Kwa nini Simba ilifungwa na Yanga

Observer2010

Senior Member
Oct 29, 2010
195
44
Nikiwa kama mtaalamu, mchambuzi na mwangalizi wa soka la kimataifa (International Observer), kiujumla huwa sitoi tathmini ya soka letu la kibongo kwa sababu kadhaa, ila wakati huu nimewiwa kuiongelea Simba Sports Club.Ukiangalia kwa undani mechi ya fainali na Yanga (CECAFA) utagundua hakika aliyestahili kushinda na alishinda, hapo Simba hawana haja ya kutafuta mchawi wala kumlaumu kocha.

Siandiki hivi kwa sababu nina mapenzi na Yanga, la hasha mimi hapa Tanzania ni mnazi mkubwa wa wana wa Msimbazi, na hili ndio hasa limenifanya niandike hivi. Sasa, kwanini Simba ilifungwa ? Walikosa malengo, ndio, walikosa malengo, mpira waliocheza ulikuwa hauna mpangilio kabisa, hii ilisababishwa na haya yafuatayo.
Katika soka popote duniani kuna basics za kitaalamu za kuiangalia timu na kuichambua ili kugundua udhaifu au ubora wa kikosi chake. Unapoangalia hili mara nyingi limekaa katika pande mbili, kuna ubora wa kimbinu au kimfumo hii inategemea sana na ubora wa kocha, na pia kuna ubora wa kiuchezaji hii inategemea aina ya wachezaji ulionao.

Timu yoyote ya soka huwa inajengwa na skeleton. Timu yoyote iliyo bora lazima iwe na skeleton iliyojengeka imara. Kwa faida ya wengi, skeleton ni nini ? Katika soka la kisasa, ukiondoa golikipa, ambaye umuhimu wake kila mmoja anajua, soka ina wachezaji 10, katika hawa 10, skeleton ya timu mara nyingi inajengwa na wachezaji 4. Timu iliyo imara sana inaweza ikajengwa na wachezaji zaidi ya hao ila katika basics, skeleton huwa inajengwa na wachezaji wanne. Wengine wanakuja kujaza nyama ya timu.

Ni wachezaji gani wanaojenga skeleton (hapa simzungumzii kabisa golikipa).

1. Central defender.
Hakuna timu duniani iliyopata kuwa bora bila ya kuwa na central defender mwenye uwezo mkubwa kabisa. Huyu ni mchezaji muhimu sana katika timu kwa maana ndiye kiongozi katika safu ya ulinzi. Huyu jamaa akitetereka timu lazima iyumbe. Simba kwa sasa hawana central defender wa maana.

2. Holding Midfielder.
Huyu ndiye mchezaji kiraka katika timu yoyote, yeye ndiye anayecover magap yote katika safu ya ulinzi na pia ndiye mpandishaji mpira kwenda mbele. Timu ikiwa haina holding midfielder mzuri hiyo timu lazima iwe na matobo. Simba haina holding midfielder wa maana.

3. Play Maker.
Huyu ni kiungo mchezesha timu, huyu ndiye mpishi mkuu wa mashambulizi ya timu. Uwezo wake mkubwa wa kutawanya mipira kwa wachezaji wake na uwezo wake wa kushambulia ndio nguzo kuu ya timu yoyote katika kusaka magoli. Timu yoyote yenye play maker bora kabisa huwa ni timu imara na yenye uwezo mkubwa wa kumiliki dimba la uwanja.

4. Striker.
Kama kuna tatizo kubwa kabisa la Simba basi ni hapa, simba ya sasa haina mshambuliaji wa maana kabisa. Kutokuwa na striker mwenye ubora ni sababu kubwa sana ya timu kucheza bila malengo. Timu yoyote iliyo bora huwa inahitaji kuwa na mshambuliaji wa kati mwenye uwezo wa kuscore. Musa Hassan Mgosi hakika amekuwa chini kabisa ya kiwango.Hawa wachezaji wanne ndio wanaofanya skeleton ya timu yoyote duniani, kukosekana kwa mmoja wao kati ya hawa au kutokuwa na kiwango cha kuridhisha kati ya mmoja wao kunafanya timu husika iwe katika matatizo sana. Ili mmoja wao akosekane basi inabidi wengine wafanye kazi ya ziada sana kuziba hilo pengo.

Kwa kutolea mifano unapozungumzia Simba bora kabisa kuwahi kutokea ilikuwa ni ya mwaka 1993 chini ya Abdalla Kibadeni Mputa na ile ya mwaka 1995 chini ya Dragan Popadic. Angalia Simba ya mwaka 1993, Central defender alikuwa Geogre Masatu, Holding midfielder alikuwa Hussein Marsha, Play maker alikuwa ni Ramadhan Lenny, huku ikiwa na striker pacha Edward Chumila na Malota Soma. Enzi hizo kukosekana kwa mmoja kati ya hawa ilikuwa Simba lazima itetereke.

Angalia Chelsea ya Morinho, ilikuwa na Central defender John Terry na Ricardo Calvalho, holding midfielder Claude Makerere, attacking midfielder Frank Lampard na striker Didier Drogba. Katika kikosi chochote ambacho Morinho alikuwa anapanga hawa watu ilikuwa lazima awapange, namba zingine alikuwa anaweza badili lakini hii skeleton ndio ilikuwa ya ushindi.

Man U iliyochukua treble 1999 ilikuwa na Jaap Stam, Roy Keane, Paul Scholes na striker pacha Dwight Yorke na Andy Cole.
Arsenal ya 2003/2004 iliyomaliza msimu bila kufungwa ilikuwa na Sol Campel, Gilberto Silva huyu jamaa washabiki wa Arsenal walikuwa wanamwita invisible wall, wakawa na Patrick Viera na striker Thiery Henry.

Hii ni mifano michache tu, ila ipo mingi sana.
Hivyo basi, Simba SC wanachotakiwa ni kutafuta wachezaji wenye ubora ili waweze kuunda hii skeleton imara, vinginevyo ubingwa na ushiriki wa michuano ya Afrika kwa mafanikio itakuwa ni ndoto.Cheers…
 
Back
Top Bottom