kujineemesha huku nyuma kukiwa na kundi la Watanzania wakiteseka hata kupata tu milo mitatu kwa siku moja.

Wakati tunasikia habari za ubadhirifu huo kuna kundi kubwa la vijana waliomaliza vyuo vikuu hawana ajira mpaka muda huu, hawana mbele wala nyuma, wanashindwa kufanya shughuli za kilimo kwa kuwa hata hela ya mbolea ni shida kwao, wamebaki wanahangaika mitaani kufanya vibarua vya kinyonyaji ili tu wapate chochote cha kukimu maisha yao.

Wapo vijana utawakuta wanabeba cement kwa shilingi mia kwa mfuko mmoja wa kilo 50 ili walipe kodi za nyumba, wapo vijana wanabeba zege licha ya kuwa na vyeti safi katika makabati yao, wapo vijana wanadamka alfajiri kwenda kufanya vibarua vya kulima ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

Sasa iweje mtu aliyepata bahati ya kuajiriwa serikalini na kulipwa mshahara na marupurupu manono na mwenye mtaji wa kutosha ashindwe kuridhika na kipato chake mpaka aanze kuiba? Nani katuroga Watanzania? Kwanini hatuna huruma, aibu wala hofu ya mwenyezi Mungu? Nani atazikwa na pesa? Nani kaburi lake litapambwa kwa pesa?

Unaanzia wapi kutafuna pesa za umma mamilioni kwa mamilioni wakati mpaka sasa kuna wakulima hawaelewi hata watapata wapi pesa za kununulia mbolea? Wakati kuna watu wanakosa hata pesa ya kukata bima ya afya ili wapate matibabu wakiugua? Wakati kuna watoto wa maskini wanashindwa hata kupata uji wa lishe? Wakati kuna watoto yatima wanashindwa hata kununua mavazi na kupata milo mitatu ya chakula iliyo bora?

Inatuma ujumbe gani kwa Watanzania wanyonge na maskini? Inawafundisha nini wanajeshi wanaokesha mipakani wakilinda mipaka ya Taifa letu usiku na mchana huku wakiwa wamesaini kiapo cha kifo kwa ajili ya kupigania, kulinda na kutetea Taifa letu? Inatuma ujumbe gani kwa manesi, wakunga, wauguzi wanaokesha mahospitalini kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu katika mazingira ya kujitoa na kujitolea?

Inatoa ujumbe gani kwa walimu huko Mbozi vijijini waliojitolea kufundisha watoto wa kitanzania? Inatuma ujumbe gani kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira? Inatuma ujumbe gani kwa askari polisi wanaokesha katika giza na mvua usiku kucha wakifanya doria na wakipambana na majambazi hatari kwa ajili ya kuyaangamiza ili Watanzania tuwe salama sisi na mali zetu?

Ni vipi Watanzania wataelewa neno uzalendo? Watatafsiri vipi maana ya uzalendo? Pesa hizo si zingelipa wafanyabiashara na wakulima walioiuzia serikali mahindi yao? Si ingeiwezesha serikali kununua mahindi kutoka kwa mkulima na hivyo kumuokoa na kupata hasara? Si ingejenga miundombinu ya barabara,vituo vya afya, usambazaji wa maji safi na salama?

Si ingetolewa hata kama Ruzuku kwa nishati ya mafuta ili yashuke zaidi na zaidi na hivyo kupunguza hata kiwango cha Nauli na gharama za usafirishaji? Si ingetolewa kama mikopo kwetu vijana tukapata hata hela ya mbolea pamoja na mbegu bora za mahindi?

Hatujasikia watu wakitelekeza wagonjwa mahospitalini? Hatujasikia watu wakishindwa kukomboa miili ya wapendwa wao waliofariki hospitalini kwa kukosa pesa ya kulipia huduma za matibabu japo matibabu hayakuokoa uhai wa wapendwa wao?

Mnafikiri ni kwanini inatokea hivyo kama siyo umaskini wa watu kushindwa gharama za matibabu mpaka kuamua kutekeleza wagonjwa wao? Unafikiri kwanini watu wanashindwa kulipa gharama za matibabu ili wachukue miili ya wapendwa wao?

Jibu ni kwa kuwa ni umaskini ndio unakuwa umechagia hali hiyo. Unakuta familia imeuza kila kitu na kila rasilimali iliyokuwepo nyumbani mpaka kufikia hatua kukosa cha kuuza na hivyo kushindwa na kuishiwa na pumzi ya kuendelea kugharamia huduma za mgonjwa wao.

Kwanini viongozi wetu na wale waliopewa dhamana mnashindwa kutambua haya kwa kuwa waaminifu kwa pesa za umma? Kwanini hamna huruma katika ofisi za umma kwa kuzitendea haki? Kwanini msifanye kazi kwa uzalendo na upendo kwa Eatanzania? Mnajuwa ni kiasi gani tunaumia watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani mnawaumiza na kuwasononesha Watanzania?

