Minara Mipya Vodacom Sh. Mil. 220, si Uongo huu?

buluwaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
207
Reaction score
45
UPDATE: Huyu Mwandishi wa JamiiForum aliyehariri hii post Kenge kweli huyu. Dola Bilion Moja zinageukaje kuwa Shilingi milioni 220? Hawa waandishi wa Tanzania kenge kweli hawa....

habari yenyewe ni hii: Vodacom has invested over $1 billion in the country in building its second and third generation infrastructure coverage during the past few years, the company announced yesterday.

Inakuwaje Shilingi milioni 220/- hiyo? Mimi nilipost 220,000,000,000/- kaja na kichwa chake nazi eti hiyo ni 220 millioni. Hovyooo....


==================================================

Mheshimiwa Magufuli Salaam. Wewe ni mtu wa Kemia. Kwa hiyo hesabu hazikusumbui...

Lakini wewe si mfanyabiashara! Kwa hiyo kuna mambo ya kibiashara naweza kukudokeza.
Mimi nina mashaka na hii taarifa hadi idara ya Kodi itaponipa uhakika kuwa ni sahihi.

Hii minara mipya ambayo Vodacom anasema amejenga ipo wapi? Isiwe namna ya kukuza gharama za uendeshaji kwa gharama za kubuni hapa ili kukwepa kitu... Hebu fanyeni Audit ya hii gharama tuone....Mmmh...nina mashaka sana na hii gharama!


Mabadilikoooo......MAGUFULI!




MAGUFULIIIII...Mabadiliko!

==================================

Chanzo: thecitizen
 

Attachments

  • OTH_7183_1.jpg
    50.4 KB · Views: 5,122
Uchaguzi huu umemkamua lowasa kwa hiyo anatafuta kila namna kufidia hilo gape ,baada ya kugundua kwenye account salio lime yumba
 
Uchaguzi huu umemkamua lowasa kwa hiyo anatafuta kila namna kufidia hilo gape ,baada ya kugundua kwenye account salio lime yumba

Hahahahaaa ungekuwa mwanaume tungesema una tabia za kike, ni kwa vile ww ni mwanamke hatushangai sana:sly:
 
Hawa nao wanapiga sana ni wa kuanza nao tuu
 
Hujui Voda wamepitisha fibre optic cable nchi nzima ndani ya mwaka ihali mamlaka za maji zimeshindwa kuweka vibomba vya plastuc kwa miaka hamsini?
 
Hiyo figure ni ndogo kwa mnara. Huo ni lazima mnara wa 35m sana sana mpaka 50m tena ni wa coverage tu.

Sitashangaa ukiwa ni wa UCAF tena.

TZS 200mil sio nyingi kwa mnara. I know coz I build them.
 
Nijuavyo vodacom hawamilikı tena minara balı wana-outsource huduma za minara toka makampuni mengne(naomba kusahihishwa na mwenye facts zaidi).Na kwa maagizo ya NEMC,minara hiyo itaweza kutumiwa na kampunı zaidı ya moja.
 

Kama zile nguzo mpya za Grid ya taifa za umeme kwa kuanzia tu mifuko isiyopungua 300 inazamishwa chini na hadi nguzo inasimama gharama yake haipungui Million 180 je ukiringanisha huo mnara wa Vodacom wenye kuwekewa vifaa mbali mbali ambavyo hata wewe gharama zake hauzijui je ni halali kwa wewe kushangaa hiyo million 220? tatizo umejikita kwenye mawazo ya kimasikini masikini ndio maana unaona hiki ni kitu cha ajabu.
 
Usichokijua ni kama usiku wa giza. Bei ya vodacom kujenga mnara ni ndogo kuliko mitandao mingine. Kwa taarifa tu ni kwamba minara ya Halotel gharama yake ni milionimia tatu na hiyo unahusisha ujenzi na ununuzi wa vifaa kuhusu gharama za kukodi aridhi hizo ni pesa nyingine. Yan kwa kifupi mkandarasi analipwa milioni mia tatu.
 
watu sim za adroid mnajua kuangalia fb na ngono tu,,,,someni mambo mengine ya msingi,,,hukua na haja ya kuleta mada ya kitoto kama hiyo hapa ,,ww google utapata majibu.....nigekua na uwezo ninegewahamisha tz mkaone dunia ikoje.
 
Mkandarasi tu analipwa over 100 million, mnara prke yake ni over 100 million hadi ifike hapa tz na kulipiwa kodi. Kuna kila dalili gharama inayotumika ni zaidi ya 200million maana bado kuna generator ambalo si chini ya million 30 na power back up ambayo ni zaidi ya 15 million.

Hakuna kilichiobwa hapo ndugu!
 
Mtoa Mada nadhani hawa wamesaidia kukupa jibu;
Mulindi,Yodoki II,J33,Gulf Streamer.

Yodoki II;
Kuna outsourcing ilifanyika ya Minara kwa kampuni ya HTT(owner wa Minara ya tigo na voda kwa sasa).
Huyu bwana HTT alianza kwa style ya kununua kwanza,kisha anakungisha yaani aje ktk nyumba yako ninunue kisha nikupangishe ila yeye atahusika na usalama wa vifaa tu.
Walianza na tiGO hii case kisha wakaja vodaaa...mbeleni akaanza kujenga minara yake yeye HTT kisha kuwapangisha makampuni ya simu.
Inavyoonekana speed ya ujengani Minara hawa HTT si kubwa kulingana na mahitaji ya kampuni kusambaa ktk maeneo,kwa hiyo yapo maeneo tigo au voda atajenga mwenyewe minara kulingana na hitaji la hapo.
Ila hawa jamaa wa HTT kidogo wajanja ...at first walianza na hiyo style ya kununua tu na kumiliki kw usalama baadaye wakaomba kujipa task ya kumanage power ya site yaani wao wahusike kuprovide power on site licha ya ownership...hiyo outsoutce ikapita wale subcon wote wa power wakawa chini ya HTT kutoka makampuni ya tigo na voda....
Tender sasa ya HTT ikawa ni ownership na power supply.

Kwa gharama hizo 220 ni kidogo,ujenzi wa mnara ni shughuli pevu ndiyo maana serikali kupitia mfuko wake wa mawasiliano (UCAF) wanasaidia hili la kujenga minara na kutoa ruzuku kwa makampuni kwenda kuweka mawasiliano maeneo ya vijijini kwa kua kampuni zinakua haziko tayari kwenda kuwekeza 500mil hata ndani ya miezi sita 10ml mauzo hakuna.

Ahsanteni.
At least nimetoa mwanga fulani!
 
Nchi ya kila mtu mjuaji lakini ki ukweli wengi hamna kitu. Ningependa Mr President J P Magufuli awachape viboko hadi wakae sawa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…