Minister Makamba's speech to the diplomatic corp in Tanzania Sep. 21 2023

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,308
24,200
21 September 2023
Dar es Salaam, Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=B6ICkQaKDxU

The Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Hon. January Makamba held a meeting with the members of the diplomatic Corp in TanzaniaHon. Makamba outlined the ministry's priority areas in enhancing bilateral, regional, and international cooperation, and expressed the Government's readiness to collaborate with them for mutual benefit.
Source : mfa_tanzania
 
Kasi ya waziri wa mambo ya nje mh. January Yusuf Makamba

View: https://m.youtube.com/watch?v=qGUOJLeVG3Y

mbali ya kawaida ya makabiliano ya kikazi kidiplomasia kufuata protokali na ruhusa ya ndiyo ya serikali ya Tanzania pia nchi ambazo mabalozi wanaziwakilisha nchini Tanzania, Mh. waziri January Makamba aanza kuiweka wazi na kuifungua wizara hii muhimu kwa diplomasia ya kiuchumi inayoonozwa na maono ya balozi namba moja ambaye ni mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuifungua nchi.
 
Makamba ana kitu, nikiliangalia tabasamu la mzee Mizengo Pinda hapo ( mmoja ya watu ninaowakubali sana), naona kabisa huyu kijana atafika mbali. Pinda mwenyewe amemkubali

Naona style yake balozi namba mbili waziri wa mambo ya nje mheshimiwa January Makamba nchi ya Tanzania itaanza kusikika kimataifa tofauti na mawaziri waliopita.

Tutegemee akauti ya mfa_tanzania YouTube, X Twitter, tanzania foreign blog n.k pia zitajaa taarifa za Tanzania katika lugha ya kimataifa ya kiingereza na kuondoka katika hali ya sasa ambapo ni taabu sana dunia kupata habari za wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ktk lugha hiyo kubwa rasmi ya kimataifa na serikali ktk majukwaa mbalimbali ukilinganisha na Uganda, Kenya, Zambia n.k

Hali ilikuwa safi enzi za waziri Dr. Augustine Mahiga ambapo interview kibao kati ya waziri huyo na media za kimataifa zilijaa na kufuatiliwa duniani kote kutokana na kutambua umuhimu ya lugha ya diplomasia ya kiingereza

TOKA MAKTABA :
Pretoria, Republic of South Africa

Tanzania's minister of foreign affairs Augustine Mahiga at the 37th SADC Summit

View: https://m.youtube.com/watch?v=pTE4TEnzXeg
Source : SABC News
 
21 September 2023
Dar es Salaam, Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=B6ICkQaKDxU

The Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Hon. January Makamba held a meeting with the members of the diplomatic Corp in TanzaniaHon. Makamba outlined the ministry's priority areas in enhancing bilateral, regional, and international cooperation, and expressed the Government's readiness to collaborate with them for mutual benefit.
Source : mfa_tanzania

I must pay attention and listen it carefully and repeatedly because he might cook data and informations as he was doing to other ministries. Only President trust him
 
Naona style yake balozi namba mbili waziri wa mambo ya nje mheshimiwa January Makamba nchi ya Tanzania itaanza kusikika kimataifa tofauti na mawaziri waliopita.

Tutegemee akauti ya mfa_tanzania YouTube, X Twitter, tanzania foreign blog n.k pia zitajaa taarifa za Tanzania katika lugha ya kimataifa ya kiingereza na kuondoka katika hali ya sasa ambapo ni taabu sana dunia kupata habari za wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ktk lugha hiyo kubwa rasmi ya kimataifa na serikali ktk majukwaa mbalimbali ukilinganisha na Uganda, Kenya, Zambia n.k
Wewe huna vinasaba na Makamba?
 
05 October 2023
Dar es Salaam, Tanzania

WAZIRI MAKAMBA AZUNGUMZIA RATIBA YA RAIS SAMIA INDIA , OCTOBER 8 HADI 11 OCTOBER 2023



View: https://m.youtube.com/watch?v=oWJixy8Wugc

5 Oct2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya Kitaifa nchini India kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba 2023 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya India, Mheshimiwa Droupadi Murmu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salam kuwa ziara hiyo inafanyika ikiwa ni miaka minane imepita tangu ziara ya mwisho ya Kiongozi wa Tanzania nchini humo iliyofanywa na Rais wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2015.

Akiongelea umuhimu wa ziara hiyo, Mhe. waziri January Makamba amesema ziara hiyo ni muhimu kutokana na historia iliyopo kati ya Tanzania na India kidiplomasia, kiuchumi, kibiashara, kidini, kiutamaduni na Maisha ya India ambayo yapo nchini Tanzania.

Amesema ziara hiyo ina lenga kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na India na kuongeza kuwa katika ziara hiyo makubaliano ya kushirikiana kupitia sekta za kimkakati kama afya, viwanda, ulinzi na usalama, elimu, teknolojia ya habari na mawasiliano, uchumi wa buluu, maji, kilimo, biashara na uwekezaji pamoja na kutangaza fursa za biashara na uwekezaji za Tanzania ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wa India waje nchini.

