Mimi Yanga ila kwa mpira ule na Mbeya City tuombe Neema za Mungu tu

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,556
2,560
Hakika nisiwe mnafiki mimi kama mwanachama na mshabiki kindakindaki wa timu ya Wananchi au kwa jina lingine mabingwa wa kihistoria hadi dakika hii sijaona cha maana walichofanya timu yangu uwanjani.

Kuanzia kwenye muunganiko wa kikosi ni zero, fitness ya wachezaji zero, hakuna ubora wa kikosi zaidi ya kuona wakirukaruka tu.

Hakika Yanga yetu bado kabisa ina kazi kubwa sana ili kufikia ubora wa wapinzani wetu Msimbazi.

Angalizo: Hiki kikosi kikiendelea kucheza namna hii hakika nawaambia mwaka huu tunapigwa chuma 6 na Msimbazi.
 
Wanayanga mujitathmini kwa mara nyingine kuchukua ubingwa sidhani maana kwa ule mpira wa jana hakuna combination kabisa pale kati sasa sijui mkikutana na ihefu, mtibwa , kmc sijui mtakuwa kwenye hali gani
 
mimi naona simba ndio mbovu zaidi, pamoja na kucheza pamoja muda mrefu hakuna kitu, mechi na ihefu walibebwa na refa, juzi na mtibwa hakuna walichocheza mpira wa hovyo hovyo, bora yanga hawajakaa pamoja muda mrefu tuwape muda
Usiseme simba mbovu tusubili tare 20.09 uone Simba akiwa mkapa stadium anacho kifanya dhidi ya biashara nyie mkienda viwanja vibovu mnalalamika kwa nn jana mlishindwa kuonesha ubora wenu kwenye kiwanja safi
 
Mnapata tabu sana......
Iache tu Yanga...... Mwanzo mwisho timu inaspirit ya kuhitaji ushindi...... Mbumbumbu saizi hawezi kuelewa
 
Wanayanga mujitathmini kwa mara nyingine kuchukua ubingwa sidhani maana kwa ule mpira wa jana hakuna combination kabisa pale kati sasa sijui mkikutana na ihefu, mtibwa , kmc sijui mtakuwa kwenye hari gani
Kmc ndo hatuwawezi kabisa
 
Mnapata tabu sana......
Iache tu Yanga...... Mwanzo mwisho timu inaspirit ya kuhitaji ushindi...... Mbumbumbu saizi hawezi kuelewa
Spirit gani wewe mpira haueleweki na hapo ndo kiwanja kizuri je tukienda kwenye vumbi
 
Una jina zuri linafanana na klabu yetu pendwa sema ulikosea kushabikia mikia fc ulitakiwa ushabikia team wajina wako
 
Spirit gani wewe mpira haueleweki na hapo ndo kiwanja kizuri je tukienda kwenye vumbi
Tatizo mnaingia uwanjani na matokea sio kuangalia mpira.

Mpira wa jana ndio unaotakiwa kwenye ligi, timu zinapambana mwanzo mwisho.

Mbeya City kabadilika Sana mechi ya jana kacheza mpira mkubwa Sana.

Naamini marefa wakiwa wanachezesha kwa haki kama Jana tutakuwa ligi bora kabisa Tanzania.

Ndio maana hata Mbeya City walivyofungwa hujasikia malalamiko kama mikia FC wanavyolalamikiwa kwa kubebwa na marefa.
 
mimi naona simba ndio mbovu zaidi, pamoja na kucheza pamoja muda mrefu hakuna kitu, mechi na ihefu walibebwa na refa, juzi na mtibwa hakuna walichocheza mpira wa hovyo hovyo, bora yanga hawajakaa pamoja muda mrefu tuwape muda
Jana vyura wamebebwa sana na refa aibu,
 
Tatizo mnaingia uwanjani na matokea sio kuangalia mpira.

Mpira wa jana ndio unaotakiwa kwenye ligi, timu zinapambana mwanzo mwisho.
Mbeya city wabovu tu yaani ule ushindi wa jana nawewe ndo umeona ushindi tunaoutaka
 
Yaani ile timu sio kwa simba tu hata azam atatupiga nyingi

Sikubaliani na wewe! Timu iko vizuri sana ukilinganisha na misimu miwili iliyopita. Kinacho kosekana Yanga kwa sasa ni muunganiko wa timu kutokana na wachezaji wengi kuwa wapya, na pia baadhi yao kukosa utulivu na maamuzi ya haraka.

Lakini pia usisahau wachezaji wa timu nyingi ndogo wana desturi ya kukamia timu kubwa/kongwe ili kutengeneza majina na kusajiliwa baadae. Na hiki ndicho kilicho sababisha Prisons na hiyo Mbeya City kucheza mpira mkubwa dhidi ya Yanga, lakini walipocheza na KMC waliishia tu kufungwa.
 
Back
Top Bottom