Mtu anaiba halafu anaona sawa tu? Sifa tu? Ufahari tu? Hivi mnajua maisha ya Watanzania wanyonge katika kupata milo yao? Mnajua adha za wakulima mashambani? Mnajuwa muda wanaoamka kwenda shambani? Mnajua wengine wanakoswa koswa hadi kung'atwa na nyoka? Mnajuwa wapo vijana wapo tayari kufanya kazi hata kwa elfu tatu kwa siku? Sasa kwanini ninyi hamliziki? Hivi mnaweza kuvaa viatu vya Watanzania wa huku mitaani tukisema tubadilishane viatu? Anayeweza aniambiea.

Kuondoa masikitiko, maumivu, machungu, machozi, kudumisha uzalendo kwa Watanzania ni lazima hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji zichukuliwe haraka sana kwa wale wote waliohusika moja kwa moja au kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Kutokufanya hivyo italeta picha mbaya kwa Watanzania na kuiweka serikali katika wakati mgumu wa kutokuaminika machoni pa Watanzania na kukosa ushirikiano kutoka kwa Watanzania, lakini pia itashusha morali ya kazi kwa watumishi wengine kama vile wanajeshi, manesi, wauguzi, waalimu, nk, wanaofanya kazi kwa uzalendo na kujituma kwa ajili ya Taifa letu.

Tusiwakatishe tamaa Watanzania kwa ajili ya watu wachache walioamua kuwa waroho na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu. Tuwafute machozi Watanzania kwa kuwachukulia hatua hawa wabadhirifu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Wanaosikia uchungu wamechukua hatua gani. Mmama akisikia uchungu anaenda kujifungua, wewe na uchungu wako umefanya nini
Kwanza tumeruhusiwa kula kwa urefu wa kama zetu, wewe unajua urefu wa kamba yangu?
Watanzania tumejaa unafiki. hata hao wabunge wanaoongea kwa hisia mwisho wa siku utasikia anaunga mkono hoja kwa asilimia mia, unafiki mtupu.
Tafuta fursa upige muamala mambo yasonge
 
Lazima wawajibishwe .mimi siwezi kuwatetea mafisadi wanaotafuna pesa zetu bila huruma wakati sisi tunahenyeka mitaani na maisha mpaka kupata tu hela ya mbolea ni shida.halafu mwingine anashindwa kuwa na huruma na fedha za umma .kwanini mtu asione Mungu kama nafasi ya upendeleo kuwa sehemu ya serikali kati ya mamilioni ya watanzania wenye sifa kama zake? Kwanini mtu apokee mamilioni kama mshahara na marupurupu mengine mengi halafu bado anatuibia nyingine? Inaumiza sana kiukweli na kuleta hasira kali unapoona watu wengine waliopewa dhamana za uongozi wanatafuna pesa kama mchwa huku wengine mkihangaika kwenye vumbi na jua kali kutafuta miamia kwa shida na taabu kubwa..
Wewe ni mnafiki usingekuwa na unafiki ungeacha kumtetea Rais.
Huyo Mama Ndiyo Kiongozi wa Hao Unaowaita Mafisadi.lkn ukifikia kumtaja unakwepa nakumsifia .Hakuna wizi kama Rais atakuwa hausiki au Mmoja wa wanaowaibia wananchi.
 
Rais wetu ni msafi na mzalendo na ndio maana namtetea na nitaendelea kumtetea kwa nguvu zangu zote ,kwa kuwa natambua dhamira yake njema kwa Taifa letu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona hisia kalia sana, maumivu makubwa sana, uchungu mkubwa sana wa Watanzania huku mitaani kwangu wanapoendelea kusikia na kufuatilia kile kinachoendelea katika bunge letu pale Dodoma juu ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa, wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi, kukata tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya Watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha na kujineemesha huku nyuma kukiwa na kundi la Watanzania wakiteseka hata kupata tu milo mitatu kwa siku moja.

Wakati tunasikia habari za ubadhirifu huo kuna kundi kubwa la vijana waliomaliza vyuo vikuu hawana ajira mpaka muda huu, hawana mbele wala nyuma, wanashindwa kufanya shughuli za kilimo kwa kuwa hata hela ya mbolea ni shida kwao, wamebaki wanahangaika mitaani kufanya vibarua vya kinyonyaji ili tu wapate chochote cha kukimu maisha yao.

Wapo vijana utawakuta wanabeba cement kwa shilingi mia kwa mfuko mmoja wa kilo 50 ili walipe kodi za nyumba, wapo vijana wanabeba zege licha ya kuwa na vyeti safi katika makabati yao, wapo vijana wanadamka alfajiri kwenda kufanya vibarua vya kulima ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

Sasa iweje mtu aliyepata bahati ya kuajiriwa serikalini na kulipwa mshahara na marupurupu manono na mwenye mtaji wa kutosha ashindwe kuridhika na kipato chake mpaka aanze kuiba? Nani katuroga Watanzania? Kwanini hatuna huruma, aibu wala hofu ya mwenyezi Mungu? Nani atazikwa na pesa? Nani kaburi lake litapambwa kwa pesa?

