Mioyo ya Watanzania inaumia kwa uchungu mkubwa inaposikia habari za Ubadhirifu wa Fedha za Umma

Kwa sasa hatua kali zinakwenda kuchukuliwa maana kutokuchukua hatua kutawavunja nguvu na kuwakatisha Tamaa wengi .kutapoteza maana na nguvu ya kuendelea kutamka neno uzalendo hadharani maana wengine watajiona kuwa uzalendo maana yake kuwa fukara na maskini wakati wengine wakijipakulia Minofu iliyonona ,huku wengine wakifa kwa njaa.
images (22).jpeg

Hawa wamechukuliwa hatua gani tangu March 29 report ilipopokelewa?

Au hawaishi Tanzania?
 
Hao wabunge 19 wa CHADEMA walishafungua kesi mahakamani huko kudai haki yao.lazima mahakamani na maamuzi yake yaheshimiwe.kwa hiyo hilo siyo la kuilaumu serikali yetu.
kesi hiyo ni ya kisiasa zaidi kulinda wezi na ndiyo maana haihitimishwi. Haina maslahi kitaifa.suala la ubadhirifu ni complicated,kazi kweli kweli
 
kesi hiyo ni ya kisiasa zaidi kulinda wezi na ndiyo maana haihitimishwi. Haina maslahi kitaifa.suala la ubadhirifu ni complicated,kazi kweli kweli
Mahakama zina utaratibu wa kumaliza kesi kulingana na mwenendo wa kesi husika,kwa hiyo hakuna habari za kuwahi wala kuchelewa mahakama.
 
Kama nimeelewa uzi wako n kwamba mama yako unaempamba hapa jukwaani kila siku ameshindwa kuongoza na kusimamia matumizi ya fedha za umma

Yafaa ang'atuke ili kulinda heshima kidogo ambayo sijui hata kama anayo
 
Hao unaowahita wanakesha kulinda mipaka yetu ndio wanaowakingia kifua wananchi wakitakakuhinyohosha serikali utawahona mitaani wakiwatetea wezi hili sisi wananchi tuendelee kuhibiwa kodi zetu kwa vile wao wanalala bule na kula bule na mishahala wanapata

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Hao unaowahita wanakesha kulinda mipaka yetu ndio wanaowakingia kifua wananchi wakitakakuhinyohosha serikali utawahona mitaani wakiwatetea wezi hili sisi wananchi tuendelee kuhibiwa kodi zetu kwa vile wao wanalala bule na kula bule na mishahala wanapata

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
Watanzania wana imani kubwa sana na Rais wao Dr Samia na Serikali ya CCM juu ya kuchukua hatua kwa wezi wote na wabadhirifu wa fedha za umma. Katika hili wameona kwa nyakati tofauti tofauti namna ambavyo serikali imekuwa ikiwawajibisha watu mbalimbali bila kujali nyadhifa zao imekuwa ikiwafikisha mahakama.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona hisia kalia sana, maumivu makubwa sana, uchungu mkubwa sana wa Watanzania huku mitaani kwangu wanapoendelea kusikia na kufuatilia kile kinachoendelea katika bunge letu pale Dodoma juu ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa, wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi, kukata tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya Watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha na kujineemesha huku nyuma kukiwa na kundi la Watanzania wakiteseka hata kupata tu milo mitatu kwa siku moja.

Wakati tunasikia habari za ubadhirifu huo kuna kundi kubwa la vijana waliomaliza vyuo vikuu hawana ajira mpaka muda huu, hawana mbele wala nyuma, wanashindwa kufanya shughuli za kilimo kwa kuwa hata hela ya mbolea ni shida kwao, wamebaki wanahangaika mitaani kufanya vibarua vya kinyonyaji ili tu wapate chochote cha kukimu maisha yao.

Wapo vijana utawakuta wanabeba cement kwa shilingi mia kwa mfuko mmoja wa kilo 50 ili walipe kodi za nyumba, wapo vijana wanabeba zege licha ya kuwa na vyeti safi katika makabati yao, wapo vijana wanadamka alfajiri kwenda kufanya vibarua vya kulima ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

Sasa iweje mtu aliyepata bahati ya kuajiriwa serikalini na kulipwa mshahara na marupurupu manono na mwenye mtaji wa kutosha ashindwe kuridhika na kipato chake mpaka aanze kuiba? Nani katuroga Watanzania? Kwanini hatuna huruma, aibu wala hofu ya mwenyezi Mungu? Nani atazikwa na pesa? Nani kaburi lake litapambwa kwa pesa?

Unaanzia wapi kutafuna pesa za umma mamilioni kwa mamilioni wakati mpaka sasa kuna wakulima hawaelewi hata watapata wapi pesa za kununulia mbolea? Wakati kuna watu wanakosa hata pesa ya kukata bima ya afya ili wapate matibabu wakiugua? Wakati kuna watoto wa maskini wanashindwa hata kupata uji wa lishe? Wakati kuna watoto yatima wanashindwa hata kununua mavazi na kupata milo mitatu ya chakula iliyo bora?