Akiongelea faida zinazotarajiwa kupatikana kutokana na ziara hiyo, Mhe. Makamba amesema katika ziara hiyo inatarajiwa kuwa hati mbalimbali za makubaliano MoU zitasainiwa na hivyo kuleta tija katika maeneo ya Mafunzo ambapo Maelfu ya Watanzania watapata nafasi za mafunzo na kujengewa uwezo katika nyanja mbalimbali nhini India na kuongeza kuwa India imeazimia kutoa ufadhili na fursa za mafunzo zaidi ya elfu moja katika fani mbalimbali.

Amesema ziara hiyo itawezesha maendeleo na mapinduzi ya kidijitali na inatarajiwa kuwa India itaanzisha kiwanda cha mitambo ya kuunda bidhaa za kielektroniki na kuanzisha mifumo ya kutumia Akili Tarakilishi AI nchini.

Amesema kuwa ziara hiyo inatarajia kuinua ubora wa huduma za Afya nchini ambapo taasisi ya upandikizaji wa figo na kiwanda cha kutengeneza chanjo za wanyama na binadamu zenye ubora vitaanzishwa, kuwezesha ushirikiano mkubwa kati ya Hospitali zetu na Hospitali za India zinazotoa huduma za afya kwa mifumo ya Tiba Asilia pamoja na kuwezesha upatikanaji wa dawa zenye ubora kwa gharama nafuu.

Akiongelea faida itakazopata sekta ya Kilimo Mhe Waziri Makamba amesema kupata masoko kwa mazao ya kilimo kwa kuwa tunazalisha mbaazi, korosho na mazao mengine ambayo India ni sehemu ya soko pamoja na kuinua na kuongeza biashara ya mazao yanayozalishwa nchini hususan mbaazi, kunde, parachichi na ufuta. “

Tukumbuke kuwa bei ya mbaazi mwaka huu imekuwa kubwa hii ni kwa sababu India wamenunua mbaazi kwa wingi kwahiyo ziara hii itahakikisha soko la mbaazi linakuwa kubwa na linaendelea kuwepo sio msimu huu lipo au msimu ufuatao linakosekana,” alisema Mhe. Waziri.

Amesema ziara hii pia itawezesha uwekezaji wa moja kwa moja kwa kuvutia uwekezaji kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa na kampuni mbalimbali kutoka India; kuimarisha Ulinzi na Usalama katika usafiri wa majini ambapo India inatarajia kuanzisha karakana ya utengenezaji wa vyombo vya majini na ukarabati.

Mhe. waziri January Makamba amesema katika ziara hiyo Mhe. Rais Samia anatarajiwa kufungua Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India litakalowezesha wafanyabiashara na kampuni mbalimbali za nchini kupata fursa za kufanya biashara ya bidhaa zao na uwekezaji nchini India na kushiriki mikutano ya uwili na majadiliano kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara wa India pamoja na kushuhudia ubadilishinaji wa Hati za Makubaliano kati ya Sekta Binafsi za Tanzania na India.

Akiongelea kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na India, Mhe. waziri January Makamba amesema Uhusiano huo uliasisiwa na waasisi wa mataifa hayo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mahatma Gandhi ulitokana na falsafa za viongozi hao ambao walipenda kutafuta suluhu ya amani pasipokuwa na umwagaji damu.

Akiongelea yatakayojiri katika ziara hiyo Mhe. Waziri Makamba amesema Mhe. Rais Samia akiwasili nchini India atapokelewa rasmi tarehe 9 Oktoba, 2023 na Rais wa India, Mhe. Droupadi Murmu ambaye ataambatana na Mhe. Narendra Modi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya India na kufanyiwa sherehe za mapokezi rasmi ambayo yatahusisha gwaride rasmi na kupigiwa mizinga 21.

Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Rais Samia atakuwa na mazungumzo ya faragha na Mhe. Waziri Mkuu Modi na kufuatiwa na mazungumzo ya uwili kati ya ujumbe wa Tanzania na India na watashuhudia ubadilishanaji wa Mikataba na Hati za Makubaliano kati ya Tanzania MoU na India na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea muhtasari wa mazungumzo yao.

Jioni ya siku hiyo tarehe 9 October 2023 Mhe. Rais Samia atazungumza na mwenyeji wake, Rais wa India, Mhe. Droupadi Murmu na kushiriki dhifa ya kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake katika Ikulu ya India.Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
 
Ukishaona maneno MIKATABA na HATI ZA MAKUBALIANO jua tumepigwa kama ilivyokuwa kwenye DP World!.
 
21 September 2023
Dar es Salaam, Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=B6ICkQaKDxU

The Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Hon. January Makamba held a meeting with the members of the diplomatic Corp in TanzaniaHon. Makamba outlined the ministry's priority areas in enhancing bilateral, regional, and international cooperation, and expressed the Government's readiness to collaborate with them for mutual benefit.
Source : mfa_tanzania

Kuongea na vitendo vioane.

Inspiration ni kwenye utekelezaji na siyo utamu wa uongo
 
Back
Top Bottom