Minister of impossibe-PLO Lumumba

french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
3,525
3,649
Juzi na jana nilikuwepo kwenye mkutano wa madini wa kimataifa. Nilibahatika kusikiliza speeches za maprofesa pamoja na wanasiasa lukuki waliokuwepo pale. Prof. Lumumba ni kati ya watoa mada wachache ambao walinivutia.

Uwezo wake wa kuongea bila ya kusoma mahali huku akiwa na uhakika na anachokiongea ni jambo moja zuri sana ambalo watu wote walilipenda. Alisema kuna baadhi za nchi za kiarabu wana miniister of impossible, yaani yale mambo ambayo ni impossible you have to make/turn them possibe. Akasema ikiwezekana na sisi Tanzania tuwe na waziri wa impossibe.

Je itawezekana kwa hapa kwetu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Minister of impossible tunae kinachokosekana ni ministry. Minister si ndio mwenyewe magufuli the bulldoser.
 
..Profesa LUMUMBA yuko KINADHARIA zaidi.

..Ukisikiliza hotuba zake mbili tatu you will figure him out and he becomes very predictable after that.

..Ni sawa na Prof.Kabudi. Hotuba na michango yake mara nyingi huwa ya kujirudia-rudia.

..Kwa mtizamo wangu hatukupaswa kumualika Prof.Lumumba ktk mkutano wa wawekezaji sekta ya madini.

Sina uhakika kama Prof ana uzoefu na utaalamu na uzoefu wa kutosha ktk sekta ya madini.

..Na unaweza kukuta serikali imemlipa Prof.Lumumba kuhudhuria mkutano huo.
 
Shida yetu ni sisi wenyewe wananchi, na haya ndiyo yanayoturudisha nyuma:

1. Tuu wavivu sana.
2. Hatuna msimamo, yetu ni kuropoka tuu bila action, ni rahisi kutumika.
3. Wengi wetu tunapenda vitu ama watu bila kutafakari, kwa nini nafanyi hivi na kwa manufaa gani. Utaona tuna mashabiki wengi wa CCM au Vyama Pinzani, ukiwauliza ni siasa gani ya chama kilichokupendeza ama chenye manufaa kwako, mtu hawezi kukujibu, kwani hajui bali kapenda kelele ama uongo wa mtu fulani.

4. Hatuna maamuzi kabisa. Hapa TZ inaweza tokea scandal ya kuangusha uongozi wa serekali ama chama, tukapiga kelele kwa siku moja au mbili, lakini hatutaweza kugoma wala kuandamana, ili msimamo au uamuzi ubadilishiwe na wahusika. Tunatawalika vizuri tena kwa HYDROLIC STERING WHEEL.

5 . Watanzania tuu waoga zaidi ya kunguru au Mbwa koko. Kwa kelele za mvunguni na matusi ya nguoni, tunachukua OSCAR AWARD, lakini Constable akipiga chafya, tuna mbiyo kumshinda Chui.

6. Tuna wivu sana na tuu Mahasidi wakubwa.

7. Ni wepesi wa kusifia na kuponda.

8. Hatujiamini na Hatuaminiki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Professa wa kubana pua hana jipya.
Hamna jamaa yupo vizuri mno. Mfanao alisema ili kuwabana wawekwzaji kwenye madini nchi za africa lazima tuwe na sheria zinazokaribia kufanana. Hii itasaidia hii itasaidia kwani kampuni haiwezi kusema naacha kuwekeza nchi flan nanatunaenda kkuwekeza nchi nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna jamaa yupo vizuri mno. Mfanao alisema ili kuwabana wawekwzaji kwenye madini nchi za africa lazima tuwe na sheria zinazokaribia kufanana. Hii itasaidia hii itasaidia kwani kampuni haiwezi kusema naacha kuwekeza nchi flan nanatunaenda kkuwekeza nchi nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Kenya ndio maana huwa hawamsikilizi huyo mkomunisti
 
Huyo takataka kazi yake ni kusifia watawala apate mialiko kwenye makongamano kama hayo. Mropokaji tu na hana anachokisimamia
 
Tangu aliposifia uongozi imekuwa tabu.Lazima apate mualiko wa kuunga juhudi mkono.Betraying hopes za watanzania kipindi ambacho demokrasia nchini inapondwa.
 
Waafrika wakisoma sana wanakuwa machizi
Kama huyu jamaa kaanza kutumika kwenye siasa za maji taka za ccm
 
Ni wazo zuri ...lakini Kwa cha hiki cha ccm na uongozi huu sidhani itawezekana
 
Katika Afrika wapo waafrika wenye mawazo au nia ya kuthubutu lakini hawapewi nafasi na watawala.
Mfano mzuri ni Mwl.Nyerere alifunga migodi kwa kisa cha wazawa kukosa ujuzi na Elimu wa kusimamia migodi,pindi tukiweza ndio tuchimbe na kufaidika kama nchi.
Lakini cha ajabu Mkapa aligawia wazungu migodi ya dhahabu kama pipi.Na Kikwete nae akagawa vitalo vya mafuta na gesi wageni kwa kihelehele cha uvascodagama .
Hata yule profesa waziri aliekuwa anategemewa kutukomboa alikumbwa na kashfa nzito alifukuzwa na serikali mbili tofauti kwa mikataba mbovu ya madini na nishati.
Lakini pammoja na makosa makubwa waliofanya watawala na wasaidizi wao sijaona maraisi hao kubezwa au Kufukuzwa kwenye chama tawala,au kunyanganywa ukwasi waliojilimbikiza kinyume,achilia mbali na kushatakiwa.
Sana sana naona mtawala wa sasa akihangaika na wapinzani kuwatia kolokoloni,kuwanyamazisha,kuwazuia kufanya mikutano huku akijua wapinzani hawajawahi kutawala nchi tokea uhuru.
Ni wazi impossible haiwezi kuwa possible kwa nchi kama yetu.
 
Ministry of impossible si ndio kama TISS or MI5 huko kwa mabeberu.

Ebu imagine wenzetu kwenye vita ya pili ya dunia Germany walikuwa na ndege zaidi, askari wengi zaidi na kila resource ya kufanya washinde vita wao.

Isipokuwa MI5 ikaja na impossible plan ya kutafuta kila idea ya msomi ambayo ingeweza wasaidia kushinda vita na kuifanyia kazi.

Ni kwenye vita ndio wakaibuka watu kama ‘Alan Turin’ na enigma machine iliyoweza vunja code za ujerumani na kuwapa advantage kwenye attack zao, kipindi hiki ndio waliibuka watu Robert Watson-Watt na invention za radar zilizowapa advantage ya kujiandaa kwa kujua ndege ngapi zinakuja.

A lot of warfare invention zilitokana na kipindi ambacho the impossible was a mission which ought to be achieved; sio sisi taasisi gani ya usalama imejaza viazi.
 
Back
Top Bottom