- Thread starter
- #41
HTT (Helios Towers Tanzania) ni sehemu ya kampuni iitwayo Helio Towers Africa. Hawa jamaa wapo Ghana, DRC na South Africa. Makao makuu ya Helios yapo U.K
Excellent! Vodacom Tanzania ni kampuni Tanzu ya Vodafone kupitia tawi lake lililopo Afrika ya kusini--yaani Vodafone ambayo makao yake makuu yapo London, Uingereza. Kama nimekuelewa vizuri hii Kampuni HTT yenye kuuziwa minara Tanzania ambayo ndiyo huyu Vodacom kaiuzia minara ina Makao yake makuu London? INAONEKANA hawa jamaa wanafahamiana vizuri sana hawa.
Af inaonekana wewe jamaa uliyejipachika jina baya la Hater unajua mambo mengi sana wewe! Hebu tuone sasa nisaidie kujua Ni kina nani hasa wakurugenzi wa HTT? Vodafone ni Listed Public Liability London Stock Exhange nadhani. Swali? Nani hasa major Share holder wa HTT? Je, hakuna duplication ya interest katika Vodafone na HTT? Zama hapo tuone--ikibidi tuma mwambata wa Uchumi pale ubalozi wetu London atuambie kama hakuna duplication ya interests kati ya Vodafone na HTT tuone tunaibuka na lipi kujua hizi dola billioni moja za Vodacom zimezamishwa wapi hasa!