Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 37,194
- 85,297
Sasa nimekuelewa sana mkuu.Kitu kingine ambacho wachangiaji mmeshindwa kuelewa ni kuwa, hapa nimelenga uchimbaji mdogo yaani kama wewe hapo unaamua kuwekeza katika uchimbaji locally sasa badala ya kuchimba kwa mazoea ya kubashiri tu hivi sasa nimeshuhudia maeneo ya Bulyanhulu (vijijini) watu wanaungana (wasomi na wajasiriamali) na kuanzisha uchimbaji. Geologist anatafutwa na analipwa lkn anashawishiwa kuwa shareholder ili kuwapa elemu hawa wengine. Mimi nilishiriki kuambatana na Geologist kunionyesha "Mark" za eneo la kuchimba pamoja na hayo namtumia sana kila baada ya kuongeza kimo cha shimo anapeleka samples maabara. Mimi nilikuwa na lengo kuwa badala ya huyo Geologist kuwaza kuajiliwa ni vizuri akaungane na wachimbaji wadogo wenye PLANTS za kuchenjua dhahabu kuanzisha uchimbaji mdogo na baadae atakuja kujikuta ashakuwa mfanyabiashara. Haiwezekani kila anayesoma na kuhitimu awaze tu kuajiriwa
Asante kwa kunipa darasa la local mining