Unaanzia wapi kutafuna pesa za umma mamilioni kwa mamilioni wakati mpaka sasa kuna wakulima hawaelewi hata watapata wapi pesa za kununulia mbolea? Wakati kuna watu wanakosa hata pesa ya kukata bima ya afya ili wapate matibabu wakiugua? Wakati kuna watoto wa maskini wanashindwa hata kupata uji wa lishe? Wakati kuna watoto yatima wanashindwa hata kununua mavazi na kupata milo mitatu ya chakula iliyo bora?

Inatuma ujumbe gani kwa Watanzania wanyonge na maskini? Inawafundisha nini wanajeshi wanaokesha mipakani wakilinda mipaka ya Taifa letu usiku na mchana huku wakiwa wamesaini kiapo cha kifo kwa ajili ya kupigania, kulinda na kutetea Taifa letu? Inatuma ujumbe gani kwa manesi, wakunga, wauguzi wanaokesha mahospitalini kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu katika mazingira ya kujitoa na kujitolea?

Inatoa ujumbe gani kwa walimu huko Mbozi vijijini waliojitolea kufundisha watoto wa kitanzania? Inatuma ujumbe gani kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira? Inatuma ujumbe gani kwa askari polisi wanaokesha katika giza na mvua usiku kucha wakifanya doria na wakipambana na majambazi hatari kwa ajili ya kuyaangamiza ili Watanzania tuwe salama sisi na mali zetu?

Ni vipi Watanzania wataelewa neno uzalendo? Watatafsiri vipi maana ya uzalendo? Pesa hizo si zingelipa wafanyabiashara na wakulima walioiuzia serikali mahindi yao? Si ingeiwezesha serikali kununua mahindi kutoka kwa mkulima na hivyo kumuokoa na kupata hasara? Si ingejenga miundombinu ya barabara,vituo vya afya, usambazaji wa maji safi na salama?

Si ingetolewa hata kama Ruzuku kwa nishati ya mafuta ili yashuke zaidi na zaidi na hivyo kupunguza hata kiwango cha Nauli na gharama za usafirishaji? Si ingetolewa kama mikopo kwetu vijana tukapata hata hela ya mbolea pamoja na mbegu bora za mahindi?

Hatujasikia watu wakitelekeza wagonjwa mahospitalini? Hatujasikia watu wakishindwa kukomboa miili ya wapendwa wao waliofariki hospitalini kwa kukosa pesa ya kulipia huduma za matibabu japo matibabu hayakuokoa uhai wa wapendwa wao?

Mnafikiri ni kwanini inatokea hivyo kama siyo umaskini wa watu kushindwa gharama za matibabu mpaka kuamua kutekeleza wagonjwa wao? Unafikiri kwanini watu wanashindwa kulipa gharama za matibabu ili wachukue miili ya wapendwa wao?

Jibu ni kwa kuwa ni umaskini ndio unakuwa umechagia hali hiyo. Unakuta familia imeuza kila kitu na kila rasilimali iliyokuwepo nyumbani mpaka kufikia hatua kukosa cha kuuza na hivyo kushindwa na kuishiwa na pumzi ya kuendelea kugharamia huduma za mgonjwa wao.

Kwanini viongozi wetu na wale waliopewa dhamana mnashindwa kutambua haya kwa kuwa waaminifu kwa pesa za umma? Kwanini hamna huruma katika ofisi za umma kwa kuzitendea haki? Kwanini msifanye kazi kwa uzalendo na upendo kwa Eatanzania? Mnajuwa ni kiasi gani tunaumia watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani mnawaumiza na kuwasononesha Watanzania?

Mtu anaiba halafu anaona sawa tu? Sifa tu? Ufahari tu? Hivi mnajua maisha ya Watanzania wanyonge katika kupata milo yao? Mnajua adha za wakulima mashambani? Mnajuwa muda wanaoamka kwenda shambani? Mnajua wengine wanakoswa koswa hadi kung'atwa na nyoka? Mnajuwa wapo vijana wapo tayari kufanya kazi hata kwa elfu tatu kwa siku? Sasa kwanini ninyi hamliziki? Hivi mnaweza kuvaa viatu vya Watanzania wa huku mitaani tukisema tubadilishane viatu? Anayeweza aniambiea.

Kuondoa masikitiko, maumivu, machungu, machozi, kudumisha uzalendo kwa Watanzania ni lazima hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji zichukuliwe haraka sana kwa wale wote waliohusika moja kwa moja au kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Kutokufanya hivyo italeta picha mbaya kwa Watanzania na kuiweka serikali katika wakati mgumu wa kutokuaminika machoni pa Watanzania na kukosa ushirikiano kutoka kwa Watanzania, lakini pia itashusha morali ya kazi kwa watumishi wengine kama vile wanajeshi, manesi, wauguzi, waalimu, nk, wanaofanya kazi kwa uzalendo na kujituma kwa ajili ya Taifa letu.

Tusiwakatishe tamaa Watanzania kwa ajili ya watu wachache walioamua kuwa waroho na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu. Tuwafute machozi Watanzania kwa kuwachukulia hatua hawa wabadhirifu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

View: https://www.youtube.com/watch?v=qZEvDCvujEI
 
Proverb 29: 18 "Where there is no vision, the people perish: but he that keepeth the law, happy is he."

Mambo haya mambo.....
 
Back
Top Bottom