Inatuma ujumbe gani kwa Watanzania wanyonge na maskini? Inawafundisha nini wanajeshi wanaokesha mipakani wakilinda mipaka ya Taifa letu usiku na mchana huku wakiwa wamesaini kiapo cha kifo kwa ajili ya kupigania, kulinda na kutetea Taifa letu? Inatuma ujumbe gani kwa manesi, wakunga, wauguzi wanaokesha mahospitalini kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu katika mazingira ya kujitoa na kujitolea?

Inatoa ujumbe gani kwa walimu huko Mbozi vijijini waliojitolea kufundisha watoto wa kitanzania? Inatuma ujumbe gani kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira? Inatuma ujumbe gani kwa askari polisi wanaokesha katika giza na mvua usiku kucha wakifanya doria na wakipambana na majambazi hatari kwa ajili ya kuyaangamiza ili Watanzania tuwe salama sisi na mali zetu?

Ni vipi Watanzania wataelewa neno uzalendo? Watatafsiri vipi maana ya uzalendo? Pesa hizo si zingelipa wafanyabiashara na wakulima walioiuzia serikali mahindi yao? Si ingeiwezesha serikali kununua mahindi kutoka kwa mkulima na hivyo kumuokoa na kupata hasara? Si ingejenga miundombinu ya barabara,vituo vya afya, usambazaji wa maji safi na salama?

Si ingetolewa hata kama Ruzuku kwa nishati ya mafuta ili yashuke zaidi na zaidi na hivyo kupunguza hata kiwango cha Nauli na gharama za usafirishaji? Si ingetolewa kama mikopo kwetu vijana tukapata hata hela ya mbolea pamoja na mbegu bora za mahindi?

Hatujasikia watu wakitelekeza wagonjwa mahospitalini? Hatujasikia watu wakishindwa kukomboa miili ya wapendwa wao waliofariki hospitalini kwa kukosa pesa ya kulipia huduma za matibabu japo matibabu hayakuokoa uhai wa wapendwa wao?

Mnafikiri ni kwanini inatokea hivyo kama siyo umaskini wa watu kushindwa gharama za matibabu mpaka kuamua kutekeleza wagonjwa wao? Unafikiri kwanini watu wanashindwa kulipa gharama za matibabu ili wachukue miili ya wapendwa wao?

Jibu ni kwa kuwa ni umaskini ndio unakuwa umechagia hali hiyo. Unakuta familia imeuza kila kitu na kila rasilimali iliyokuwepo nyumbani mpaka kufikia hatua kukosa cha kuuza na hivyo kushindwa na kuishiwa na pumzi ya kuendelea kugharamia huduma za mgonjwa wao.

Kwanini viongozi wetu na wale waliopewa dhamana mnashindwa kutambua haya kwa kuwa waaminifu kwa pesa za umma? Kwanini hamna huruma katika ofisi za umma kwa kuzitendea haki? Kwanini msifanye kazi kwa uzalendo na upendo kwa Eatanzania? Mnajuwa ni kiasi gani tunaumia watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani mnawaumiza na kuwasononesha Watanzania?

Mtu anaiba halafu anaona sawa tu? Sifa tu? Ufahari tu? Hivi mnajua maisha ya Watanzania wanyonge katika kupata milo yao? Mnajua adha za wakulima mashambani? Mnajuwa muda wanaoamka kwenda shambani? Mnajua wengine wanakoswa koswa hadi kung'atwa na nyoka? Mnajuwa wapo vijana wapo tayari kufanya kazi hata kwa elfu tatu kwa siku? Sasa kwanini ninyi hamliziki? Hivi mnaweza kuvaa viatu vya Watanzania wa huku mitaani tukisema tubadilishane viatu? Anayeweza aniambiea.

Kuondoa masikitiko, maumivu, machungu, machozi, kudumisha uzalendo kwa Watanzania ni lazima hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji zichukuliwe haraka sana kwa wale wote waliohusika moja kwa moja au kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Kutokufanya hivyo italeta picha mbaya kwa Watanzania na kuiweka serikali katika wakati mgumu wa kutokuaminika machoni pa Watanzania na kukosa ushirikiano kutoka kwa Watanzania, lakini pia itashusha morali ya kazi kwa watumishi wengine kama vile wanajeshi, manesi, wauguzi, waalimu, nk, wanaofanya kazi kwa uzalendo na kujituma kwa ajili ya Taifa letu.

Tusiwakatishe tamaa Watanzania kwa ajili ya watu wachache walioamua kuwa waroho na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu. Tuwafute machozi Watanzania kwa kuwachukulia hatua hawa wabadhirifu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Watanzania hawa wa simba na yanga na kubet????

Watanzania weng ni marehemu wanaoishi
 
Wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa, wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi, kukata tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya Watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha
Si kweli, watanzania bado hawajaona uchungu, Tanzania haijapata uhuru mwaka 2022, ni toka 1961(Tanganyika)

Hizi habari za ufisadi si mpya, kila mwaka taarifa ya CAG inasema kuhusu ufisadi, na watanzania wapo kimya wanafurahia tu.
 
Back
Top Bottom